Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

Air Msae enzi hizo, Arusha - Dar

Tulipofika tu Moshi stendi pale, safari ikaingia kutu maana gari ikaanza mwaga oil kama mtu anayetapika...

Huku na kule injini ikashushwa na mchezo ukaishia hapo...
Aiseee hamkufaulishwa
 
Hao ni City Boys. Walifungiwa kufanya biashara baada ya kifungo kuisha wakarudi
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hawajaachana mbali na Saibaba [emoji28][emoji28]

Mara ya pili tena kupanda Msae ikajifia maeneo ya Kibaha barabara ya zamani, wakati huo barabara ya Dar - Chalinze inajengwa upya...

Nikaapa sipandi tena hilo basi, maana mara zote mbili nimeishia kupata nalo majanga
 
SAIBABA,
Nilikua nasafiri kutoka dar kwenda arusha kwaajili ya interview, safari jumapili interview jumatatu,

nilikata tiketi siku mbili kabla ya safari, siku ya safari nafika stand wananiambia gari yangu imeondoka wananipa gari nyingine ya saa mbili, kumbe gari halijaondoka ila lilikua halijajaza, nimekaa kwenye gari hadi saa8 mchana ndio inatoka wakasema ata kama saa6 usiku lazima tuingie arusha siku iyoiyo,
mwendo tuliokua tunaenda njiani kama msafara wa msiba wa malkin Elizabeth
Tunafika same saa6 usiku dereva na konda wakatuacha kwenye gari wakaenda kulala wanapojua wao wanarudi saa2 asubuhi jumatatu, tunaingia arusha saa6 mchana nikafika hadi sehemu tuliyotakiwa kufanya interview nimechelewa na watu wote wameondoka ilikua chuo cha uhasibu arusha.
Iyo safari sitaisahau na SAIBABA sitalisahau.
 
Sasa interview ilikuaje mkuu
 
Duh walikukatili sana *****
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…