Ni bora kununua gari yenye kilometa 200,000 kutoka Japan kuliko kununua gari yenye kilometa 50,000 Tanzania.

Hawa kina Doto magari ndo waharibifu wenyewe. Pia show rooms nao wanarudisha sana kilometa.

Jan Japan wako very real wanakupa hadi docs za mnada na service history file
Aisee nimenunua gari kwa mtu hilux 2.8D ya mwaka 2004, inetembea km 300k na hii gari mtu alinunua mwaka 2005 toyota tz mpya kabisa
Huwa najiuliza hizi ambazo watu wananunua kutoka nje gari ya mwaka 2000 au zaidi ila unakuta mileage 80k mpaka 120k sijui kana kwamba zinakua zimepaki tu au la.
 
H
Gari imetengenezwa 2002 halafu dalali anaonyesha imetembea 60,000 KM.

Tufanye haikupata mteja mpaka 2005.

So imetumika kuanzia 2005 mpaka 2024. Imekua barabarani kwa miaka 19. Kwa KM 60,000 hii ni kusema kila mwaka ilitembea 3157 KM.

Ikimaanisha kwamba hii gari tangu 2005 mpaka 2024 ilikua inatembea wastani wa 8 KM kwa siku.

Na hii ni kumaanisha huyu ni first user na wewe utakua second.

Mwisho inakua tatizo la umeme la gari lina tatizo jingine ambalo inabidi wewe na fundi wako mkatafute fundi mwingine.
Ha! Ha! Wazee wa probability mnawakabia madalaloi kwa juu! Maana sio kwa hesabu hizi
 
Hii ndoshida ya Bongo unakuta gari eti lina km 67000 ukiliangalia unajua wamechezana km
 
Wewe angalia gari imetengenezwa mwaka gani alafu soma mileage then chukua mwaka uliopo toa mwaka lililotengenezwa ukipata jibu chukua 365 zidisha kwa hiyo tofauti ya miaka alafu chukua mileage gawanya kwa jibu utakalo pata hapo.

Ukiona mileage ipo chini sana achana nalo wakileta mdomo waambie unakuja na machine kupima mwenyewe muone kama kweli waataka biashara. Alafu sikilizia watakavyo kuruka
 
Madalali wa magari nchini Tanzania kila siku wamekuwa wakiharibu biashara ya magari ya mkononi kwa kukosa elimu ya biashara.

Uaminifu, ukweli na uwazi ni msingi MKUBWA sana kwenye ukuaji wa biashara yoyote ndio maana kwa kulijua hilo, wenzetu wa nje hawarudishi nyuma kilometa ambazo zinasoma kwenye odometer, umbali ambao Gari imetembea.

Gari ambayo imeingia nchini ikiwa imetembea kilometa 102,005, wauzaji watailazimisha Gari hiyo isomeke kwamba imetembea kilometa 35,000 kitu ambacho ni uhuni na kukosa weledi.

Soko la ndani la magari linaharibiwa na wauza magari wenyewe.
Labda scania, lori au coaster ndo ununue iko na 200km Japan, ila gari ndogo ya kutembelea ni ujinga ukinunua hata gari ina 150,000 na ni uzembe kuchukua gari iliyo tembea saana
 
Una kiasi GANI? Pesa yako ndio determination ya Gari utakayonunua
 
Aisee nimenunua gari kwa mtu hilux 2.8D ya mwaka 2004, inetembea km 300k na hii gari mtu alinunua mwaka 2005 toyota tz mpya kabisa
Huwa najiuliza hizi ambazo watu wananunua kutoka nje gari ya mwaka 2000 au zaidi ila unakuta mileage 80k mpaka 120k sijui kana kwamba zinakua zimepaki tu au la.
Radiator zinapewa maji ya upako, na engine oil hutumia mafuta ya Mwamposa
 
Gari ambayo imetembea Japan zaidi ya km 100,000 ni gari nzuri kwasababu Japan gari ikifika km hizo huwa wanasheria zao za kuifanyia gari ukaguzi WA usalama wa gari ikiwemo service ya Kilakitu kibovu..

Kwa Japan kutembelea gari yenye milage kubwa ni gharama Sana ndiyo maana wamiliki wengi wanauza magari Yao kabla ya kuifikia km 100,000.
Wabongo wengi hawajui hiki kitu wanafikiri gari yenye milage ndogo ndiyo Bora kumbe ni kujidanganya. Gari zenye milage kubwa Kwa Japan ndiyo the best na wamiliki wa hayo magari ni maboss , kulipia vibali vya uchakavu Kwa Japan ni gharama Sana ndiyo maana ukiingia kwenye mtandao wa be forward na SBT utakuta gari iliyotembea milage kubwa inauzwa sawa na Ile yenye milage ndogo
 
Hapa wengi ikifikisha kilometa kuanzia 75,000 huacha kufanya service za maana kwani anavizia kabla ya 90,000 aitie sokoni
 
Mkiendelea kununua magari kwa kuangalia Mileage mtaendelea kudanganywa sana ukitaka gari angalia mwaka wa gari unaoutaka na taarifa za gari kuhusu services na ubora wa mashine yake kama una changamoto au la ila ukirukia kwenye Odometer au namba mtaendelea kupigwa tu..mtu ananunua gari ya mwaka 2000 eti ina 40,000 Mileage wakati nanunua Ford ranger SA ya mwaka 2017 inasoma 172,000 mimi nauza na hizo nilizopata nilipokua nanunua..
 
Huu ndio unaitwa uadiifu na uaminifu
 
Back
Top Bottom