Ni benki ipi nzuri kupokelea mshahara kati ya CRDB na NMB?

Ni benki ipi nzuri kupokelea mshahara kati ya CRDB na NMB?

mamba1

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2015
Posts
466
Reaction score
248
Naomba msaada kuhusu ni benki nzuri inayotoa huduma kiurahisi kati ya Nmb na Crdb naaamanisha kuwahi kutoa pesa mapema ya mshahara
 
Naomba msaada kuhusu ni benki nzuri inayotoa huduma kiurahisi kati ya Nmb na Crdb naaamanisha kuwahi kutoa pesa mapema ya mshahara
Duuh!! Hivyo unataka mshahara ukitoka tu uwe wa mwanzo mwanzo kupata. Teh.

Nenda NMB Mkuu.
 
CRDB ndo benki bora, haina foleni na mikopo yao masharti nafuu.

nipo na crdb miaka 10 sasa... makato mengi yapo relatively the same. wakizidi ni sh 150
 
CRDB ndo benki bora, haina foleni na mikopo yao masharti nafuu.

nipo na crdb miaka 10 sasa... makato mengi yapo relatively the same. wakizidi ni sh 150
Hapa natofautiana na wewe. CRDB haifai tena, inarudi nyuma na nadhani wana muda sasa wameanza kupiga roba za mbao.
 
Mimi pia nimeajiriwa na nafanya biashara ya huduma za kifedha hivyo nitakushauri alafu utachagua mwenyewe:

Kwa nini NMB?
1. Huduma zao zinapatikana sehemu nyingi sana. Maeneo mengi branch zao zipo kila mahali. Mawakala wao pia wanapatikana kwa urahisi.

2. Mtandao wao haukwami kwami. Ni mara chache kukosekana kwa mtandao wa NMB.

3. Huduma kwa mteja wanajitahidi sana kupata majibu kwa wakati kulinganisha na CRDB.

4. Upatikanaji wa mikopo kwa hivi karibuni ni haraka kulinganisha na CRDB zinazochukua muda mrefu hata kama umetimiza vigezo vyote.

5. Salary Advance unapata kwa haraka sana kulinganisha na kule kwingine.

Kwa nini CRDB?
1. Huduma yao ya Simbanking inakuwezesha kutoa mpaka 10M bila kadi. Kulinganisha na NMB ambayo cardless ni limited to 1M.

2. Gharama zao za utoaji fedha kwa mawakala ni nafuu kulinganisha na NMB.

3. Ukitaka huduma ya internet banking unapata bila longolongo.

Basi, chaguo ni lako.
 
Back
Top Bottom