@PascalMayalla!
Ujuwe wewe humu unaheshimika sana kama senior member [emoji120]
Lakini usije ukawa unatetea vitu ambavyo jamii kwa upana wake inaona haviko sawa.
Hiyo clip anachoongea Makamba ni upuuzi mtupu.
Ngoja niulize.....
Anapoongea kwa kusema eti wao wameona mbele zaidi kwa kusaini mkataba mpya wa ujenzi wa njia za usambazaji umeme (Distributions)kutoka bwawani kuingia kwenye gridi ya Taifa.
:Badala ya kukalia tu kwenye ujenzi wa bwawa lenyewe"
Anamaanisha nini?
Anataka kutuaminisha watanzania kwamba
Serikali ya awamu ya Tano ilisaini mkataba wa ujenzi wa Bwawa bila kuwa na mpango wa connection ya usambazaji (distribution)?
Hilo lisingewezekana,maana hata Masanja Kadogosa wa SGR kila siku anapoelezea maendeleo ya mradi wake.
Pia huongelea ujenzi wa vituo vya kupokelea umeme kutoka Bwawa la Nyerere.
Labda Makamba anachofanya hapo ni yaleyale ya kusaini mikataba mipya ili kuweka 10% yake?
Kama tunavyomuona akifanya tangu ameshika wizara hii.
Mbona kwenye hiyo clip haongelei rasmi ni nini kinaendelea na kimefikia wapi kwa sasa?
Huyu ni waziri mpigaji hata Body language yake inaonyesha jinsi anavyotafuta cha kuongea ili kisitibue mpango wake.
mayalla unaheshimika ila angalia usitetee wataokuja kuchafuka na hivyo mkachafuka woote pamoja.
Ahsante.