Ni asilimia 21 tu zitaenda kwa Wazanzibari katika Nafasi 1,097 za kazi kutoka TRA, marekebisho yanahitajika

Kwanza hizo nafasi 250 nyingi sana. Huu ni upendeleo mkubwa kwa zanzibar. Ukiangalia mlinganisho wa idadi ya watu bara na zanzibar inatakiwa zanzibar watengewe nafasi kama 24 tu.
 
Sasa mkoa upewe ngapi? Hata hizo nyingi sana
 
Usizungumze kitu huna uhakika nacho

Nna Ndugu zangu wengi Sana wanafanyakazi Zanzibar...tena serikalini kabisa
Wengine wametokea Iringa huko hata Dar hawaijui
Hao ni very few and exceptional hao hawakosekani tofauti na wao wanapopata faida nyingi na upendeleo tofauti na watanganyika and yet hu complain daily kuwa muungano umewameza
 
Huu muungano una siri kubwa, nyerere alishasaini mikataba...inshort siku tukiachana na Zanzibar kesho yake Oman wanatia kambi kuitawala na inakuwa New york ya East Afrika
Inaweza hata isiwe hyo new York ya Africa basi tu enzi hzo miungano ilikuwa influenced na mambo ya cold war Zaid and security purposes mengine hayana mashiko
 
Kama TRA ni moja mbona ukitoka kule kuja huku unalipishwa tena.?
 
Hao ni very few and exceptional hao hawakosekani tofauti na wao wanapopata faida nyingi na upendeleo tofauti na watanganyika and yet hu complain daily kuwa muungano umewameza

Asilimia 80 ya wafanyakazi wa mahoteli Zanzibar wanatoka Bara...
Hii unayosema very few umeitoa wapi?
 
Asilimia 80 ya wafanyakazi wa mahoteli Zanzibar wanatoka Bara...
Hii unayosema very few umeitoa wapi?
Hotel kazi za darasa la saba mkuu, ni cheap labor hyo ka house girl tu, huwezi linganisha na wataalamu
 
Kero zake hazitaisha milele[emoji23][emoji23]
Sure maana haueleweki hasa nini kipo hapo katikati huku watanganyika tuko isolated huku one side ikibenefit na ndio kinara wakulalamika
 
TRA mi kazi ya maana kwa wengi maana inahuusisha madili na rushwa! Lakini kama ni mshahara tu ni kazi ya kawaida!
Yes ni kazi ya kawaida ila huwezi linganisha na uhotelier mkuu. Hyo kazi ni roho ya nchi kwenye kukusanya mapato ukiacha notion ya wapiga hela na rushwa
 
Hotel kazi za darasa la saba mkuu, ni cheap labor hyo ka house girl tu, huwezi linganisha na wataalamu
kiukweli ilibidi iwe 50 % pasu kwa pasu, hii 21 ya kinyonyaji, Ni haki ya kuwa na usawa kwa pande zote mbili kwenye muungano.
 
Hotel kazi za darasa la saba mkuu, ni cheap labor hyo ka house girl tu, huwezi linganisha na wataalamu

Ajira ni ajira tu. Hata house girl akitoka nje ya Tanzania lazima apate kibali cha uhamiaji. Kwa hiyo mtu anaetoka Tanzania bara kufanya kazi Zanzibar bila kusumbuliwa na uhamiaji. Hapo maana yake amepewa upendeleo. Wanapohesabu ajira wanahesabu yeyote alieajiriwa hata kama ni mpika chai ama mfagiaji.

Pia Zanzibar ni nchi kamili. Sio sawa na mwanza ama mbeya..

Jiulize why Zanzibar lazima iwe na raia wake katika vyeo viwili vya juu kila awamu yaani mgombea urais na mgombea mwenza wa Tanzania ni lazima mmojawapo atoke zanzibar kila awamu. Mbona mbeya wala morogoro hawatoi mgombea urais ama mgombea mwenza kila awamu. Ama unahisi hawapendi hivyo vyeo vya juu?
 
Hotel kazi za darasa la saba mkuu, ni cheap labor hyo ka house girl tu, huwezi linganisha na wataalamu


Kwani si TRA wana kusanya Hadi Zanzibar?
Wavunje TRA isiwe ya Muungano
Wa Zanzibar wawe na TRA Yao..

Hapo ndo tuhoji why iajiri Wazanzibar?

Binafsi siku zote natamani Muungano ufe...
Wewe unahisi Zanzibar ndo inafaidika..
Wengine tunaamini Zanzibar ndo inafanywa masikini na huu Muungano
 

Ukweli huu muungano wa Zanzibar hawautaki kabisa. Ila wa bara ndio tunautaka.

Halafu humu vilaza wengi hawajui Zanzibar = Zanzibar only. Huku Tanzania = Tanganyika + Zanzibar.

Yaani bila Zanzibar hakuna Tanzania. Na hapo TRA ni Tanzania revenue authority .kila taasisi yenye neno Tanzania m Zanzibar ana haki ya kuajiriwa napo maana yeye ni m Tanzania

Lakini m Tanganyika ama mbara hana haki ya kuajiriwa Zanzibar revenue authority sababu neno Zanzibar halimuhusu yeye mbara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…