becknature
JF-Expert Member
- Mar 9, 2017
- 665
- 825
Aisee nimenunua gari kwa mtu hilux 2.8D ya mwaka 2004, inetembea km 300k na hii gari mtu alinunua mwaka 2005 toyota tz mpya kabisaHawa kina Doto magari ndo waharibifu wenyewe. Pia show rooms nao wanarudisha sana kilometa.
Jan Japan wako very real wanakupa hadi docs za mnada na service history file
Ha! Ha! Wazee wa probability mnawakabia madalaloi kwa juu! Maana sio kwa hesabu hiziGari imetengenezwa 2002 halafu dalali anaonyesha imetembea 60,000 KM.
Tufanye haikupata mteja mpaka 2005.
So imetumika kuanzia 2005 mpaka 2024. Imekua barabarani kwa miaka 19. Kwa KM 60,000 hii ni kusema kila mwaka ilitembea 3157 KM.
Ikimaanisha kwamba hii gari tangu 2005 mpaka 2024 ilikua inatembea wastani wa 8 KM kwa siku.
Na hii ni kumaanisha huyu ni first user na wewe utakua second.
Mwisho inakua tatizo la umeme la gari lina tatizo jingine ambalo inabidi wewe na fundi wako mkatafute fundi mwingine.
Labda scania, lori au coaster ndo ununue iko na 200km Japan, ila gari ndogo ya kutembelea ni ujinga ukinunua hata gari ina 150,000 na ni uzembe kuchukua gari iliyo tembea saanaMadalali wa magari nchini Tanzania kila siku wamekuwa wakiharibu biashara ya magari ya mkononi kwa kukosa elimu ya biashara.
Uaminifu, ukweli na uwazi ni msingi MKUBWA sana kwenye ukuaji wa biashara yoyote ndio maana kwa kulijua hilo, wenzetu wa nje hawarudishi nyuma kilometa ambazo zinasoma kwenye odometer, umbali ambao Gari imetembea.
Gari ambayo imeingia nchini ikiwa imetembea kilometa 102,005, wauzaji watailazimisha Gari hiyo isomeke kwamba imetembea kilometa 35,000 kitu ambacho ni uhuni na kukosa weledi.
Soko la ndani la magari linaharibiwa na wauza magari wenyewe.
Una kiasi GANI? Pesa yako ndio determination ya Gari utakayonunuaLabda scania, lori au coaster ndo ununue iko na 200km Japan, ila gari ndogo ya kutembelea ni ujinga ukinunua hata gari ina 150,000 na ni uzembe kuchukua gari iliyo tembea saana
Radiator zinapewa maji ya upako, na engine oil hutumia mafuta ya MwamposaAisee nimenunua gari kwa mtu hilux 2.8D ya mwaka 2004, inetembea km 300k na hii gari mtu alinunua mwaka 2005 toyota tz mpya kabisa
Huwa najiuliza hizi ambazo watu wananunua kutoka nje gari ya mwaka 2000 au zaidi ila unakuta mileage 80k mpaka 120k sijui kana kwamba zinakua zimepaki tu au la.
Hapa wengi ikifikisha kilometa kuanzia 75,000 huacha kufanya service za maana kwani anavizia kabla ya 90,000 aitie sokoniGari ambayo imetembea Japan zaidi ya km 100,000 ni gari nzuri kwasababu Japan gari ikifika km hizo huwa wanasheria zao za kuifanyia gari ukaguzi WA usalama wa gari ikiwemo service ya Kilakitu kibovu..
Kwa Japan kutembelea gari yenye milage kubwa ni gharama Sana ndiyo maana wamiliki wengi wanauza magari Yao kabla ya kuifikia km 100,000.
Wabongo wengi hawajui hiki kitu wanafikiri gari yenye milage ndogo ndiyo Bora kumbe ni kujidanganya. Gari zenye milage kubwa Kwa Japan ndiyo the best na wamiliki wa hayo magari ni maboss , kulipia vibali vya uchakavu Kwa Japan ni gharama Sana ndiyo maana ukiingia kwenye mtandao wa be forward na SBT utakuta gari iliyotembea milage kubwa inauzwa sawa na Ile yenye milage ndogo
Huu ndio unaitwa uadiifu na uaminifuMkiendelea kununua magari kwa kuangalia Mileage mtaendelea kudanganywa sana ukitaka gari angalia mwaka wa gari unaoutaka na taarifa za gari kuhusu services na ubora wa mashine yake kama una changamoto au la ila ukirukia kwenye Odometer au namba mtaendelea kupigwa tu..mtu ananunua gari ya mwaka 2000 eti ina 40,000 Mileage wakati nanunua Ford ranger SA ya mwaka 2017 inasoma 172,000 mimi nauza na hizo nilizopata nilipokua nanunua..