Ni basi gani zuri la Dar - Mwanza ambayo hailali Morogoro, huduma nzuri na luxury?

Ni basi gani zuri la Dar - Mwanza ambayo hailali Morogoro, huduma nzuri na luxury?

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
5,082
Reaction score
20,806
Naomba msaada wa kufahamu gari nzuri ya Mwanza -Dar ambayo hakuna kulala Morogoro. Watu wengine wanasema Dar Lux, wengine Ally's na wengine Happy Nation.

Naomba wenyeji mnisaidie kujua ipi nzuri hapo na ya uhakika.

Natanguliza shukrani.
 
Nakushauri kama una fedha ya kutosha panda Air Tanzania, achana na mabasi yanalala Morogoro labda kama wanavunja sheria. Itaakuwaje Kamanda akichachamaa siku unasafiri? Utalala njiani.
 
Hakuna gari inayolala Morogoro siku hizi.

Miezi kama miwili iliyopita nimepanda basi lililotokea Nyanda za huko nikajiunga nalo saa 1 usiku pale nanenane Dodoma na tukaingia Dar saa 9 alfajiri
 
Hiyo route haina luxury buses, kuna mfano wa luxury buses tu.
 
Darlux full AC mwendo wa wastani unaenyoy safari
pia kuna Isamilo mpya kabisa nauli 50,000/ndiyo nakuja nayo Dar,Moro tumeshapita kitambo ,tunaitafuta Chalinze.
 
pia kuna Isamilo mpya kabisa nauli 50,000/ndiyo nakuja nayo Dar,Moro tumeshapita kitambo ,tunaitafuta Chalinze.
Jamani kwa kweli hizi vipima mwendo ni mateso yani unakaa kwenye gari kila style kila kitu kinauma.

Yani sa 4 hii ndio mpo chalinze huku kipindi kile Mwanza -Dar sa 7:30 upo ubunge unafika unakuta taarifa ya habari bado.
 
Back
Top Bottom