Ni biashara gani inaweza ingiza atleast faida ya TZS 5M kama nikiwekeza TZS 30M?

Ni biashara gani inaweza ingiza atleast faida ya TZS 5M kama nikiwekeza TZS 30M?

Mtaji huu upeleke remoteness. Peleka bidhaa huko! Kariakoo hiyo hela ya maji tu... Huwez kufika kokote unless ukodi ukuta kama machinga.

Jikite na remoteness tu
 
Biashara kwenye makaratasi faida ya mill 5 inapatikana ila kiuhalisia net profit halisi kwa mtaji huo ni mill 3 kwa biashara za kuuza jumla hapo umetoa kila kitu tra,wafanyakazi ,Kodi ya pango ,na loss kitu kisichokwepeka kwenye biashara mill 3 unaipata
 
Kua na mtaji ni kitu kizuri kwenye biashara

Lakini kitu kikubwa sana kuliko vyote ni idea, passion na commitment

Ukiambiwa biashara ya machungwa inalipa sana...... je unaijua undani wake, umefanya utafiti wakina kuijua? Je ni kitu unakipendelea kufanya au sababu umeambiwa kuna faida?
Je ume dedicated kukomaa vijijini kukusanya mzigo iwe jua iwe nvua nk nk

Ukifanya biashara ambayo huna passion nayo lazima utakwama tu
Anza kujiuliza wewe sababu hakuna anayekujua vizuri zaidi ya wewe mwenyewe

Kama unapenda kazi za kukaa kwenye kaofisi na feni basi angalia biashara za kuuza makorokoro ya simu kama makasha, chaji na waya za simu, headphones, betrii, screen protector nk nk
Tafuta fremu sehemu iliochangamka watu weka biashara yako

Kama unapenda biashara za mazao ila upendi kusafiri fungua biashara ya mazao kama mchele unga maharage nk
Uza rejareja na jumla

Kama unapenda na unaweza pori to pori biga biashara ya mazao ya kuoza(kama nyanya) ni risk lakini ikikubali unakutoa haraka
Au biashara ya nafaka mikoani unaleta dar nk

Kitu cha kwanza ni wewe unapenda nini
Hakuna kitu kizuri kufanya biashara kwenye kitu una passion nacho utafanya kwa bidii huku una enjoy
Pili hakikisha unaijua kiundani biashara unayotaka kuifanya
 
Habari wana jf,

Naomba mwenye business idea ambayo nikiwekeza 30m naweza pata faida ya atleast 5m per month.
Nunua daladala kubwa weka route ya Mbezi...Mpigi magohe au Mbezi...Msumi.
Makusanyo kwa siku 250,000 = 7,500,000 kwa mwezi....Sasa hapo zikitokea hadithi huwezi kosa 5m.
Angalizo....kama ukiweza kukomaa mwenyewe ndio hela utaiona
 
Unaweza ukafafanua kidogo hiyo remoteness mkuu?
Baharesa huwa ananunua maembe pale mwandege. Kuna bro wangu anayakusanya huko lindi mpaka pwani kwenye gari anaenda kuuza pale. Ukishauza tu kwa mtaji wa million 3 unapata million Moja juu hapo hapo.

Maeneo ya vijiji hata ukifungua duka kubwa unakula pesa sana mana nauza huwa makubwa. Fursa vijijini zipo sana za kupata hela. Hata shibyabga Kuna maeneo yanaitwa Nindo! Huko wanahitaji bidhaa hasahasa vya matumizi. Wembe, juisi, keki keki hizi .. ubaya wa hayo maeneo ni mbali mnoo! Ndichi huko
 
Twende kitaalamu Ml 5 ni kama 21.8% kwenye Mil 30 sasa kwa nature ya biashara nyingi za hapa nchini biashara inayoweza kukupa faida ya asilimia hizo kulingana na mtaji uliowekeza Absolutely ni biashara ya chakula ila Cha kuzingatia ni eneo la biashara na namna utakavyoiweka biashara yako. Yangu ni hayo tu. Natanguliza shukrani👏
 
Baharesa huwa ananunua maembe pale mwandege. Kuna bro wangu anayakusanya huko lindi mpaka pwani kwenye gari anaenda kuuza pale. Ukishauza tu kwa mtaji wa million 3 unapata million Moja juu hapo hapo.

Maeneo ya vijiji hata ukifungua duka kubwa unakula pesa sana mana nauza huwa makubwa. Fursa vijijini zipo sana za kupata hela. Hata shibyabga Kuna maeneo yanaitwa Nindo! Huko wanahitaji bidhaa hasahasa vya matumizi. Wembe, juisi, keki keki hizi .. ubaya wa hayo maeneo ni mbali mnoo! Ndichi huko
shukran.
 
Juisi za matunda zote za baharesa huwa ananunua matunda yake kwa wafanyabisahara. Hata zile za mananasi, hayo maukwaju na mengine mengine. Muhimu ni kufatilia kwa undani wewe mwenyewe humo viwandani.

Binafsi najichanga hapa kupata mtaji ukifika ninaoutaka naenda palepalr kiwandan kupata neno kwa wahusika. Mana nataka kukusanya ukwaju, na na msimu wa maembe nabeba embe na nanasi.

Nataka kuanza kuyalima kabisa huko mkuranga. Hata Zanzibar watu wanatoboa na biashara hasa za matunda. Huku wanadili na mahoteli
 
Kuna vituo vya mafuta lakini havina mitaji hivyo ukiwa na mobile fuel truck unaenda depo unanunua jumla kisha unaenda ku supply kwa mali kauli.. Faida yako ni Tsh 100 kwa lita..
Asubuhi unasambaza lita zako 3000 jioni unakusanya hela zako.. Kwa mzigo wa lita 3000 faida ni Tsh 300,000.. Fanya supply kwa siku 5 tu za wiki una 1.5 safi kabisa the minimum

Kuhusu waste mfano wa waste ya Alminium
Unanunua kilo 4700 unaenda kuuza 5000.. Zidisha mara tani kisha toa faida
Tani 10 ni million 47 kununua kuuza ni milion 50 faida milion 3 kwa mwezi supply tani 20 tuu
 
Biashara kwenye makaratasi faida ya mill 5 inapatikana ila kiuhalisia net profit halisi kwa mtaji huo ni mill 3 kwa biashara za kuuza jumla hapo umetoa kila kitu tra,wafanyakazi ,Kodi ya pango ,na loss kitu kisichokwepeka kwenye biashara mill 3 unaipata
Huu ndo uhalisia labda aitupe kwenye kununua nafaka na hapo akauze kwa jumla mashineni sio Rahisi kupata faida ya 30m kutoka million 5 hata Mimi ingekuwa nanesa vibaya mno
 
Kuna vituo vya mafuta lakini havina mitaji hivyo ukiwa na mobile fuel truck unaenda depo unanunua jumla kisha unaenda ku supply kwa mali kauli.. Faida yako ni Tsh 100 kwa lita..
Asubuhi unasambaza lita zako 3000 jioni unakusanya hela zako.. Kwa mzigo wa lita 3000 faida ni Tsh 300,000.. Fanya supply kwa siku 5 tu za wiki una 1.5 safi kabisa the minimum

Kuhusu waste mfano wa waste ya Alminium
Unanunua kilo 4700 unaenda kuuza 5000.. Zidisha mara tani kisha toa faida
Tani 10 ni million 47 kununua kuuza ni milion 50 faida milion 3 kwa mwezi supply tani 20 tuu

Chuma ndio rahisi zaidi maana kipo kingi sana unanunua kwa 800 kilo unauza mpaka 1100
Kuna viroba Vikubwa (jafafa) unusual 5000 unauza 8000
Kuna oil chafu nknk
 
Habari wana jf,

Naomba mwenye business idea ambayo nikiwekeza 30m naweza pata faida ya atleast 5m per month.
Unajua Matajiri woote Dunani walitatua shida za watu, kwa hiyo na wewe unaweza kutoka kwa kutatua shida za watu. Mfano watu wana njaa unawauzia chakula, watu wanatembea uchi unawauzia mavazi,watu wanashida ya mbolea unawauzia hitaji lao.

Sasa kuhusu 30m kupata faida ya 5m inategemea uko wapi na kuna uhitaji gani.
Mfano:
Ukiwa Kibororoni pale Moshi 30m ukiingiza kwenye Kitimoto utapata hiyo 5m kama faida.
Ukiwa Mwanza hiyo 30m ukiingiza kwenye samaki utapata hiyo 5m kama faida.
Ukiwa Kahama Geita huko hiyo 30m ukiingiza kwenye Madini utapata hiyo 5m kama faida.
Ukiwa Dodoma hiyo 30m ukiingiza kwenye soko la Mbuzi na Kondoo Utapata hiyo 5m kama faida.
Ukiwa Singida hiyo 30m ukiingiza kwenye mafuta ya Alizeti unanunua unarifain na kuuza 5m inapatikana.

Katika vyote nilivyovitaja hapo juu kipo kitakachokusaidia. Juhudi na maarifa inatakiwa kwenye biashara.
 
Back
Top Bottom