Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

Matundulu Express la Dar - Katoro linakutu inatudondokea abiria kutoka darini....yani unatoka ubungo kufika kimara tu kutu imeshajaa kwenye mfuko wa shati, unamwaga na kuendelea na safari. Sitalisahau
[emoji23][emoji81][emoji119][emoji119] nyiee hapana aisee
 
ilikwenda bure mzee maana hiyo lipa number huwezi hata kureverse transaction...lakini bado nakumbuka lipa number ya mabasi ya abc ni ya somebody ngairo. ni mfumo wa kitapeli tu
Mifumo ya usafilishaji ni aibu bado sana bongo matapeli wwngi mno
 
Happy nation, jamani lile gari siti ndefu ukikaa huwezi kunyoosha miguu kabisa, alafu bovu ,linanyata , Dar to Mbeya tulifika saa tano usiku, Ila Rungwe ndo balaa, Dar to mbeya tulifika saa sita usiku.
Kuna mabasi ya aina tofauti kutegemea umri yako ya vijana huenda spidi ya mwewe yako ya watu wa makamo na wazee

Hilo happy nation la Mbeya ni kwa ajili ya wazee ulijichanganya ungepanda Sauli

Kama wewe kijana panda happy nation ya kwenda Bukoba uone mziki wake ndio huwa la kwanza kufika Bukoba toka Dar
 
Matundulu Express la Dar - Katoro linakutu inatudondokea abiria kutoka darini....yani unatoka ubungo kufika kimara tu kutu imeshajaa kwenye mfuko wa shati, unamwaga na kuendelea na safari. Sitalisahau
🤣
 
Mwaka 2006 nilipanda basi ya Mohammed Trans kutoka Dar kuelekea Mwanza, safari ilianza vizuri tu kuanzia Dar hadi Dodoma hakukuwa na shida yoyote, kufika Manyoni ilikuwa bado ni vumbi kipindi hicho ikaanza kunukia ile harufu ya vyuma (Madereva na mafundi watanielewa hapa) lakini basi iliendelea kutembea hivyo hivyo. Nilikuwa nimekaa upande wa kushoto seat No. 45 kutoka mbele ndipo zilipo tairi za nyuma. Tukapita Ikungi hadi ilikuwa imebaki kama 20km kufika Singida mjini ndipo tairi zote mbili za nyuma upande niliokaa zilichomoka na kuelekea porini huku nikiwa naziona jinsi zilivyokuwa zikikimbia [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23]
Dah! Aisee basi iliserereka na kusimama.
Watu wote tulishuka kwenye basi kufika chini iligundulika kuwa stadi zote zimekatika!! Hiyo ilikuwa jioni majira ya saa 11 hivi. Tulikaa pale hadi saa 2 usiku. Tangu siku hiyo niliichukia sana kampuni ya mabasi ya Mohammed Trans
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Nacheka kama mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…