Saibaba washawahi kunikatisha tiketi kwenye basi lao zuriii chuma iko inaunguruma tunasubiria saa 12 ifike tuanze safari, mara tukashushwa wanasema dereva sijui hayupo, tukapelekwa kwenye saibaba lengine bovu lilikuwa sijui linaenda Songea aisee gari imejaa mende na kunguni, inapakia abiria kama daladala kila kituo inasimama, ndoo kama zote ndio nikajua kumbe hizi ndoo ni seats pia.
Kilichoniuma niliacha Chaula mpya nikasema nibadili upepo halafu kwa nauli ileile nikasafirishwa na gari bovuuu limejaa kunguni na hata pipi hatukupewa. Na bado niliposhushwa ilibidi nichukue boda tena mpaka nyumbani wakati ningepanda Chaula ingeniacha mahali ambapo ningetembea kwa mguu tu nisingeingia gharama za boda.
Na huo ndio ukawa mwisho wangu kupanda saibaba. Yani kuna makampuni nimeya blacklist ikiwemo saibaba.