Ni aibu kiasi gani utaipata endapo mtu akishika simu yako ghafla na akaanza kuikagua?

Ni aibu kiasi gani utaipata endapo mtu akishika simu yako ghafla na akaanza kuikagua?

Uhalisia wa mtu upo kwenye simu yake hasahasa search history zake kwenye mitandao mbalimbali.

Kuna watu wengine tena wa maana kabisa na wengine ni viongozi wa dini, search history zao za Telegram ni Utamu motomoto.

Simu huficha mengi sana.

Kuna huyo mmoja anajiita mchungaji of course hata watu wanamwiita mchungaji anachapa sana injili watu wanaokoka sana alooo hata wewe ukimuona utamuamini 100%

Kwenye simu yake kuna Jehanam ana groups zote za connection ana mapicha ya hovyo yaani kiufupi moto wake utakuwa wa gesi Kama atakufa na zile dhambi

Simu hizi zitawapeleka wengi Jehanam
 
๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Me naogopa akijua ni member wa Jf, na wakati alishaniuliza unaijua JF,
Nikajibu siijui ndy kitu gani hichoooo???
Akajibu nanukuu " Yan JF ni platform ambayo wadada wanajiuza huko, kuna kitu kinaitwa PM"
Miye nikajibu sawaaaaaaa
 
Binafsi simu yangu kwa % kubwa utakuta Dj mix's za kutosha, screenshots za comments za kujenga na video clips za mpira wa miguu. Baaasi.

Juzi kuna dada alikuwa ananionesha video fulani ilivyoisha ikaenda next ni video za utupu akaishia kuona aibu nikajifanya kama sijaona.

Kingine cha muhimu mtu akikupa simu yake fanya ulichopaswa kufanya na sio kuipekuwa hata kama hayupo hapo. Binadamu tuna mengi sana tena ya ajabu na aibu.
 
Back
Top Bottom