Ni Aya au story gani katika quran au Biblia zilizokusaidia wakati wa shida au kufaulu mitihani ya maisha?

Ni Aya au story gani katika quran au Biblia zilizokusaidia wakati wa shida au kufaulu mitihani ya maisha?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Lengo la hivi vitabu ni kukusaidia kuvuka hatua moja ya chini kwenda nyingine bora ya juu. Vikitumika nje ya hapo ni matumizi mabaya.

Mimi
Aya hii iliwahi kunisaidia kipindi ninaumwa na sikuwa na msaada wa karibu. Nilipona bila kwenda hospitali nikiamini Kila ninachokula na kunya hata kama hakina virutubisho kikiingia kinatoa ugonjwa wangu.

Kutoka 23:25
Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
 
Nilikuwa na UADUI mkubwa na GENTAMYCINE aya hii ikafanya awe rafiki yangu.
IMG_20231026_175858.jpg
 
Lengo la hivi vitabu ni kukusaidia kuvuka hatua moja ya chini kwenda nyingine bora ya juu. Vikitumika nje ya hapo ni matumizi mabaya.

Mimi
Aya hii iliwahi kunisaidia kipindi ninaumwa na sikuwa na msaada wa karibu. Nilipona bila kwenda hospitali nikiamini Kila ninachokula na kunya hata kama hakina virutubisho kikiingia kinatoa ugonjwa wangu.

Kutoka 23:25
Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
Hakika wema na fadhili zitanifuata, nami nitakaa nyumbani mwa BWANA siku zote
 
Sala za kuomba ulinzi na msaada wa nguvu za kimwili na kiroho kwa Mungu dhidi ya Maaduii.

Zaburi 91, 69, 70, 71, 140.

Kumsifu Mungu.

Zaburi 145, 118.

Methali 16.

Vitabu vya Zaburi na Methali ni vya kusoma kila siku.

Visa vya Wana wa Israel, Manabii na ufunuo wa siku za mwisho vinavutia sana kusoma.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mhubiri 3:1

[1]Kwa kila jambo kuna majira yake,
Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

To every thing there is a season, and a time to every purpose under the heaven:
We Jamaa ulipotelea wapi?

Hii dunia, eti Mtu anajiita "Kichwa kichafu" ilihali anasoma Biblia [emoji16]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Zaburi 35

1 Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami.

2 Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie.

3 Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.

4 Waaibishwe, wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya.

5 Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha chini.

6 Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa Bwana akiwafuatia.

7 Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.

8 Uharibifu na umpate kwa ghafula, Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe; Kwa uharibifu aanguke ndani yake.

9 Na nafsi yangu itamfurahia Bwana, Na kuushangilia wokovu wake.

10 Mifupa yangu yote itasema, Bwana, ni nani aliye kama Wewe? Umponyaye maskini na mtu aliye hodari kumshinda yeye, Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.

11 Mashahidi wa udhalimu wanasimama, Wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12 Wananilipa mabaya badala ya mema, Hata nafsi yangu ikaingia ukiwa.

13 Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu.

14 Nalijifanya kama kwamba ni rafiki au ndugu yangu, Naliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye.

15 Lakini nikijikwaa hufurahi na kukusanyana, Walinikusanyikia watu ovyo nisiowajua, Wananipapura wala hawakomi.

16 Kama wenye mzaha wakikufuru karamuni Wananisagia meno.

17 Bwana, hata lini utatazama? Uiokoe nafsi yangu na maharabu yao, Na mpenzi wangu na wana-simba.

18 Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi.

19 Walio adui zangu bure wasinisimange, Wanaonichukia bila sababu wasining'ong'e.

20 Maana hawasemi maneno ya amani, Na juu ya watulivu wa nchi huwaza hila.

21 Nao wananifumbulia vinywa vyao, Husema, Ewe! Ewe! Jicho letu limeona.

22 Wewe, Bwana, umeona, usinyamaze; Ee Bwana, usiwe mbali nami.

23 Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu.

24 Unihukumu kwa haki yako, Ee Bwana, Mungu wangu, Wala wasinisimangize.

25 Wasiseme moyoni, Haya! Ndivyo tutakavyo; Wasiseme, Tumemmeza.

26 Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu.

27 Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe Bwana, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.

28 Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa.
 
Sala za kuomba ulinzi na msaada wa nguvu za kimwili na kiroho kwa Mungu dhidi ya Maaduii.

Zaburi 91, 69, 70, 71, 140.

Kumsifu Mungu.

Zaburi 145, 118.

Methali 16.

Vitabu vya Zaburi na Methali ni vya kusoma kila siku.

Visa vya Wana wa Israel, Manabii na ufunuo wa siku za mwisho vinavutia sana kusoma.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Asante sana. Hizi nitazifanyia kazi.
 
Back
Top Bottom