Ni aibu sana kijana wa kiume kujisifia kuwa unatongozana na mke wa mtu. Hizi tabia mlijifunzia wapi?

Ni aibu sana kijana wa kiume kujisifia kuwa unatongozana na mke wa mtu. Hizi tabia mlijifunzia wapi?

Malezi malezi malezi, tuwajibike kwa nafasi zetu kuepuke kizazi cha hivi....pengine wazazi / walezi waliteleza ila tuna nafasi ya kutengeneza kwenye kizazi gen Alpha
 
"Nyakati ngumu huunda wanaume wenye nguvu, wanaume wenye nguvu huunda nyakati nzuri, nyakati nzuri huunda wanaume dhaifu, na wanaume dhaifu huunda nyakati ngumu."

Kipindi unakuwa uliwahi kusikia wakubwa zako wanashare stories za kula na kutongoza wake za watu?

Mke wa mtu ni uchungu uliojificha katika kona ya mbali katika moyo wa mwanaume yoyote.

Ni uchungu ambao hauwezi kuu ona katika nyuso yake ila ni uchungu ambao hata ukimwimbia milioni 10 atakupa nafasi ya kumrudishia taratibu ila ukimla mke wake nae anakufanya mke wake au kukutupa ruvu.

Vijana wamekuwa wadhaifu sana, mtu kabisa anashare chats za kutongozana na mke wa mtu na watu wanamsifia kweli eti "kula huyoo, kula huyoo"
Kumbe na wewe umeliona lile dogo upinde na sikumuacha hivi hivu nilimpa maneno makali sana na kufru , wanaume sijui tumekuwaje ni bonge moja la ulimbukeni ,

Tena ulivyoandika huu uzi hasira zimenipanda sana narudi kwenye uzi wake nikamshushie mitusi mpaka nipigwe BAN, Na nyie Mods upuuzi gani ule mnaruhusu?
 
Yani ni upuuuzi wa kwnda shule mkuu.

Vijana wamekuwa taka taka sana, uhuni umeingia hadi katika maisha ya kawaida sana. Zamani uhuni ulikuwa vijiweni. Tulitegemea vijana waliokuwa na exposure waweze kuwa na staha ila wametumia nafasi hii kuonesha upande wa uhuni wao.

Mtu kabisa anapata ujasiri na faraja ya kujisifia kufanya mapenzi na mke wa mtu.
Alafu unaweza kuta wanaomshabikia humu mmoja wao ndio mke wake 😂😂.
 
Back
Top Bottom