NHIF yaja na makali zaidi kwa Watanzania, yaondoa dawa lukuki kwenye orodha ya dawa zinazonufaika na malipo ya bima

NHIF yaja na makali zaidi kwa Watanzania, yaondoa dawa lukuki kwenye orodha ya dawa zinazonufaika na malipo ya bima

Status
Not open for further replies.
Kuwa mkweli utawala huu haufanyi vizuri kwenye hili. Unataka kuniambia miaka kumi ya Kikwete na kumi ya Mkapa huu utamaduni wa kuugua watu hawakuwanao? Raising wenu ameweka nguvu kwenye shughuli zinazohusu saruji tu.
Akili yako umeshindwa kujua kuwa mfuko wa Bima unapata Pesa kutoka kwenye mishahara ya wafanyakazi kati ya asililimia 3 au 6 kama sijakosea. Mishahara hii haijabadilika kwa miaka 5. Hivyo mfuko umeendelea kupata kiwango kile kile huku wategemezi wakiongezeka. Mfano aliyekuwa kapera kaoa na kupata watoto wawili. Hapo watu watatu wameongezeka bila kuongea gharama za uchangiaji. Hali kama hii lazima itaathiri mifuko yote pamoja na huu wa Bima.
Yote hayo ndui maana tunasema Uhuru,haki na maendeleo.
 
Huu ni uthibitisho mwingine haya mashirika yanaenda kufa, serikali inachota pesa kwenye hiyo mifuko halafu hawarudishi kwa wakati, sasa haya mashirika yameanza kulemewa na gharama za uendeshaji ndio maana kila siku wanapunguza huduma walizokuwa wanazitoa mwanzo ili kujaribu kuendelea kujiendesha, lakini hili halitasaidia, serikali inahusika moja kwa moja kwenye hili.

CCM haistahili tena kupata kura za mtanzania yeyote mwenye uchungu na nchi hii, au wananchi wanyonge wa nchi yetu, wanastahili kuondoka madarakani sasa, wamefeli, tuwaondoe mapema kabla hawajaharibu zaidi.
Tutaichagua CCM maana Chadema ni waongo sana, walishachukua advance ya kuuza nchi
 
Jumla ya dawa 138 zimeondolewa ktk bima ya afya kuanzia September 1,2020. Tazama dawa zilizoondolewa hapa
IMG_20200904_161755.jpg
 
Nadhani swali la maana zaidi ni Kwanini ?, Kabla hatujahukumu...
 
Bima ya afya, NHIF imezidi kuondoa madawa muhimu kwenye orodha ya madawa yanayolipiwa na mfuko huo wa bima.

Sasa dawa nyingi itabidi wanufaika wa mfuko huo wajinunulie kwa pesa tasilimu.

Kinachoendelea sasa NHIF watakua wanalipia panadol tu.
20200904_164902.jpg
 
Bima ya afya, NHIF imezidi kuondoa madawa muhimu kwenye orodha ya madawa yanayolipiwa na mfuko huo wa bima.

Sasa dawa nyingi itabidi wanufaika wa mfuko huo wajinunulie kwa pesa tasilimu.

Kinachoendelea sasa NHIF watakua wanalipia panadol tu.View attachment 1558337
Mada chochezi hii, wazijua dawa muhimu wewe? Tafuta zinaitwa TRACE MEDICINE, humo hakuna hata moja zote hizi zina mbadala wake au sio common katika mazingira ya walio wengi labda private ndio huzitumia sana
 
Sasa kuna umuhimu ggani wa kuwa na bima ya afya kama dawa muhimu unatoa badala ya kuongeza huduma.

Yaani wanajitengenezea njiaa za kuwaibia wanachama

Ccm ipumzishwe
 
Mada chochezi hii, wazijua dawa muhimu wewe? Tafuta zinaitwa TRACE MEDICINE, humo hakuna hata moja zote hizi zina mbadala wake au sio common katika mazingira ya walio wengi labda private ndio huzitumia sana
Kwahiyo aliyeandika kakurupuka?
 
Mada chochezi hii, wazijua dawa muhimu wewe? Tafuta zinaitwa TRACE MEDICINE, humo hakuna hata moja zote hizi zina mbadala wake au sio common katika mazingira ya walio wengi labda private ndio huzitumia sana
Kwamba watu wanaotibiwa private wana magonjwa tofauti na wanaotibiwa serikalini hadi wao wawe wanatumia hizo dawa sana kuliko hospitali za serikali?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom