Ni ajabu, serikali ya Tanzania kukopesha fedha mwanafunzi anaeanza chuo na kumnyima mkopo aliyemaliza chuo

Ni ajabu, serikali ya Tanzania kukopesha fedha mwanafunzi anaeanza chuo na kumnyima mkopo aliyemaliza chuo

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,783
Reaction score
2,396
Viongozi wa Tanzania, yaani unamkopesha fedha mwanafunzi anayeanza chuo ambaye hana uhakika nae kama atamaliza chuo na kupata kazi halafu unamnyima MKOPO wa biashara mwanafunzi aliyemaliza chuo au kunakuwa na mazingira magumu ya kupata mikopo ya biashara benki na kuwaambia wakajiajiri , je,hii ni akili kweli?

Viongozi wa serikali ya Tanzania wajitathimini juu ya kuwawezesha vijana wanaomaliza vyuo kupitia elimu zao kwa kuwapa mikopo ya kujikwamua unakuta kijana anaweza kufanya kazi fulani lakini kikwazo ni pesa na akienda benki au serikalini kuomba mkopo anaambiwa hana uzoefu wala dhamana sasa atapataje uzoefu na dhamana bila kufanya hiyo kazi?

Akajiajiri kwa kutumia nini?
 
Hakuna cha kushangaa hapo kwa aina viongozi uliokuwa nao. Kiongozi yeyote yule makini lazima awe na mission na vision. Bahati mbaya hao viongozi wako uliwauliza sasa hivi nini maana ya mission na vision; hata hawaelewi!
 
Niliwahi kushauri nikatukanwa nilisema serikali iwe na extension ya mkopo mfano wanafunzi wanapohitimu waendelee kupewa mkopo wa kujikimu mwaka mmoja mbele ili wajiongezee mtaani.
 
Niliwahi kushauri nikatukanwa nilisema serikali iwe na extension ya mkopo mfano wanafunzi wanapohitimu waendelee kupewa mkopo wa kujikimu mwaka mmoja mbele ili wajiongezee mtaani.
Wazo zuri , na wangeanzisha mpango wa kuwapeleka nje ya nchi kwa mkopo maana huko ajira na fursa zipo nyingi.
 
Back
Top Bottom