Ni aibu sana kijana wa kiume kujisifia kuwa unatongozana na mke wa mtu. Hizi tabia mlijifunzia wapi?

Malezi malezi malezi, tuwajibike kwa nafasi zetu kuepuke kizazi cha hivi....pengine wazazi / walezi waliteleza ila tuna nafasi ya kutengeneza kwenye kizazi gen Alpha
 
Kumbe na wewe umeliona lile dogo upinde na sikumuacha hivi hivu nilimpa maneno makali sana na kufru , wanaume sijui tumekuwaje ni bonge moja la ulimbukeni ,

Tena ulivyoandika huu uzi hasira zimenipanda sana narudi kwenye uzi wake nikamshushie mitusi mpaka nipigwe BAN, Na nyie Mods upuuzi gani ule mnaruhusu?
 
Yani ni upuuuzi wa kwnda shule mkuu.

Vijana wamekuwa taka taka sana, uhuni umeingia hadi katika maisha ya kawaida sana. Zamani uhuni ulikuwa vijiweni. Tulitegemea vijana waliokuwa na exposure waweze kuwa na staha ila wametumia nafasi hii kuonesha upande wa uhuni wao.

Mtu kabisa anapata ujasiri na faraja ya kujisifia kufanya mapenzi na mke wa mtu.
Alafu unaweza kuta wanaomshabikia humu mmoja wao ndio mke wake 😂😂.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…