Ni aibu Diamond kukosa Milioni tano ya Matunzo ya Mtoto. Aache kuzaa tu

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Msanii Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz, amedai mahakamani kuwa hana uwezo wa kumlipa Mwanamitindo Hamisa Mobeto, Sh milioni tano kama gharama za matunzo ya mtoto kwa mwezi.

Diamond amewasilisha majibu hayo katika Mahakama ya Watoto Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka baada ya Mobeto kumfungulia kesi ya madai katika Mahakama hiyo ya watoto akidai mambo mbalimbali ikiwamo matunzo ya mtoto.

Katika majibu yake Diamond amedai fedha hizo anazodai Hamisa kulipwa kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

Mobeto katika maombi yake kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck wa Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys, anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, mtoto huyo wa kiume aliyezaa na msanii huyo na kumuomba msamaha kwa umma kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Baada ya kupokea majibu hayo mahakama iliahirisha kesi hiyo ya madai hadi Novemba 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Mobeto kupitia wakili wake walimpa notisi Diamond ya kutaka amwombe radhi na kupeleka matunzo ya mtoto ndani ya siku saba lakini notisi hiyo haikutekelezeka hivyo aliamua kulifikisha suala hilo mahakamani.

Eti Msanii mwenye hela nyingi mara ajiite Dangote, kumbe ni mbwembwe tu hana kitu.
 
5 mil. per month is unreasonably much! hata bakhressa hawezi amriwa alipe hiyo hela!

I think the court will order maintenance accordingly...! but walichofanya mawakili wa mobeto ni prayer tactics...hapo wanategemea hata mahakama ikishusha na ukizingatia ubora wa maisha ya diamond,basi hawamkosi hata 1 mil. per month...lengo linakuwa limetimia...kuliko wangeanza na mil 1,wangeshushwa hadi laki 2.
 
Milioni 5??? Huyu dada anafanya mtaji sasa mana anataka kuwazid hadi waliosoma mpk masters mshahara wao kwa mwez haufiki 5 milion...hyo sasa ni kukomoana shida zote anataka azimalizie kwa mtt wa mwanamke mwenzake anasahau kaz ya usanii ni yakupanda na kushuka badala aombe hata ajengewe nyumba ya kukaa na mwanae ili hata siku diamond akishuka kimuzid asipate shida na mtt nyumba za kupanga yy anataka pesa za show off zakufurahisha mashost kwa party maskin ya mungu hajui hata kumtengenezea mwanae future yake
 
Msanii Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz, amedai mahakamani kuwa hana uwezo wa kumlipa Mwanamitindo Hamisa Mobeto, Sh milioni tano kama gharama za matunzo ya mtoto kwa mwezi.

Diamond amewasilisha majibu hayo katika Mahakama ya Watoto Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka baada ya Mobeto kumfungulia kesi ya madai katika Mahakama hiyo ya watoto akidai mambo mbalimbali ikiwamo matunzo ya mtoto.

Katika majibu yake Diamond amedai fedha hizo anazodai Hamisa kulipwa kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

Mobeto katika maombi yake kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck wa Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys, anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, mtoto huyo wa kiume aliyezaa na msanii huyo na kumuomba msamaha kwa umma kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Baada ya kupokea majibu hayo mahakama iliahirisha kesi hiyo ya madai hadi Novemba 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Mobeto kupitia wakili wake walimpa notisi Diamond ya kutaka amwombe radhi na kupeleka matunzo ya mtoto ndani ya siku saba lakini notisi hiyo haikutekelezeka hivyo aliamua kulifikisha suala hilo mahakamani.
Kwamfano mkuu wewe unaweza kumpa mzaz mwenzako hyo 5 milioni ?? Mpk useme ni aibu
 
Back
Top Bottom