Ni aibu Diamond kukosa Milioni tano ya Matunzo ya Mtoto. Aache kuzaa tu

Ni aibu Diamond kukosa Milioni tano ya Matunzo ya Mtoto. Aache kuzaa tu

Mabeto ameona huo ni mtaji...
Even hata ingekuwa mimi na ikawa uwezo wa kutoa mil10 ninao, ni kuwa sitoweza kuzitoa !
Hapo sasa akitoa ajue atategeshewa mimba nyingine na hata watu wengine then wakimbilie mahakamani wakijua wakidai matunzo ya mamilion watapata!
Hizo mil5 kwa mwezi ni nyingi, ni matunzo ya aina gani hayo?!?..
 
Msanii Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz, amedai mahakamani kuwa hana uwezo wa kumlipa Mwanamitindo Hamisa Mobeto, Sh milioni tano kama gharama za matunzo ya mtoto kwa mwezi.

Diamond amewasilisha majibu hayo katika Mahakama ya Watoto Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka baada ya Mobeto kumfungulia kesi ya madai katika Mahakama hiyo ya watoto akidai mambo mbalimbali ikiwamo matunzo ya mtoto.

Katika majibu yake Diamond amedai fedha hizo anazodai Hamisa kulipwa kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

Mobeto katika maombi yake kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck wa Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys, anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, mtoto huyo wa kiume aliyezaa na msanii huyo na kumuomba msamaha kwa umma kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Baada ya kupokea majibu hayo mahakama iliahirisha kesi hiyo ya madai hadi Novemba 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Mobeto kupitia wakili wake walimpa notisi Diamond ya kutaka amwombe radhi na kupeleka matunzo ya mtoto ndani ya siku saba lakini notisi hiyo haikutekelezeka hivyo aliamua kulifikisha suala hilo mahakamani.
Unasema ni aibu ww unaweza kumpa mwanamke uliezaa nae mil.5 per month?
 
mimi nitampa,potelea pote.
Mabeto mabeto njoo nikutunzie mtoto wa CHIBU.
 
Iwe isiwe ila milioni 5 Kwa mwezi.hizo ni hela nyingi.unafanya mtoto kama mtaji wako. Kulipa anatakiwa diamond alipe ila sio Kwa milioni 5.hamissa inabidi na yeye ajitume.
Ni kweli au chachandu...
 
Hamissa mjanja sana anajua mond hawezi kukubali kulipa hiyo hela hata mahakama haiwezi kukubali ilo ila itashushwa na ikishushwa haiwezi kua chini ya milioni 1 kwa mwezi, hata mahakama wanaangalia kipato cha baba...huwezi kuwa kwa mwezi baba unapata milion 10 au 20 halafu mtoto umpe laki 2 kwa mwezi hiyo ilikua zamani.
 
Back
Top Bottom