Ni aibu kwa vyuo vikuu hapa nchini kushindwa kugundua chanjo ya Corona na sasa vinashindana kutoa tahadhari

Ni aibu kwa vyuo vikuu hapa nchini kushindwa kugundua chanjo ya Corona na sasa vinashindana kutoa tahadhari

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Kazi kubwa za vyuo vikuu ni tatu:
  • Kuelimisha/kifundisha (teaching)
  • Kuandika vitabu (publication)
  • Kufanya tafiti (Research).
Kati ya kazi hizo tatu research ndiyo huleta maana kubwa sana kwa uwepo wa chuo kikuu chochote mahala popote. Ni sawa na benki, kwa mfano, ina kazi nyingi sana lkn utoaji wa mikopo ndiyo huleta tija na faida zaidi kwa jamii na benki yenyewe..

Nimestushwa na mfululizo wa matamko ya tahadhari dhidi ya korona yanayotolewa na vyuo vikuu hapa nchini kwa jumuiya zao.

Nilitegemea vyuo vikuu hivi viwe vimeshafanya tafiti na kuja na chanjo ya korona badala ya kutupigia kelele bila suluhisho.

Najiuliza maswali mengi kuhusu hivi vuuo vikuu. Hivi kuna wasomi kweli? Ama kuna mkusanyiko wa wahuni wenye vyeti tu? Tija yao nn kwa taifa? Vyuo viku hivi vimeshindwa kushirikiana vikatuletea hata dawa za kufubaza virusi hivi?

Malaria, ukimwi, athma, mafua ni magonjwa ambayo yapo kwa miaka lukuki lkn hivi vuuo vikuu havijagundua hata kidonge!

Sasa navitaka vyuo vikuu hivi kukaa kimya, endeleeni kunywa pombe, kufanya ngono, na kurushiana video za umbea. Mqmbo ya corona waachieni Oxford, Harvard na Berlin universities waizungumzie.

Rubbish!!!
 
We unataka kusema tuna wasomi wa vyeti na mizigo.

Wakimaliza chuo miaka 3 anakuja mtaani kuwa bodaboda
 
Aisee umewapa kazi kubwa sana hivi vyuo maana vyuo vikuu vya hapa nchini ni sawa na wacheza pool table na wazee wa kubet.

Yani kama maji ya chumvi wameshindwa kubadilisha na kuwa maji yasio na chumvi unadhani hapa nchini kuwa vyuo?

Uwezi kutengemea impact ya elimu kama utafanya elimu ya nchini ni siasa, vyuo vya hapa nchini ni utopolo tu.

Tunasema Elimu na Shule ni vitu vinayotakiwa kuendana lakini sio lazima.

Matukio ya kuprove wrong katika elimu yetu ni mengi!!!

Ndio maana kutoboa katika nchi yetu nasemaga ni pangumu kwa sababu tumeamua kuwa upande wa siasa kwa kila kitu, ni ujinga ambao wananchi bado hawajajua ndio maana tunadhani Magufuli ni bora kuliko wote kisa kawawekea elimu bure ambayo impact yao ni kupiga kura katika uchaguzi.
 
Kabisa mkuu. Profesa wa physics (umeme) anaita kishoka wa mtaani kurekebisha bulb ya umeme nyumbqni kwake
Physics na umeme ni mambo tofauti.

How ever umeme umetokea kwenye physics.

Kwa ninavyojua hakuna profesa anapiga kishoka.

Ukishafika hizo level labda uweuke mwenyewe. lakin sio kupiga kishoka. degree labda.. masters labda.. sio prof ni kitu kingine
 
Ifike mahali wewe ndio uone aibu vitu vidogo hata visivyohitaji publication mfano issue ya Doc Faustine kumkosoa Kaisari kuhusu kujipiga mvuke nini kilitokea !

Leo hii MD mzima mwenye dhamana badala ya kufanya practical approach ya alichosomea badala yake wanaweka meza kufundishana kumenya na kula matunda !

Unahitaji akili kiasi gani kutowahurumia wasomi kwa awamu hii ambapo mawazo yao yanazimwa kisiasa?
 
Nitajie vyuo vikuu viwili tu unavyovilenga katika bandiko lako...halafu nitakupa sababu za kwa nn haya uliyoyaandika hayafanyiwi kazi..
Vyuo vikuu vyote vikongwe hapa nchini
 
Chanjo ya corona inatengenezwa na egg white, umeshaona hayo ma tray ya mayai kwa siku yanayochezewa kwenye research.

Tray ya mayai bongo bei yake ni sh elfu 6-7 kwa siku watu wanaweza chezea tray 2000 kama million 14 za kitanzania now imagine research labda inachukua miezi sita.

Piga hesabu ya cost 14 m x 180 days.
Yupo huyo supplier reliable wa mayai.
Hathari zake kwa soko la mayai maana Tanzania adverse kidogo tu sokoni ya supply and demand bei hizo zinapaa.
Bado wale ambao wakijua egg york unatupa utumii kwenye research na njaa zao, waanze kulia lia mnachezea chakula.

Tujikite kukuza uchumi kwanza sio kuwaza mambo ambayo mazingira yetu hayapo tayari ku-support ata kama hao scientists tunao.
 
Chanjo ya corona inatengenezwa na egg white, umeshaona hayo ma tray ya mayai kwa siku yanayochezewa kwenye research.

Tray ya mayai bongo bei yake ni sh elfu 6-7 kwa siku watu wanaweza chezea tray 2000 kama million 140 za kitanzania now imagine research labda inachukua miezi sita.

Piga hesabu ya cost 140m x 180 days.
Yupo huyo supplier reliable wa mayai.
Hathari zake kwa soko la mayai maana Tanzania adverse kidogo tu sokoni ya supply and demand bei hizo zinapaa.
Bado wale ambao wakijua egg york unatupa utumii kwenye research na njaa zao, waanze kulia lia mnachezea chakula.

Tujikite kukuza uchumi kwanza sio kuwaza mambo ambayo mazingira yetu hayapo tayari ku-support ata kama hao scientists tunao.
Unamaanisha serikali haiwezi kughalamia mchakato huu kwasababu haina fedha?
 
Ni kiasi gani serikali inatenga bajeti kwa ajili ya tafiti? Ukiona tume ya uchaguzi ina bajeti kubwa kuliko research usilie kumlaumu prof. Wa chuo laumu hao std seven wanao pitisha bajeti bila kujali kesho ya taifa.

Nikupe mifano kadhaa:
Pale SUA wanatengeneza vaccine za wanyama unataarifa?

Unadhani uwepo wa maprof kama Issa Shivji na manguli wengine wa sheria ni kwa bahati mbaya? Mbona tuna mikataba ya kipumbavu sana, kwa nini hawakuwepo Kwenye negotiation panel?
 
Back
Top Bottom