Wangwambo
Member
- May 22, 2020
- 20
- 14
Kumekuwa na taarifa zikiripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ya kwamba mfuko wa bima ya afya kukumbwa na changamoto mbalimbali za ukwasi, na hii inadhihirishwa na NHIF wenyewe walivyokuja na mwongozo kwa wanufaika wa idadi ya siku za kwenda kupata matibabu kwa mwezi na baada ya siku chache wakasitisha.
Wanachama wengi wa NHIF wamekuwa wakilalamika na hata kugombana na baadhi ya wahudumu wa hospitali hususani za private kwenye kipengele kidogo cha kujaza gharama za matibabu. Wahudumu wengi wanajaza baada ya mgonjwa kuondoka na haijulikani wanajaza kiasi gani hii hali inapelekea NHIF kuyumba kipesa.
Nchi yetu ina watalamu wengi sana wa mifumo, ningeshauri zile sms wanazotuma mara baada ya mnufaika kupata huduma basi ziambatane na bei husika iliyotumika, hii angalau inaweze ikasaidia kunusuru NHIF kufirisika.