NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "TOTO Afya Kadi". NHIF yadai hawajafuta ila wameboresha

Hivyo vifurushi bei umeziona? Zinaendana na maisha ya Mtanzania? Si kwamba watu hawataki kulipia huduma ila hawana kipato.
 
Mfuko haujaacha kusajili watoto na bima ya afya. Utaratibu wa kusajili watoto unaendelea kupitia familia au shule wanazosoma.
Tuache muvi za kidosi. Shule za Kayumba nani anaweza kumchangia mapema sh 50,400 ili kundi likusanye pesa nyingi zilipwe bima? Kwa nini mfuko isiwe tayari kupokea fedha ya mtoto sliye tayari kwa Sasa kuliko kusubiri kundi la watoto 800 sule ya msingi x
 
Wee nawe hebu tulia huko
 
Watajiunga na nini, wanapesa labda wawafunge kamba, mtu kwa siku anaishi chini ya dola mbili, sembuse bima ya familia sh 900,000
Kwa ufupi ni kwamba wanaweka bima kwa wote kupitia mlango wa nyuma.
Lazima wazazi wajiunge ili mtoto apate bima
 
Hayo maboresho yatatumia muda gani kukamilika?

Mmeshawafikiria maskini waliokuwa wanaona Hilo ndio kimbilio lao?

Mmeshindwaje kufanya maboresho huku huduma zinaendelea?
Ni wahuni tu. Wanachukulia poa watoto wao wanatibiwa wa wenzao wawasitishie huduma. Nonsense.
 
Wameepusha ubaguzi ... saivi kata familia tu ... watoto kwa 50,400 unapata huduma mpaka milioni 20, we ulisikia wapi duniani. Okoa mfuko
Still sio solution kwa sababu ya affordability, simply wangeongeza bei ya bidhaa zisizo lazima bia, sigara, na zifananazo kuwapa majority insurance cover
 
Fine, ila wa chuo na shule ni TZS.50,400/- unasemaje kuhusu umri nao ni under 18yrs?
Hivyo ni vifirushi viwili tofauti acha ubishi boss. Hiki ni kifurushi cha mwanafunzi kile ni toto afya ila bei zilikuwa sawa. Bei kuwa sawa haimaanishi ni kitu kimoja, sawa mkuu. Kifurushi cha mwanafunzi hakisubiri 3 months kama toto afya na hakijafutwa sema wamekiboresha kwakufanya wanafunzi wavyuo na sasa washule yaani primary na secondary kuingia kupitia shule na vyuo vyao.
 
Wameepusha ubaguzi ... saivi kata familia tu ... watoto kwa 50,400 unapata huduma mpaka milioni 20, we ulisikia wapi duniani. Okoa mfuko
mfuko umejaa wezi na wapigaji wa fedha za wananchi maskini..
 
Sio wote, sema maskini
 
Wanywa bia lazima tupungue mwaka huu na nyumba za ibada zijae waumini. Kuna jamaa hapa kaanzisha mradi wa majeneza .Kufa kufaana kudadeki
 
Asanteni NHIF mi nimependa sana utaratibu wenu wa watoto kusajiliwa kupitia shule wanazosoma aisee hii imetulia kwanza mmetuondolea usumbufu wa kufuata hiyo huduma mjini sisi tuta dili na walimu wakuuu mashuleni kwetu
nawahurumia NHIF kukulipa mtu takataka Kama wewe, kwa propaganda za aina hii, utafikiri watu ni wajinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…