Ni aibu Graduate wengi kumaliza chuo hawezi kujitegemea. Nashauri wasipewe vyeti hadi kuwe na ushahidi wa kujitegemea

Ni aibu Graduate wengi kumaliza chuo hawezi kujitegemea. Nashauri wasipewe vyeti hadi kuwe na ushahidi wa kujitegemea

Aibu kubwa ni mtu kupewa mafao af anagombea Tena kisha mafao Tena kisha anagombea afu anasema vijana wajiajiri
 
tukishatuma maombi tunasubiri interview,hatufanyi kazi na hatuhami kwa wazazi mkitaka mtuue
 
Mkuu acha kurahisisha mambo kuna kitu kinaitwa Skills..., hilo lazima ujue kabla ya yote na sio jambo rahisi na linaongezeka kutokana na experience...

Mbili swali la kujiuliza zaidi hao wachoma mahindi, wanyoa nywele na seremala ni wangapi wana income ya kujitosheleza basic needs zao za kila siku ?

Kazi za kunyoa, food and hospitality unadharau ila hizo ni kazi ambazo zina skills ambazo hazijalishi usomi wako bali experience katika field.., LAKINI kwa mtu mwenye upeo mrefu ni tunataka kujenga nchi ya baba / mama ntilie, maseremala wa kubangaiza na street hawkers au nchi yenye mpangilio ambayo watu wanaweza kujishikiza kutokana na experience yao na ujuzi wao kupata basic needs ?

Kwa mtaji huu wa kutokuwabana watunga sera wananchi wataendelea kubangaiza till Kingdom Come..., na walamba asali wataendelea kuwalisha matango pori kwamba shida zao hao wanaokosa ujira wa kutosha ni wao wenyewe kutokujiongeza.... (No wonder Bongo kuna utitiri wa watoa huduma walewale kila kona wengine kuzidi hata wahitaji)
Ngumbaru wana akili za kinyesi , logic hii huyu mpumbavu aliyeandika hii mada ya kipuuzi hawezi elewa .


Sent from my Nokia 6.2 using JamiiForums mobile app
 
Unaangalia suala kwa individuals mimi naangalia suala kama complete set yaani nguvu kazi kwa ujumla....; Tunatumia Kodi zetu na muda wa kuwaongezea watu upembuzi wa kuweza kupambana na mazingira yao alafu wakija hakuna infrastructure ya kuweza kutumia kile tulichowafundisha hio ina maana gani ?

Badala ya kuwa na mama ntilie wanaouza chakula bukubuku na kujinyima na siku wakiugua wanakula mtaji wao wote kwanini tusiwe na formal restaurants / quality places ambapo mtu anatoa pesa ya kumnufaisha huyu mama anayeshinda kwenye moto siku nzima na kuajiri wadogo zake anaowalipa buku mbili kwa siku (hapo na nauli ya kuja na kuondoka) - Utaona kwamba hilo haliwezekani sababu watu hawana buying power wanakwenda kwenye cheap prices na hao wanaowapa huduma hawana option bali kufanya wanachofanya mkono uende kinywani...

Kwahio narudia tena wewe unaangalia symptons mimi naangalia root causes..., by the way na hao graduates wote wakichoma mahindi, mama ntilie na seremala itafika wakati kila mtu anajipikia chakula na kujiuzia na kujilisha - No Buying Power....
Umemaliza kabisa

Sent from my Nokia 6.2 using JamiiForums mobile app
 
Kuchoma mahindi, kupika wali na maharage, kunyoa nywele kawaida ni skills ambazo mtu anaweza kujifunza hata kwa mwezi pekee, labda kama ni mambo advanced sana mfano kwenye kunyoa kuna wle wanaochora kwa kunyoa
kwahiyo wewe uko tayari umsomeshe mwanao afu aje achome mahindi konyo wewe nyau mmoja
 
Kwani kufuga lazima uwepo mwenyewe? kwa bahati mbaya hadi sasa yupo kitaa tu ramani hazijasoma bado mwaka3 huu. anaishi kwa beti ndo inamfanya a survive. siwezi mpangia nilikuwa naitaji kwa nilicho nacho mimi. bali alionyesha kuzarau kulingana na elimu yake aliyonayo hawezi lisha kuku!
Ok sijui circumstance zake aliyopo huyo jamaa ....tuishie hapa

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
kwahiyo wewe uko tayari umsomeshe mwanao afu aje achome mahindi konyo wewe nyau mmoja
Ni heri mtoto awe anaweza kumudu hata elf 5 kila siku kwa kuchoma mahindi kuliko kuwa na degree hana hata jero ya vocha ya ku apply ajira
 
Tatizo ni kwamba vijana wanajitenva hawataki kuchangamana na watu bila kujari elimu zao kutwa kulala tu, mm ni mhitimu na sijaajiliwa nimejiajiri kufundishia tuition kuhusu elf 30 mfukoni sikosi kbs
 
s
Ni heri mtoto awe anaweza kumudu hata elf 5 kila siku kwa kuchoma mahindi kuliko kuwa na degree hana hata jero ya vocha ya ku apply ajira
sasa si ungemkabidhi shamba tu asiende shule awe mlima mahindi na mchoma mahindi
 
kubwabwaja ukiwa sebulen kwa shemej yako daslam au umejipata ni rahis mno!ukwel ni kwamba ni binadamu wachache wanaeza ku~switch kutoka katka kitu alichobobea na kuanza kitu kipya katka umri mkubwa kwan akili na mwili hukataa kukata kona na kuanza upya....mada yako ni too general na umejikita kulaumu pasi na kuonyesha huyo std7 mchoma mahind nae ali~hustle kias gan had kusimama!
 
Kumekuwa na tabia iliyojizolea umaarufu kwa wahitimu wakimaliza vyuo wanarudi nyumbani na kushinda mitaani / mitandaoni bila shughuli maalum ya kuwafanya wajitegemee, muda huwa hausimami miaka inaenda unakuta mhitimu anagonga 28+ bado yupo kwao

Wengi huwa wanaona njia pekee ya kujitegemea ni kuajiriwa, hawapo tayari kufanya shughuli zingine utawasikia "nimeshatuma maombi ya kazi flani nasubiria interview", matokeo yake miaka inaenda mtu yupo kwao.

Shughuli nyingi wanazofanya Darasa la 7 / Form 4 hata wahitimu wanaziweza, ingekuwa vyema wahitimu waanze kujitafuta huku mapema,

Darasa la 7 / Form 4 anajitegemea kwa kuchoma mahindi , inakuwaje muhitimu anabaki kwao wakati nae anaweza ?

Darasa la 7 / Form 4 anajitegemea kwa kunyoa , inakuwaje muhitimu anabaki kwao wakati nae anaweza ?

Darasa la 7 / Form 4 anajitegemea kwa umama / ubaba ntilie , inakuwaje muhitimu anabaki kwao wakati nae anaweza ?

Darasa la 7 / Form 4 anajitegemea kwa useremala , inakuwaje muhitimu anabaki kwao wakati nae anaweza ?
Kujitegemea ni kufanyaje?
 
Back
Top Bottom