Ni aibu msomi kufanya biashara ambayo hata asiyesoma anaweza kufanya

Msomi unayemsemea wewe akimbinu mbuni yake nzuri mtaji utampa wewe mkuu?
akimbinu mbunu,amembunu bunu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ unenifanya nicheke mkuu kula replyπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Unafanya biashara gani mkuu!
 
Embu tuacheni Idea za Ajabu, sijui kulima tikiti, sijui juisi ya Muwa, tuje na Idea solid ambayo asilimia kubwa inakuwa ni service business na sio manufacturing ambazo asilimia kubwa ni hasara tu.
Orodhesha idea zako tano, 'solid', unazofikiria kuzianzisha ili kuhamasisha wahusika. Au wewe siyo 'mwenye digrii'?
 
Kwani msomi akilima tikiti na akatengeneza faida tatizo liko wapi? Labda una hoja ila sijakuelewa, hebu fafanua kidogo Mangi wa duka la nguo ambae hajasoma anafanyaje na huyo aliyesoma akiuza nguo afanyaje ili kujipambanua kwamba yeye ni msomi..

Na labda cha kuongezea, Ukisoma unasomea profesheni, hakuna uhusiano na kufanya biashara, huyo jamaa wa Masters , hiyo masters itakuwa na mchango mdogo sana kwa hicho alichofanya, kama ina mchango at all!
 
Umetoa changamoto nzuri lakini ya kukandia wajasiriamali wadogo. Mtu anaweza kuwekeza kwenye hivyo vitu unavyoviona wewe vya ovyo na akatoka sana kimaisha kushinda wewe na elimu yako na mawazo makubwa makubwa! Kazi ya elimu ni pamoja na kukuwezesha kuboresha hali ya chini ya maisha/utendaji kuwa wa hali bora zaidi. Hivyo mkulima wa matikiti akiwekeza na kulima kitaalam anaweza kufika mbali sana kiuchumi na anaweza hata kulenga masoko ya nje ya nchi kwa vile atakuwa na elimu na ufahamu mpana zaidi wa kidunia.
 
ela ndio nini?
 
Cha muhimu ni kujua dhima ya biashara ni nini!
Kila anatarajia ama anayefanya biashara lengo aje kupata faida .
Na faida hutofautiana kulingana na ukubwa na thamani ya kile unachokiwekeza. Ukiwekeza kikubwa kunauwezekano mkubwa pia kupata faida kubwa mbeleni.
Na kumbuka uwekezaji wenye faida kubwa mara nyingi hukugharimu mtaji mkubwa na hata faida yake huchukua muda mrefu zaidi kujakupata faida pengine inaweza kuchukua hata miaka mitatu hata mitano kujakupata faida yako.
Kumbuka Watanzania wengi wa idea nzuri za kibiashara lakini wanakosa kianzio cha kufanya biashara yenye uwezekano wa kupata faida zaidi mwisho wa siku unajukuta unawazakufanya biashara kutokana na uwezo wako wa kupata mtaji.
Mwisho mleta mada unaonekana kutoka familia inayojiweza kifedha hivo usidharau mawazo ya wenzio hasa wale waliotoka kwenye familia duni .
 
Ila uyu jamaa benjamin nilikuwa simfuatilii, nimemperuzi peruzi huko IG jamaa sio wakawaida kimsingi ana network kubwa tena ya watu heavy wenye mawazo, amepita sehemu nyungi kakutana na wengi ana haki ya kukataa ule mshahara mkubwa kwa Bill na kujenga imaya yake anaweza kuwa tajiri namba moja TZ na level za kiafrika miaka ijayo.


Kitu pekee nilichokuwa nakiwaza sana na mtoa mada umekikazia ni kuhusu Biashara ya kutoa huduma na sio kuzalisha bidhaa kwasasa hii matajiri wengi wanatoka humo.
 
.....Hizi tuhuma za wasomi wetu na kufanya mambo ya kawaida ungeanzia, kwanza kwa walimu wao maprofesa na madakta, wanaochukulia siasa kama sehemu ya kutokea. Hawa nao wamekosa creativity!.....kuhusu vijana kuja mezani na idea zilezile inategemea na exposure na kijana husika. Chukulia mathalani kijana familia bora 'kabukua' huko stanford, tayari anakuwa mawazo ya juu zaidi. Huyu hata wazazi wake wanaweza kumsapoti kifedha, ingawa yeye ana idea. Sasa mwenzangu namie kasoma huku hela, ya mkopo anawaza kuwasaidia wazazi, ataweza kuwaza zaidi yamradi wa kufuga kuku...?
 
Kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…