Moja kwa moja nijikite kwenye mada:
Sarakasi ya kumpata mgombea wa CCM ilikuwa ni muendelezo wa yale wanayoyafanya kumpata rais wa nchi.
Kwa kuwa Mungu wa mbinguni atoaye mamlaka kwa mtu anayemchagua ameamua kuwavua nguo wote waliozoea kuvunja sheria, katiba, kanuni, miongozo na desturi kwa maslahi yao; ameingiza sintofahamu kwa kuwapa ujasiri baadhi ya watu ndani ya chama kukemea ukiukwaji wa sheria na katiba.
Nina matuamaini kuwa mtifuano huu utaleta heshima kwa wananchi.
Kuna team hapa itapoteza sana na uenda wakaishi uamishoni maisha yao yote yaliyobaki hapa duniani.
Nasikia kuna tangazo huko la kuanza mchakato upya.