Ni aibu kwa Media, Waziri na Wachambuzi wa Michezo kutoa maamuzi Goli la Yanga bila kujiridhisha


Jitahidi watu wasijue kama huna akili
 
Walimu wote wa Mathee mtusamehe bado kwenye mathee hatujafika popote...! Si mnaona jinsi tunavyojadiliana? Tupo kama mazuzu.!

Smartphone ipi...kishikwambi au ?
chukua hiyo hiyo unayotumia ipime upana kisha rejea video angalia distance kwa kutumia simu yako uliingia kwa milimetre ngapi kisha piga hesabu
 
Yule Naibu Wazir naye kiaziiii hajui hata Diplomacy anaropoka kama anaimba taarabu tuu. Kuna namna ya kuongea kama Kiongozi siyo anatanguliza mihemko na ushabiki mwishowe wanaharibu.
Yaani huyu, hata Ubunge hakustahili. Ni mambo ya JPM, kutaka ku 'balansi' ,eti, kule kuna SUGU, nasi tuna Mwana………..!
 
Umalaya si kujiuza tu kama hivi ufanyavyo hapa!
 
ALIYEKATAA BAO LA YANGA AITWA FIFA.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limemteua refa Beida Dahane aliyechezesha mechi ya Mamelodi na Yanga, Ijumaa iliyopita kuchezesha mechi za soka za mashindano ya Olimpiki itakayofanyika Ufaransa kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu.

Dahane (32) ni miongoni mwa marefa 12 kutoka Afrika ambao wamepata fursa hiyo huku kiujumla wakiteuliwa marefa 89 kutoka nchi tofauti duniani.

Marefa kutoka Afrika walioteuliwa kuchezesha Olimpiki mwaka huu ni walioteuliwa kuchezesha michezo ya Olimpiki mwaka huu ni Karboubi Bouchraw wa Morocco, Mahmood Ismail(Sudan), Diana Chkotesha(Zambia), Fatiha Jermoumi(Morocco), Elvis Noupue (Cameroon), Stephen Yiembe.(Kenya), Mahmoud Ashour (Misri), Lahlou Benbraham (Algeria), Ahmed Abdoulrazack (Djibouti), Emiliano Dos Santos (Angola) na Shamirah Nabadda Uganda).

Ijumaa iliyopita Dahane alizua mjadala baada ya kukataa bao la kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki ambalo kwa mujibu wa baadhi ya picha za video na za mnato, mpira ulivuka wote mstari wa goli ingawa kwa uamuzi wa refa, haukuvuka wote.

Katika mchezo huo Yanga iliondolewa kwenye hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa penalti 3-2.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…