Wanaume wa Dsm sasa mmezidi. Inakuwaje mwanaume mzima na midevu yako unatumia neno 'mwaya'?
Utasikia..
Haya mwaya!
Ndiyo mwaya!
Twende mwaya!
Niambie mwaya!
Nini maana ya neno mwaya?
Wanaume wa Daslam badilikeni aisee..
Kwa watu wa Tanga (Wabondei au Wasambaa, sina uhakika na Wadigo, Wazigua au Wasegeju) hili neno ni gender-neutral. Wanawake kwa wanaume, watoto na wazee hulitumia.
Neno hilo linalotumika badala ya:
[emoji830]Mwenzangu
[emoji830]Aisee
[emoji830]Ndugu
[emoji830]nk.
Kiswahili kimejaa maneno kibao ya makabila ya Tanga. Msianze kuwachagulia wanaume watumie neno gani la Kiswahili litokanalo na Kitanga.
Maneno kama:
[emoji830]SONI (aibu au haya)
[emoji830]MBWAI (ni nini)
[emoji830]CHEREKO (kufurahia)
[emoji830]CHAMBILECHO... (kama alivyosema...)
[emoji830]SOGA au SHOGA (rafiki)
[emoji830]TAMBA (kujisifu, pia kusafiri)
[emoji830]WAMBA au WAMBE (sema au eleza)
[emoji830]nk.
Mbona Watanga hawachukii wakisikia Kiswahili kinapotoshwa na watu wa DSM na wa bara wanapoweka neno GA au PO katika kilakitu:
[emoji830]NinakupendaGA
[emoji830]NilikuwePO
[emoji830]ChangamkiaGA fursa
[emoji830]nk.
Neno MWAYA ni neno clean kabisa na halina uhusiano na homosexuality kabisa kwa wanaume. Muulize mtu yoyote yule wa TANGA.
Habari ndio hiyo. Sasa kama MBWAI, MBWAI bwana.[emoji16][emoji16][emoji23]