Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Nimeuza viazi vya mafungu na kwenye sado pale Temeke sterio sokoni hapo nipo chuo UDSM mwaka wa pili dah halafu najishangaa hata nilikuwa sioni aibu.. lakini leo marafiki zangu ndio wanaulizia ile biashara maana ninayofanya saivi ni tofauti na matarajio yao. Thanks god kwa kidogo ninachopata.
Nilivyo soma tu jina hapo juu nikayakubali maneno yako bila ubishi wowote
 
Watu tunapotezana, biashara ya mtaji mdogo eti mtu anakwambia stationary kweliiiiii?!

Biashara ndogo ni za mitaji isoyozidi laki, na hiyo laki iwe isha cover mahitaji ya biashara vikorokoro vyote.

Mfano mzuri ni picha iliyosindikiza hii thread, kuuza mahindi.

Jiko 15,000
Mkaa 5000
Mahindi 15000
wavu 7000
nk nk 10000

Ukipga total hapo hata laki hufikishi. Hizo ndio biashara ndogo tunazotaka kusiona kwenye hii thread.

Mtu anakwambia alikua anabetisha anabetishia watu mpk mkeka wa laki 3 na ana mashine mbili hivi hiyo ni biashara ndogo kweli!?

Hebu tujue tofautisha biashara ndogo na Biashara za wenye pesa wanazozifanya kwa udogo.

Nategemea kukutana na wauza mishkaki humu
wauza mahindi
wauza pweza
wauza karanga
wauza maji ya kandoro
wauza skrepa
wauza chupa za maji
nk nk nk

Nategemea kukutana na watu wa aina hyo ila nyie wengine mnatupoteza tu hapa mna hela kabisa tena muache ita biashara zenu ndogo maana mitaji tu mliyowekeza hapo wenzenu tunaimezea mate.

Naomba waliofanya biashara anazozimaanisha mleta thread muendeleee kuteremsha mambo, nyie wengine kausheni tu Thread hiii nategemea iwe na nondo ambazo atae ingia apate hamasa ila sio nyie mnaotutajia biashara za mamilioni mnatuambia et ni ndogo.
Noma
 
Kama huwez kutaja biashara yenyewe unatuambia Ili iweje?
 
Back
Top Bottom