Ni benki ipi nzuri kupokelea mshahara kati ya CRDB na NMB?

Ni benki ipi nzuri kupokelea mshahara kati ya CRDB na NMB?

Naomba msaada kuhusu ni benki nzuri inayotoa huduma kiurahisi kati ya Nmb na Crdb naaamanisha kuwahi kutoa pesa mapema ya mshahara
NMB ni wazuri kwa sababu tu wana matawi nchi nzima na wilaya zote,ila hawa jamaa wana wizi wa siri siri mnoo,vi buku 10,10 kupotea kwenye akaunti ni kawaida san.
NAKUSHAURI>pitishia mashahara NMB then fungua akaunti benki nyingine ya kutunzia fedha zako faida ya kupitishia mshahara NMB ni kwa ajili ya mahitaji ya mikopo siku za usoni maana wana mikopo ya fasta fasta.
 
Anatumia nmb lakini mishahara inalipwa na hazina?
Wewe nenda tu huko CRDB! Ila baadae usije tena kulalamikia makato yasiyo eleweka kwenye hiyo akaunti yako. NMB ina unafuu sana ukilinganisha na hiyo CRDB.
 
Kama Unataka mpunga mapema CRDB wapo vizuri Ila kwa makato yao na Hali hii ya TOZO nakushauri nenda NMB tu.
 
Nje na hapo. Vipi mshahara umetoka tayari?
 
Mishahaa inatolewa hazina maanake kuna watu wananambia Crdb unaweza kukaaa hata siku tatu bila pesa je ni ya kweli
 
Nipo crdb toka 2015. Mshahara tunapokea siku moja wote haijalishi upo tawi gani kwasababu kwa Sasa mishahara inatoka hazina. Suala la makato huwa naskia huko Nmb ukiacha buku 5 mwezi ujao huikuti wanaiba kitu ambacho crdb hakipo. Katika suala la mikopo crdb ndio the best hasa mshahara ukiwa unapita kwao. Masuala ya foleni mwisho wa mwezi ndio kero kubwa na wakati mwingine huwa tunakuwa Kama tunadharaulika Sana mwisho wa mwezi. Utakutana na lugha za kejeli Sana kila mwisho wa mwezi. So nakushauri nenda crdb huta juta kwa huo uamzi. Kuna watu nipo nao hapa kazini wengine wanampango wa kuhamia crdb
 
Hivi Kuna utofauti wa kupokea pesa kati ya NMB na CRDB? kama watu wanaofanya kazi serikalini lakini mmoja anatumia NMB na mwengine CRDB, je mshahara ukitoka mmoja anaweza kuwahi kupata na mwengine akachelewa?
 
Back
Top Bottom