Huu ni uthibitisho mwingine haya mashirika yanaenda kufa, serikali inachota pesa kwenye hiyo mifuko halafu hawarudishi kwa wakati, sasa haya mashirika yameanza kulemewa na gharama za uendeshaji ndio maana kila siku wanapunguza huduma walizokuwa wanazitoa mwanzo ili kujaribu kuendelea kujiendesha, lakini hili halitasaidia, serikali inahusika moja kwa moja kwenye hili.
CCM haistahili tena kupata kura za mtanzania yeyote mwenye uchungu na nchi hii, au wananchi wanyonge wa nchi yetu, wanastahili kuondoka madarakani sasa, wamefeli, tuwaondoe mapema kabla hawajaharibu zaidi.