NHIF wao kwenye service portal wameseti kila kitu automatically.
Bei ya dawa imesetiwa, mfano Cough syrup 1,300/=. Sasa wewe mto huduma unaweza kuwa na dawa za Cough syrup brand tofauti tofauti ambapo bei pia ni tofauti.
Ukimpa mgonjwa dawa ya 3,000/=, kule kwenye portal ukiingiza hilo jina la dawa uliyotoa(hapa jina ni moja tu, Generic name lililosetiwa), bei itasoma 1,300/= ambayo utalipwa.
Sasa huoni unapata hasara?
Dawa za kutoka Ujerumani ndio zina bei kubwa, wewe ukiwa unawapa wagonjwa hizo dawa halafu utegemee kulipwa na NHIF unakula hasara mbaya sana.
Ili mtoa huduma aepuke hiyo hasara atalazimilika kutoa dawa za kutoka India ambazo ni bei chee halafu ubora mdogo.