Ni biashara gani uliwahi kuambiwa ukifanya utapiga pesa sana ila baada ya kuingia mchezoni ulibaki unajuta?

Ni biashara gani uliwahi kuambiwa ukifanya utapiga pesa sana ila baada ya kuingia mchezoni ulibaki unajuta?

Under-cover

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2023
Posts
1,834
Reaction score
3,042
Biashara ya kukopesha pesa yani ukimuona unae mdai kabeba begi yuko kwenye boda , inabidi na wewe uchukue boda fasta umfukuzie, mwisho unaona anaingia kwa dobi, inabidi upitilize na hujui unaelekea wapi.

Kudownload na kuinstall pesa.

Bajaji

Biashara ya kukopesha pesa, yani ukimuona unaemdai kabeba begi yuko kwenye boda, inabidi na wewe uchukue boda fasta umfukuzie, mwisho unaona anaingia kwa dobi

Kilimo cha matikiti.

Kilimo cha matikiti.
Kuna mwaka nilijaribu hiki kilimo... hakuna rangi niliacha kuziona.

Biashara ya kuuza peremende.

Ilinidodea kabisa

BIASHARA YA KUUZA POMBE ILA NILIPO OKOKA NA KUMPOKEA YESU KRISTO NA KUOKOKA NDIPO ALIPO NIONESHA BIASHARA AMBAYO MPAKA SASA NAPATA PESA NZURI TU

BIASHARA YA POMBE ILIKUWA NI KUPOTEZA TU MARA MATUSI,KUKOSWA NA CHUPA UGOMVI HERA KUPOTEA POTEA TU LAKINI BAADA YA YESU KUNIBADILISHIA NA KUNIPA BIASHARA SAFI NA ENJOY MAISHA

hiho hiashara ya horex! wazee wa bearish and bull..🤣

Kilimo cha kutumiwa picha kutoka kijijini wewe ukiwa mjini.

Naapa hii Dunia Ina rangi nyingi ni swala la mda tu kuanzia kuziona.

Hakuna biashara inayolipa zaidi ya unga zingine ziote kudanganyana

Kudownload na kuinstall pesa.
hio ni betting

Madini

Kudownload na kuinstall pesa.
Hii ni biashara gani

Hii ni biashara gani
ka forex hako ka chinjachinja!..🤣

ka forex hako ka chinjachinja!..🤣
Hahahaha aviator

hiho hiashara ya horex! wazee wa bearish and bull..🤣
Forex mtafute ontario sisi tumejifunziq huko

Forex mtafute ontario sisi tumejifunziq huko
mkuu jijibu kwa kusoma jina lako...😂

Wazee biashara sio lelemama fungua moyo

Kuna mwaka nilijaribu hiki kilimo... hakuna rangi niliacha kuziona.
Acha kabisa ni hatari sana. Ingawa sikufukia malengo ila kuna somo nililipata.

mkuu jijibu kwa kusoma jina lako...😂
KWaNNI KWANI NIMEKUJIBU VIBAYA ?
 
Biashara sio kwa ajili ya kila mtu aisee, wengine inabidi tulime wengine waajiriwe nk. Binafsi sijakutana na majuto zaidi ya kujifunza zaidi kuliko kujuta, kila kitu kwenye haya maisha kina changamoto na majuto kikija vibaya na namna gani ya kukabiliana nacho.
 
Mwaka 2019, kuna Rafiki yangu.. mmoja alikuwa Dodoma Anafanya biashara ya kuuza Nazi . Saba saba .

Bwana jamaa akanipanga. Nazi Dodoma itoka hatar..yaan ukishusha mzigo asbh Saa nne tu ume maliza mzigo..

Ha ha ha wee si nikatupia laki 9 yangu bwana. Ha ha ha mpaka leo mie huwez niambia biashara ina lipa nika ingia kichwa kichwa .
 
Kuna mtu alinishawishi tupeleke mafuta Zambia, mwisho wa siku gari lilipata ajali sijaambulia hata mia.. 🥹🥹🥹
Hiki kitu kila nikikumbuka lazima moyo uume halafu nilitoka kuchukua mkopo bank.
 
Nilinunua korosho tani 3 na nusu (kangomba)kg 1 nilinunua elf2 TANECU wanakuja kutangaza mnnada wa kwanza Inasoma Kg 1 Tsh 1800 hapo kabla ya makato ya vyama vya msingi.
Noma mm kipind cha magu tuliambiwa onyesha shamba tukapotea.

Ila saiv watapiga hela kilo elf 4.
 
Biashara ya mgahawa wa chakula...tena eneo ambalo lina watu wanafanya tayari doh!

Biashara ya forex mmmh sirudii tena
 
Biashara ya vinywaji..yaani juice fresh, maji, na soda, .....plus snacks safi sana hii tena si ghalama hata muhimu connection na watu na ubunifu
 
Back
Top Bottom