DOKEZO NHIF wanataka kutuua na dawa za bei chee

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa Tanzania hivi karibuni umefanya marekebisho katika kifurushi chake kinachohusisha pia dawa, yakiwemo madawa ya antibiotic, ambapo imepunguza sana bei. Anaye command soko la dawa Tanzania ni NHIF. Na sasa hii ni RASMI kwamba soko la dawa litatawaliwa na makampuni ya dawa ya India, na hakika wameweza kutuletea dawa tunazozitaka. Ikumbukwe huko India kwa muda mrefu madaktari wao wanagoma kutoa dawa ze bei chee.

Kutegemea dawa za bei chee kutoka India, ambako kuna malalamiko mengi juu ya utengenezaji duni, kunakuja kuleta usugu wa antibiotics. Hebu fikiria NHIF wanataka walipe Antibiotic ya Ceftriaxone ya gramu moja kwa Tsh 1,300/=, wakati ukitaka Ceftriaxone ambayo inaweza kuwa bora, kwa bei ndogo, yamkini utapata ya Egypt, ambayo bei yake ya jumla haitopungua 9,000/=. Egypt ni kati ya nchi ambazo zina sheria kali za kuzalisha antibiotics. Wanataka kutuua hawa wandugu. Lakini nani alisema unapofanya costing uchukue the lowest?

Fikiria unanunua gari. Wakati unachagua gari ulikuwa ukitazama bei ndogo pekee bila kuzingatia historia ya gari husika, usalama, au jinsi linavyoaminika, unaweza kujikuta gari uliyonunua unatumia muda mwingi kwenye garage, au mbaya zaidi, inaweza kuharibika kipindi unaihitaji sana. Mfano huu unaweza kutumika kwa Tanzania ya sasa ya kutaka kupata dawa za bei chee, hasa antibiotics, ili kupunguza gharama za huduma ya afya.

Kwa kununua dawa kwa bei chee hasa antibiotics kutoka vyanzo vya uzalishaji visivyokuwa makini, kama baadhi ya wauzaji nchini India, Tanzania inachagua gari la bei ndogo bila kujali vitu vingine. Chaguo hili linaweza kuokoa pesa sasa, lakini linakuja na gharama zilizofichika ambazo zinaweza kuwa na madhara makubwa zaidi siku za usoni:

1. Ongezeko la Usugu wa Antibiotics: Kama vile gari la bei ndogo linavyoweza kushindwa kuwaka, antibiotics za bei chee zinaweza kushindwa kupambana na maambukizi. Bacteria wanaweza kuwa sugu kwa dawa hizi, ikimaanisha maambukizi ya kawaida ya bacteria yanaweza sababisha kifo kwa sababu antibiotics hazifanyi kazi.

2. Ubora wa Huduma ya Afya Hatarini: Kwa kuruhusu dawa duni kuingia sokoni, tunahatarisha afya na imani kwa mfumo wetu wa huduma ya afya. Ni kama kuwa na barabara zilizojaa na magari mabovu; hatimaye, usalama wa kila mtu unahatarishwa.

3. Gharama za Muda Mrefu: Kama vile gari la bei ndogo linavyokuwa ghali kutokana na matengenezo ya mara kwa mara, antibiotics duni zinaweza kusababisha magonjwa ya muda mrefu, matatizo makubwa zaidi ya afya, na gharama kubwa zaidi za huduma ya afya baadaye kwa sababu ya matibabu yasiyo na ufanisi na kuenea kwa bacteria sugu.

Kwa kifupi, ingawa ni muhimu kufanya huduma ya afya kuwa nafuu, ni muhimu pia kuhakikisha kwamba dawa tunazotumia ni salama, za ufanisi, na za ubora wa juu. Kuokoa pesa leo haipaswi kuja kutugharimu kesho. Kama ilivyo kwa magari, wakati mwingine bei chee huwa ghali zaidi baadaye.

Ccm ni wanyonya damu, mbwa kabisa,
 
Shida na kwa upande wa watoa huduma ipo, wanaweza kukupa dawa ya India lakini mfuko wa NHIF ukadaiwa bei ya dawa ya ujerumani. Mungu tuokoe waja wako kwani mboga na ugali vyote vya moto!
 
Unazijua bei za dawa za Ujerumani?...Umeziona bei za dawa za NHIF?...fanya homework yako usiwe mvivu...hilo fuko lenu haliwezi kulipa dawa ya Germany hata iwe Paracetamol
 
Kwenye Maandamani ya MWanza mww yenye mtoo ali andamana? kumbuka yalikuwa ya amani.

Sikiliza hizi kulalamika hazisaidii kitu, Watawala wanajua fika wanatawala aina gani ya Raia, watawala sio wajinga.
Sawa
 
Nchi tumejaa vilaza, tumejaza waogaa, wanafki, machawa wachumia tumbo acha hili dude linaloitwaa CCM litukomeshe tukiduwazwa na Aman ya kinafki!
 
Unazijua bei za dawa za Ujerumani?...Umeziona bei za dawa za NHIF?...fanya homework yako usiwe mvivu...hilo fuko lenu haliwezi kulipa dawa ya Germany hata iwe Paracetamol

Kuna haki na wajibu,
Je mkuu niny raia mkiambiwa mlipie 1M kwa bima ili mpate dawa za ujerumani mtaweza ?
 
Watanzania tulivyo mazuzu tumewaachia huu mjadala wamiliki wa vituo binafsi, tumenyamaza Kama vile haituhusu wakati ni afya zetu zinachezewa.
wadau wakubwa ambao ni wachangiaji, hawashirikishwi kwenye mazungumzo yanauofantika yakidaiwa kuwahusisha wadau. Wadau gani bila wanaowezesha uwepo wa mfuko?
 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa Tanzania hivi karibuni umefanya marekebisho katika kifurushi chake kinachohusisha pia dawa, yakiwemo madawa ya antibiotic, ambapo imepunguza sana bei. Anaye command soko la dawa Tanzania ni NHIF. Na sasa hii ni RASMI kwamba soko la dawa litatawaliwa na makampuni ya dawa ya India, na hakika wameweza kutuletea dawa tunazozitaka. Ikumbukwe huko India kwa muda mrefu madaktari wao wanagoma kutoa dawa ze bei chee.

Kutegemea dawa za bei chee kutoka India, ambako kuna malalamiko mengi juu ya utengenezaji duni, kunakuja kuleta usugu wa antibiotics. Hebu fikiria NHIF wanataka walipe Antibiotic ya Ceftriaxone ya gramu moja kwa Tsh 1,300/=, wakati ukitaka Ceftriaxone ambayo inaweza kuwa bora, kwa bei ndogo, yamkini utapata ya Egypt, ambayo bei yake ya jumla haitopungua 9,000/=. Egypt ni kati ya nchi ambazo zina sheria kali za kuzalisha antibiotics. Wanataka kutuua hawa wandugu. Lakini nani alisema unapofanya costing uchukue the lowest?

Fikiria unanunua gari. Wakati unachagua gari ulikuwa ukitazama bei ndogo pekee bila kuzingatia historia ya gari husika, usalama, au jinsi linavyoaminika, unaweza kujikuta gari uliyonunua unatumia muda mwingi kwenye garage, au mbaya zaidi, inaweza kuharibika kipindi unaihitaji sana. Mfano huu unaweza kutumika kwa Tanzania ya sasa ya kutaka kupata dawa za bei chee, hasa antibiotics, ili kupunguza gharama za huduma ya afya.

Kwa kununua dawa kwa bei chee hasa antibiotics kutoka vyanzo vya uzalishaji visivyokuwa makini, kama baadhi ya wauzaji nchini India, Tanzania inachagua gari la bei ndogo bila kujali vitu vingine. Chaguo hili linaweza kuokoa pesa sasa, lakini linakuja na gharama zilizofichika ambazo zinaweza kuwa na madhara makubwa zaidi siku za usoni:

1. Ongezeko la Usugu wa Antibiotics: Kama vile gari la bei ndogo linavyoweza kushindwa kuwaka, antibiotics za bei chee zinaweza kushindwa kupambana na maambukizi. Bacteria wanaweza kuwa sugu kwa dawa hizi, ikimaanisha maambukizi ya kawaida ya bacteria yanaweza sababisha kifo kwa sababu antibiotics hazifanyi kazi.

2. Ubora wa Huduma ya Afya Hatarini: Kwa kuruhusu dawa duni kuingia sokoni, tunahatarisha afya na imani kwa mfumo wetu wa huduma ya afya. Ni kama kuwa na barabara zilizojaa na magari mabovu; hatimaye, usalama wa kila mtu unahatarishwa.

3. Gharama za Muda Mrefu: Kama vile gari la bei ndogo linavyokuwa ghali kutokana na matengenezo ya mara kwa mara, antibiotics duni zinaweza kusababisha magonjwa ya muda mrefu, matatizo makubwa zaidi ya afya, na gharama kubwa zaidi za huduma ya afya baadaye kwa sababu ya matibabu yasiyo na ufanisi na kuenea kwa bacteria sugu.

Kwa kifupi, ingawa ni muhimu kufanya huduma ya afya kuwa nafuu, ni muhimu pia kuhakikisha kwamba dawa tunazotumia ni salama, za ufanisi, na za ubora wa juu. Kuokoa pesa leo haipaswi kuja kutugharimu kesho. Kama ilivyo kwa magari, wakati mwingine bei chee huwa ghali zaidi baadaye.

Nataka ifike mahali wote tuongee Lugha moja
 
Unachosema kina matter, ila angalia upande wa pili pia,
Tukisema tutoe dawa quality ya Egypt, eg ceftriaxone tuuze 15k, watu wetu wataweza mudu ? Kisha panaldo tuuze za 3000, tutaweza ?
Mana kama tukitaka dawa hizo ujue bei ya bima itakuja kuwa mtu mmoja 1M, ukienda hospital ukapewa dawa mbili jua bill ni laki na, je tutaweza ?

Usiseme tu kina Ummy wanaleta cheap drugs,
Wote tunataka kutibia Aga khan ila bill tunaweza ? Mana dispensary hizo ceftriaxone zinachomwa kwa 5k, ila bado 80% ya watu hawamudu kulipa full dose at once, sasa zikija hizo za 15k?

Anyway, tuendelee kwa sasa kutumia dawa za India na China, huku tukijenga uchumi imara ili tuweze tumia za Egypt
Ili swala la tutaweza huwa mnalitoa wapi??
Kwani mwananchi ndo anayetoa Pesa??

Bima inatakiwa Itumie hizo pesa inazokusanya kwa Faida ya Wananchi na sio kwa faida yao wenywe..
Na wakifanya hivyo vyote vinawezekana
 
Hili suala ndio wapinzani wanatakiwa walivalie njuga maana linamgusq mwananchi moja kwa moja
 
Watu wapo busy na simba na yanga na kusahau mambo Kama haya muhimu.
 
Ili swala la tutaweza huwa mnalitoa wapi??
Kwani mwananchi ndo anayetoa Pesa??

Bila inatakiwa Itumie hizo pesa inazokusanya kwa Faida ya Wananchi na sio kwa faida yao wenywe..
Na wakifanya hivyo vyote vinawezekana
Sasa unataka kutoa 192k kisha utibiwe kwa dawa za ujerumani ? Uwe unafikiri na wew,

Wafanyakazi eg wanaolipwa 1M wanalipa 300k kisha wanaongezewa 300k na serikali, jumla 600k kwa watu 6, kwa kiasi hicho unataka kutibiwa kwa dawa za mjerumani ambapo panaldo ni 10K ?
 
swala la dawa ni kamba. medicine is cheap sana. especially in India. in western countries expensive sababu ya labour cost. also ceftriaxone ni ceftriaxone. acheni kudanganywa kuwa ya Germany sijui Egypt is better that any other. biggest lies ever.

funny side all African and Europe countries go to India for medical tourism. hii kamba kubwa sana
 
Jana Mtoto wa rafiki yangu alienda hospital ya Private hapa Mwanza alipimwa Damu na choo lakini Mkojo walikataa na fun enough alikutwa na Malaria na minyoo lakini wakasema akanunue dawa maana dawa zilizopo hazilipiwi na NHIF Huyu Ummy Mwalimu anafanya nini mpaka leo ofisini na Mama Samia ameamumua kunymazia ? Hajui tunaingia kwenye uchaguzi atawaambia nini wananchi ambao wengi wameathirika na kufutwa kwa kifurushi cha toto Card kwa watoto ?
mimi mwenyewe simwelewi waziri na RAIS .sijui wanawaza kushinda uchaguzi kwa mabavu?
 
swala la sawa ni kamba. medicine is cheap sana. especially in India. in western countries expensive sababu ya labour cost. also ceftriaxone ni ceftriaxone. acheni kudanganywa kuwa ya Germany sijui Egypt is better that any other. biggest lies ever.

funny side all African and Europe countries go to India for medical tourism. hii kamba kubwa sana
Hii kawaambie mafala...
FYI humu jamvini kuna mapapa wa knowledge.
 
Jana Mtoto wa rafiki yangu alienda hospital ya Private hapa Mwanza alipimwa Damu na choo lakini Mkojo walikataa na fun enough alikutwa na Malaria na minyoo lakini wakasema akanunue dawa maana dawa zilizopo hazilipiwi na NHIF Huyu Ummy Mwalimu anafanya nini mpaka leo ofisini na Mama Samia ameamumua kunymazia ? Hajui tunaingia kwenye uchaguzi atawaambia nini wananchi ambao wengi wameathirika na kufutwa kwa kifurushi cha toto Card kwa watoto ?
Rais mambo ya namna hii huwa hapendi ...muacheni
 
Shida na kwa upande wa watoa huduma ipo, wanaweza kukupa dawa ya India lakini mfuko wa NHIF ukadaiwa bei ya dawa ya ujerumani. Mungu tuokoe waja wako kwani mboga na ugali vyote vya moto!
NHIF wao kwenye service portal wameseti kila kitu automatically.

Bei ya dawa imesetiwa, mfano Cough syrup 1,300/=. Sasa wewe mto huduma unaweza kuwa na dawa za Cough syrup brand tofauti tofauti ambapo bei pia ni tofauti.

Ukimpa mgonjwa dawa ya 3,000/=, kule kwenye portal ukiingiza hilo jina la dawa uliyotoa(hapa jina ni moja tu, Generic name lililosetiwa), bei itasoma 1,300/= ambayo utalipwa.

Sasa huoni unapata hasara?

Dawa za kutoka Ujerumani ndio zina bei kubwa, wewe ukiwa unawapa wagonjwa hizo dawa halafu utegemee kulipwa na NHIF unakula hasara mbaya sana.

Ili mtoa huduma aepuke hiyo hasara atalazimilika kutoa dawa za kutoka India ambazo ni bei chee halafu ubora mdogo.
 
Back
Top Bottom