NHIF yakusudia kusitisha Mkataba wa Huduma kwa Hospitali za APHTA Ikiwemo Aghakani na TMJ

NHIF yakusudia kusitisha Mkataba wa Huduma kwa Hospitali za APHTA Ikiwemo Aghakani na TMJ

Labda in confidence ila si kwauzi hivi maana watu hawana uelewa wa mambo mengi.
Ni sawa maana Kuhusu Bei Wamepunguza bila kuangalia Soko! (Japo wanasema wameangalia soko)
Kuhusu huduma, baadhi wamechinja sana ila zingine wamerudisha bei zake nyuma
 
KIufupi hili ndo walilokuwa wanalitaka Hospitali binafsi kwa sababu lilikuwa likiwakata sana
Lilikua likiwakata wapi wakati walikua wanauibia mfuko,wanakusainisha zile fomu kabla hawajakupa huduma Kisha wanaandika gharama za juu
 
Lilikua likiwakata wapi wakati walikua wanauibia mfuko,wanakusainisha zile fomu kabla hawajakupa huduma Kisha wanaandika gharama za juu
Hili jambo sio la kweli..
Kwanini Usikague huduma ulizopatiwa kabla ya kusaini..
Na sasa hivi kusaini ni kwa njia ya digitali kwa nini usikatae uwaambie huduma mlizonipa sio mlizoandika..?
Hakuna anayeweza kukusainisha formu ikiwa haijaandikwa kitu lbda kama Hospitali za serkali..
 
DAWA YA MOTO NI MOTO. AGHA KHAN ITAKUFA, wanachuo wote wanatibiwa in those hospitals. Let’s wait and see who wins.

They actually create a fear vacuum. If you act we act.
Tangu lini Agha khan wakategemea bima.....?
 
Umeelewa nilichokiandika boss au unaandika kwa mihemuko, unaambiwa kusitisha huduma kwa wateja wa NHIF ni direct inflict inayopelekea kuvunja mkataba. Hospitali zote ulizoziona zilisitisha huduma mpaka settlement ipatikane ila mkataba hauruhusu hicho kitu ndio maana mkataba unavunjwa automatically.
Mkataba unavunjika pale usipolipa hela

Serikali ilianza kuvuunja yenyewe kwa kutowalipa watu hela zao

Wamesitisha huduma baada ya kutolipwa

Wewe hunilipi,hela za kutolea huduma nazitoa wapi?

Automatically mkataba unajivunja wenyewe...maana hakuna hela,nitakupa dawa gani ndugu?

Hebu acha ukichaa
 
Hawezi kufanya hivyo kwasababu leseni yake ya kuendesha hospitali haimruhusu hivyo. Hapo sio NHIF tena bali wizara ya afya.
Hela inaangalia leseni?

Unajua nyie serikali ni vichaa ujue!

Yaani wewe hela ya kuleta dawa hakuna,dawa nitoe wapi?

Njoo ukae hapo barazani,sikupi huduma!

Utakua ni mkataba wa wizi huo

Yaani mkataba wa kusema toa huduma tu hata nisipokua hela maana yake ni mkataba wa wizi wa kuniibia na ni badili to begin with.

Hakuna mkataba wa namna hiyo

Hospitali binafsi zisikae zifanye biashara na serikali maana ni WEZI

Never againa,piga chini hawa takataka majambazi kabisa
 
Serikali iliyojaa watendaji wenye uelewa mdogo.
Ccm oyeeeeee.
Kwani kati ya Secta binafsi na Wao Nani anahitaji mwenzake.
Akili za akina Steven Wasira bhana.

Serikali hamjiwezi hata kidogo,hata hivyo mtakuwa mmeamua kuwakomesha watumishi wenu wenyewe.
Kwa vile ni Maiti zinazotembea Wala hazitajali zitaona yote sawa.
Kenya wamefanya maandamano ya kuishinikiza Serikali Yao iajili watumishi Kwa maana wapo wachache.
Ila huku hutakuja kuona.Sijui labda Kwa vile kazi wanapeana KINDUGU.
Wanaogopa kukasirishana ndugu😅😅.Nchi hii ngumu.

Sisi Walala hoi,miaka nenda Rudi Hospitalini tunalipa keshi in hands.

Sasa nyie watoto wa mama,subirini.🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hili jambo sio la kweli..
Kwanini Usikague huduma ulizopatiwa kabla ya kusaini..
Na sasa hivi kusaini ni kwa njia ya digitali kwa nini usikatae uwaambie huduma mlizonipa sio mlizoandika..?
Hakuna anayeweza kukusainisha formu ikiwa haijaandikwa kitu lbda kama Hospitali za serkali..
Hivi ni kweli mtanzania kaenda hospital anaambiwanna daktari Saini hapa hatosaini!!?..Mimi mwenyewe nishasainishwa Sana na nimeanza kutumia nhif 2002 huko
 
Hivi ni kweli mtanzania kaenda hospital anaambiwanna daktari Saini hapa hatosaini!!?..Mimi mwenyewe nishasainishwa Sana na nimeanza kutumia nhif 2002 huko
Mzee mwaka 2002 NHIF ilikuwa inapokea mapingamizi makubwa sana japo kwenye mwezi Wa saba hivi ndo sheria ikatungwa kuwa Kila mtumishi wa serkali akatwe NHIF..

Kwahyo NHIF rasmi imesimama kuanza kutoa huduma mwaka 2003..

Daktari ndo anamsainisha Formu Mgonjwa?
Mzee hebu kuwa serious bhasi watu wa mapokezi na Dirisha la dawa na dirisha la Mauzo wanafanya kazi gani??
 
Mkataba unavunjika pale usipolipa hela

Serikali ilianza kuvuunja yenyewe kwa kutowalipa watu hela zao

Wamesitisha huduma baada ya kutolipwa

Wewe hunilipi,hela za kutolea huduma nazitoa wapi?

Automatically mkataba unajivunja wenyewe...maana hakuna hela,nitakupa dawa gani ndugu?

Hebu acha ukichaa
Kama hawakulipwa pesa wanaruhusa ya kwenda mahakamani, natumai hujawahi kuuona mkataba wa bima wa afya na hospitali ulivyo. Usibuni vitu usivyovijua boss.
 
Hela inaangalia leseni?

Unajua nyie serikali ni vichaa ujue!

Yaani wewe hela ya kuleta dawa hakuna,dawa nitoe wapi?

Njoo ukae hapo barazani,sikupi huduma!

Utakua ni mkataba wa wizi huo

Yaani mkataba wa kusema toa huduma tu hata nisipokua hela maana yake ni mkataba wa wizi wa kuniibia na ni badili to begin with.

Hakuna mkataba wa namna hiyo

Hospitali binafsi zisikae zifanye biashara na serikali maana ni WEZI

Never againa,piga chini hawa takataka majambazi kabisa
Sasa vunja leseni ndiyo ujue kwanini kuanzia biashara mpaka daktari anapewa leseni. Afya sio biashara ndugu na mkataba hauvunjwi hivyo boss lasivyo ungejua kwanini kuna faini kama ukivunja mkataba bila kufuata utaratibu. Medicine sio biashara ya vitu, shika hilo kwanza.
 
Watu wanaotumia NHIF ndio watakaoumia.....Hii bima ni takataka kitambo sana...
Isitoshe Agakhan walikuwa hawaitaki...Pole sana wanachama...
Kama huna changamoto za kiafya utaita NHIF takataka. Sisi wengine NHIF ndiyo kila kitu katika maisha
 
Mbona km barua imekuwa addressed kwa TMJ, halafu title inasema Agakhan?!
Au mimi ndiyo sijaelewa?
 
Wait and see . Wait and see . Very different economic generations
. No one is paying 100k-200k per treatment . Every month for the rest of the life . In this economy . Also the lack of funds forced them to accept the insurance
Unajua wagonjwa wanaotibiwa Agakhan wewe?
 
Jibu lako linaweza lisiwe sahihi sana. AGHA KHAN bei za za matibabu ziko juu sana ukilinganisha na hospitali nyingi achilia mbali za umma. Hivyo watu wengi waliokuwa wanatibiwa huko ni wale wa NHiF. Na kuna kamchezo ka kupandisha bei kwenye Bill zao. Hivyo kuwa kosa wateja wa NHiF ubaridi utawaingia kama si kutetemeka. No matter how big their
Bei za matibabu ziko juu lakini na huduma ni nzuri pia ukilinganisha na hospital nyingine.
 
Mkuu

Kodi hata ukirudisha walipie,ultimately inabebwa kama ilivyo inawekwa kwenye invoice za wananchi wanalipia wao,sio hizi hospitali

Unakuja na hoja ya kifala sana ya kodi as if kodi wanatoa wao,wanatoa wananchi..

Hakuna hospitali linalipa kodi,unalipia wewe wewe kiazi mwananchi uliechagua mawanasiasa mapumbavu eti yakutibu

Hayo mawanasiasa mliyoyachagua yawatibu,basi nendeni yawatibu kama yanaweza

Msililalamikie hizi hospitali....zinafanya biashara,huwezi bei tambaa

Na ukija na ujinga wa kodi,no sweat,bring it on,wanazihamishia kwa wananchi right away ndio walipie bei ya sindano inakuwa 1,000,000...mfe kabisa!

Ni ajabu sana mwanadamu unakuja hapa duniani unashindwa kujitunzia pesa zako ili ukiumwa utijibie,eti unampa mwanasiasa akushikie kama litoto lidogo ili ukiumwa likakutibie,cha ajabu linakula hizo pesa then ukiumwa badala ya kulalamikia aliekushikia hela unamlalamikia mtoa huduma

The problem here cha kwanza ni mwananchi,wa pili ambae ndio alieharibu kila kitu ni serikali....wewe mwananchi unampaje serikali akushikie hela?Umekua mtoto mdogo?Lazima mfe wote
Facts hizi. Akili za ujamaa ndio zinaua hii nchi. Kila kitu serikali fanya hiki
 
Kuanzia leo tar.1 March 2024, vituo binafsi vya huduma za afya nchini vimekubaliana kutokupokea wateja wa NHIF. Maana yake ni kwamba wagonjwa wanaotibiwa kwa NHIF wako hatarini kukosa huduma. Kumbuka, takwimu zinaonesha zaidi ya 80% ya wagonjwa mahospitalini ni wanachama wa NHIF. Ni chini ya 20% tu ndio wanaotumia bima za makampuni binafsi au kujilipia cash. Kwahiyo 80% ya wagonjwa wote nchini hawajui hatma zao.

KIINI CHA MGOGORO
Kiini cha mgogoro ni vifurushi vipya vilivyopendekezwa na NHIF kwenye utoaji huduma. Vifurushi hivyo vimepunguza bei kwenye huduma nyingi na za msingi na vimeongeza bei kwenye huduma chache na zisizotumika mara kwa mara.

Kwa mfano, huduma ya kujifungua kwa upasuaji (C-section) bei imepunguzwa kutoka 300,000/= hadi 220,000/= tu. Vituo binafsi vimesema haviwezi kutoa huduma kwa bei hii. Procedure kama hii inahitaji timu ya watu angalau 6 au zaidi. OBGY, Assistant Surgeon, Anesthetist, Surgical Technologist, Delivery Nurse, Supporying staff. Hapo bado vifaa tiba kama mitungi ya Oxygen, sindano, madawa, nyuzi, gauze etc. Sasa kwa 220K utafanyia nini? Utanunua gauze? utamlipa daktari? utalipia umeme? utanunua vifaa tiba? Utalipia Oxygen?

Ikumbukwe hata 300,000/= iliyokuwa inatolewa awali bado ilikua haitoshi. Maana yake ni kwamba vituo binafsi vilikua vinatumia rasilimali zake za ndani kuongezea kwenye kiasi kinachotolewa na NHIF ili mama mjamzito asikose huduma. Hii inaitwa Corporate Social Responsibility. Yani unachukua faida kidogo unayopata kwenye huduma zingine, una-topup kwenye huduma ambazo hazina fungu la kutosha. Hospitali nyingi binafsi zinafanya hivyo. Sasa unapokuja kushusha tena kutika 300K hadi 220K unataka hospitali zijiendesheje?

Hakuna hospitali itakubali kufanya hii procedure. Unless otherwise wacompromise quality na kufanya procedure ambayo ni substandard. Yani badala ya chumba cha upasuaji kuwa na wataalamu 6 wawe watatu. Badala ya kumtumia Anasthesiologist atumike Nurse. Badala ya kutumia mashine ya Oxygen, wafungue madirisha ??. Inachekesha lakini huku ndipo serikali dhaifu ya CCM inapotaka kutupekeka. Na mwisho wa siku muathirika ni mwananchi maskini. Hawa ndio watafia kwenye vitanda vya upasuaji. Hao viongozi walioshusha bei wao hata wakiugua malaria, wanaenda India.

MAPITIO YA VIFURUSHI YALIFANYIKA LINI MARA YA MWISHO?
Mara ya mwisho bei za vifurushi vya NHIF zilipitiwa mwaka 2016. Kwahiyo hadi leo ni miaka 8 imepita. Sasa jiulize miaka 8 gharama za maisha zinapanda au zinashuka? Kama mwaka 2016 NHIF ilikua inalipa 300K kujifungua kwa upasuaji, kwanini leo wanataka kulipa 220K? Yani kila kitu kimepanda, halafu wewe unashusha bei?. Oxygen imepanda, bei ya gauze imepanda, madawa yamepanda, umeme umepanda, vifaa tiba vimepanda. Hata gharama za kuwalipa watoa huduma zimepanda. Msingi wa kushusha bei unatoka wapi? Nilitegemea baada ya miaka 8 NHIF iongeze fungu kwenye huduma, na sio kushusha.

Nimetolea mfano mmoja wa C-section, lakini huduma nyingi zimeshushwa bei. Kwa mfano ukivunjika NHIF watakulipia 12,000/= tu kuwekewa POP. Maana yake ni kwamba ukikuta gharama za POP ni 50,000/= utalazimika kuongezea 38,000/= kutoka mfukoni kwako, maana NHIF watakulipia 12,000/= tu.

Zipo huduma chache zimepandishwa (eg Consultation kwa Specialist) lakini nyingi zimeshushwa bei. Na hiki ndio kiini cha mgogoro wa serikali na hospitali binafsi. Ikumbukwe kwamba hospitali za serikali zinapewa ruzuku, kwahiyo haziwezi kulalamika hata kama zinaumia. Lakini hospitali binafsi zina haki ya kulalamika maana hazipewi ruzuku.

Na hizi binafsii zimegawanyika makundi mawili. Zile za mashirika ya dini na zile binafsi kabisa. Zile za mashirika ya dini angalau zinasamehewa kodi. Lakini hizi binafsi kabisa zinatozwa kodi maana zinaambiwa zinafanya biashara. Na ukihesabu wanalipa jumla ya kodi 32 kuanzia kodi za TRA, Halmashauri, mabaraza mbalimbali, TBS, NEMC, OSHA, TMDA etc.

Sasa jiulize mtu analipa kodi 32 kwenye serikali yako, halafu unataka afanye C-section kwa 220K kweli? Hiyohiyo alipe mishahara, ununue umeme, maji, vifaa tiba na bado alipe kodi zote 32 kwenye hela hiyohiyo? Mna wazimu?

Ikumbukwe NHIF ilileta mapendekezo ya vifurushi hivi December mwaka jana, wadau wakavikataa. Kamati ya bunge ya afya na masuala ya ULIMWI ikaingilia kati, ikasema vifurushi vya zamani viendelee kutumika wakati hivi vipya vikifanyiwa marekebisho. Bunge likaagiza iundwe kamati ya kupitia upya vifurushi hivyo itakayoshirikisha wizara, NHIF na watoa huduma, kwa maana ya hospitali za umma na zile za binafsi.

Lakini hospitali binafsi hazikushirkishwa. Kamati iliyoundwa ilihusisha wataalamu wa wizara, TIRA na NHIF tu. Mathalani Sekretarieti yote ya Kamati iliundwa na wajumbe kutoka NHIF tu. Maana yake ni kwamba NHIF waligeuka mahakimu kwenye kesi yao wenyewe, contrary to cardinal principles of Law. Kwahiyo NHIF walizuga kufanya review na kurudi na bei zilezile za awali zilizokataliwa na wadau, japo walifanya marekebisho kidogo sana.

Lakini wadau wa sekta binafsi kwa maana ya APHTA, CSSC na BAKWATA hawakushirikishwa kuunda Kamati, badala yakewaliitwa kwenye kikao cha wizara tar.19 February 2024 kwenda kuelezwa kile ambacho kamati imeamua. Hapa maamuzi ya bunge yalipuuzwa.

Lakini pia bunge lilizuia bei mpya kuanza kutumika mpaka pale sheria iliyoanzisha NHIF itakapopitiwa upya na kufanyiwa marekebisho ili kuaccomodate watoa huduma binafsi. Lakini sheria bado haijapelekwa bungeni ili kufanyiwa marekebisho, tayari NHIF inalazimisha bei mpya zianze kutimika leo. Huku ni kulidharau bunge kwa viwango vya juu.

Kwanini NHIF wanashinikiza bei mpya zitumike haraka haraka? Ni kwa sababu mfuko upo hoi bin taabani na unakaribia kufilisika. Kwa akili zao "finyu" wanadhani bei za huduma ndio zinafanya mfuko ufilisike, ndio maana wanajarjbu kuzipunguza. Lakini si kweli. Hata wapunguze bei, kama hawatashughulikia chanzo cha tatizo bado mfuko utafilisika tu.

CHANZO CHA NHIF KUYUMBA KIFEDHA
1. Fedha za NHIF kutotumika sawa na makusudio. Ripoti ya CAG ya mwaka 2022 inaonesha kuwa wanafanyakazi wa NHIF wamekopeshana zaidi ya Bilioni 41 ambazo ni michango ya wanachama. Yani unakatwa pesa kwenye mshahara wako ili ukiugua utibiwe, kumbe mmewapa watu mtaji wa kukopesha bila riba. Yani wamegeuza mfuko kuwa KIKOBA, halafu haohao leo wanashanga kwanini mfuko unafilisika? ??

2. Serikali kutoa huduma bure kwa wazee bila kufidia gaharama. Sera ya wazee kutibiwa bure ni nzuri sana. Lakini serikali inatakiwa kufidia gharama. Kwa mfano mzee akienda hospitali kutibiwa macho. Gharama zake zikawa 50,000/=. NHIF wanamlipia huyu mzee. Lakini serikali haitoi fedha kurudisha NHIF. Hii ni moja ya sababu ya huu mfuko kufilisika, hata ripoti ya CAG imeeleza kuwa seeikali inadaiwa na NHIF.

3. Centralization ya huduma za bima ya afya kwa watumishi wa umma. Zamani baadhi ya tasisi za serikali ziliruhusiwa kuwa na bima binafsi. Baadhi ya taasisi hizo kama BOT, NSSF, TRA, TANAPA, TANROADS, TANESCO etc zilikua zinatumia bima za makampuni binafsi kama AAR (currently Assemble), Jubilee, Strategies, etc. Lakini Magufuli akalazimisha watumishi wote wa umma kutumia NHIF. Na hapa ndipo mfuko ulipozidiwa., kwa sababu wengi walipohamia NHIF ilibidi watengenezewe vifurushi vyao vya VIP ili kuendana na huduma za kule walikotoka. Matokeo yake NHIF ikawa na mzigo mkubwa uliowashinda kubeba.

UJINGA WA SERIKALI
Jana baada ya hospitali binafsi zote kupitia umoja wao wa APHTA, kutangaza hazitapokea wagonjwa wa NHIF, tulitegemea serikali itakaa nao chini kutafuta suluhu kwa maslahi mapana ya afya za watanzania. Lakini mtu mmoja akaniambia ukitaka kujua serikali ina watu wajinga, wataanza kuzitisha hospitali binafsi na kuzifanyia surbotage ili kulazimisha zitoe huduma kwa bei zilizopendekezwa na NHIF.

Na hiki ndicho kilichotokea. Leo serikali imetoa onyo kwa hospitali za Agha Khan, Kairuki na Regency kwamba eti zinakiuka mkataba baina yao na NHIF. Kumbuka tamko la APHTA jana lilisema hospitali zote binafsi zitasitisha huduma leo. Sasa kwanini zitishwe hizo tatu tu? Hapa lengo ni devide and rule theory. Wakizitisha hizi hospitali kubwa wanajua nyingine zitafyata mkia. Yani ukiona Agha Khan ametishiwa akasurrender, wewe na hospitali yako huko Tandahimba utathubutu kukataa, hata kama unaumizwa?

Na hawataishia kuzitisha tu, wataenda mbali zaidi kufanya surbotage. Utaanza kusikia hospitali zinafanyiwa ukaguzi, mara zimekwepa kodi, mara zimeajiri watu bila mikataba, mara zimejenga majengo mapya bila kibali. Yani ili mradi kuzifrustrute ili tu zikubaliane na vifurushi vipya. Hii ndio mbinu pekee iliyobaki na inatumiwa sana na serikali za kiimla, zilizoshindwa kutatua changamoto kwa kutumia akili.

ATHARI ZAKE NI ZIPI?
1. Kwanza kuna watu watapoteza maisha kwa sababu ya huu mvutano wa NHIF na vituo binafsi vya kutolea huduma. Mtu amekosa huduma Peramiho, mpaka aende Songea mjini kama ni dharura anaweza kupoteza maisha.

2. Mgogoro huu utasababisha usumbufu usio wa lazima kwa wagonjwa. Umetoka huko Mpiji Magohe, unaenda Kairuki unaambiwa hamna huduma, unalazimika kukanyaga hadi Mwananyamala. Ukifika unakuta muda wa huduma umeisha, hadi kesho tena.

3. Vituo vya umma vitaelemewa sana na kushindwa kutoa huduma. Takwimu zinaonesha kuwa hapa Dar peke yake vituo binafsi ni 79% na vya serikali ni 21%. Na kwa nchi nzima vituo binafsi ni 42% na vya umma ni 58%. Hivi unawezaje kuhudumia watu wote kwenye vituo vya umma kama si kujimwambafai kwa ujinga?

4. Maelfu ya watu watapoteza ajira. Ili vituo viweze kujiendesha kwa hizi bei mpya, itabidi vipunguze idadi ya wafanyakazi na matikeo yake wengi watapoteza ajira. Serikali itakosa kodi (PAYE) na mzigo wa watu tegemezi utaongezeka.

5. Huduma nyingi zitatolewa chini ya kiwango ili kupunguza gharama za uendeshaji.

6. Vituo vingi vya kutolea huduma vitafungwa. Wamiliki wataona bora wabadilishe biashara ili kuepusha mgogoro na serikali. Matokeo yake wananchi maskini watalazimika kufuata huduma vituo vya mbali na hivyo kuongeza gharama zaidi.

NINI KIFANYIKE?
1. Jambo la kwanza kabisa, Serikali isitishe vifurushi vipya, na badala yake vile vya zamani viendelee kwanza wakati suluhu ikitafutwa.

2. Kamati ya kureview bei mpya ya vifurushi ihusishe wadau wote kwa usawa. Wawepo watu wa wizara, NHIF, hospitali za umma, hospitali binafsi (APHTA, CSSC, BAKWATA) na wananchi ambao ndio beneficieries.

3. Bunge liharakishe mapitio upya ya sheria iliyoanzisha NHIF ili hospitali binafsi na vituo binafsi vya kutolea huduma viweze kutambulika kisheria kama wadau wa NHIF.

4. Serikali ihakikishe fedha zote zilizokopwa NHIF zinarudishwa kama ilivyoelezwa kwenye ripoti ya CAG. Haiwezekani watu wajikopeshe hela kwenda kununua magari, viwanja, nyumba halafu usumbufu waje kupata wagonjwa. Hatukatwi mishahara yetu ili watu wakanunue magari, tunakatwa ili tutibiwe.

5. Serikali ihakikishe inalipa madeni yote yaliyotokana na huduma bure kwa wazee. Na uwekwe utaratibu rasmi wa kuendelea kulipia wazee matibabu yao badala ya kuacha mzigo huo kwa NHIF pekee.

6. Baadhi ya taasisi za umma ziruhusiwe kutumia bima za makampuni binafsi ili kupunguza mzigo kwa NHIF. Taasisi kama BOT, TRA, TANAPA, TPA, TANESCO etc zinaweza kabisa kulipia watumishi wake bima kwenye makampuni binafsi na kupunguza mzigo NHIF.

7. Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya NHIF ifumuliwe na kusukwa upya.!

Malisa GJ
 
NHIF needs to be re engineered. Management imeshindwa kazi. They don't pay for services rendered to their clients. Hata hospital za serikali given the choice, they would not give service to NHIF card holders.
Tanzania kuendesha matibabu kwa bima ni jambo gumu sana sana. Tatizo ni kuwa tumeshajijengea utamaduni wa kutokuwa waaminifu jambo ambalo kwenye tiba ya matibabu, ni sumu mbaya sana.
 
Back
Top Bottom