MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Nimeshangaa kusoma kwamba eti kiongozi wa klabu ya Biashara anasema anachojali “ni fedha tu za Udhamini wa GSM, na hayo mambo mengine hayawahusu”. Hicho ni kiwango kikubwa cha kutojua wajibu wake kama kiongozi wa klabu ya Ligi Kuu, haki za klabu hiyo na vyanzo vya mapato.
.
Kwa kiongozi kama huyo unaona dhahiri ni kwa sababu gani Biashara ilishindwa kwenda Libya kucheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho baada ya kushinda 2-0 nyumbani. Na unaona dhahiri sababu za timu hiyo kwenda kwa mbinde Djibout kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho.
.
Hawa si aina ya viongozi wanaotakiwa kuongoza klabu za Ligi Kuu kama upeo wake wa masuala ya udhamini, uwazi na haki za klabu ni mdogo kiasi hicho. Lakini ni muhimu pia kwa Bodi ya Ligi kuanza kukuza chapa ya Ligi Kuu kama bidhaa yake kubwa badala ya kung’ang’ania mfumo wa zamani wa udhamini.
.
Haiwezekani Ligi Kuu ikawa na wadhamini wakuu wawili, mmoja akiwa amedandia gari wakati safari imeshaanza. Ni kituko kingine hicho.” - Angetile Osiah.