Mimi pia nimeajiriwa na nafanya biashara ya huduma za kifedha hivyo nitakushauri alafu utachagua mwenyewe:
Kwa nini NMB?
1. Huduma zao zinapatikana sehemu nyingi sana. Maeneo mengi branch zao zipo kila mahali. Mawakala wao pia wanapatikana kwa urahisi.
2. Mtandao wao haukwami kwami. Ni mara chache kukosekana kwa mtandao wa NMB.
3. Huduma kwa mteja wanajitahidi sana kupata majibu kwa wakati kulinganisha na CRDB.
4. Upatikanaji wa mikopo kwa hivi karibuni ni haraka kulinganisha na CRDB zinazochukua muda mrefu hata kama umetimiza vigezo vyote.
5. Salary Advance unapata kwa haraka sana kulinganisha na kule kwingine.
Kwa nini CRDB?
1. Huduma yao ya Simbanking inakuwezesha kutoa mpaka 10M bila kadi. Kulinganisha na NMB ambayo cardless ni limited to 1M.
2. Gharama zao za utoaji fedha kwa mawakala ni nafuu kulinganisha na NMB.
3. Ukitaka huduma ya internet banking unapata bila longolongo.
Basi, chaguo ni lako.