Ni CCM tena CHADEMA yapigwa bao mchana kweupe

washenzi wakubwa nyie hamna hata aibu, yan nyie hamtaki upinzani wafanye siasa et kisa mnajenga uchumi wakati huo huo nyie mnafanya siasa kisa tu mna dora.

Kama nyie ni wanaume ruhusuni upinzani wafanye siasa muone kama hamtokuja kushangaa.
Mkuu upinzani unafanya siasa. CHADEMA wanaendelea na operesheni haki Tanzania bara na visiwani.
Vyama vya upinzani vinashiriki chaguzi ndogo katika majimbo na kata.
 
Mkuu usimezeshwe maneno. Propaganda za wapinzani kuhusu uchaguzi zinasikitisha sana.
CCM imejenga na kukarabati hospitali za rufaa, mikoa, wilaya na vituo vya afya. Umeme umepelekwa na unazidi kupelekwa katika vijiji na vitongoji, barabara za vijijini zinaenda kujengwa wa kiwango ambacho zitakuwa zinapitika wakati wote na mengine mengi.
Utendaji kazi wa CCM ni wa mfano na vyama vya upinzani zinatakiwa kujifunza kutoka CCM.

Kama hospitali zinafanya mtu kubaki madarakani, basi makaburu wa Afrika kusini wangekuwa madarakani mpaka leo. Miaka 60 mko madarakani hajafanya hayo mambo leo ndio mnajifanya mtayaweza?
 
Tukiwa wadogo tulionywa na wazazi pamoja na jamii kuwa katika jambo lolote ni lazima ujipange ili ufanikiwe na waswahili wakaongeza kwa kusema "Asiyekubali kushindwa si mshindani." CHADEMA wamekuwa wakisahau methali hii ya wahenga na kuwa wahanga katika mengi kwa sababu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa kikishindana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia kwenye uchaguzi ili waweze kushika dola na masuala mengine ya kichama lakini katika yote CHADEMA imekuwa ikishindwa.

Mnamo tarehe 27/05/2021 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa katika uzinduzi wa operesheni haki jijini Arusha alijipata na kusema "Tunataka tuwaonyeshe CCM namna watu wanaweza kufanya kazi kisayansi. Tutafanya kazi kidigitali. Tunakwenda kutoa kadi mpya za Chama chetu, kadi za kidigitali. Tutakuwa na kadi za aina tano kwenye Chama chetu, utajipanga uwe na kadi ya daraja (level) gani."

Mbowe aliwaaminisha wanachama na wafuasi wa CHADEMA kuwa kazi imeisha na wameshaishinda CCM katika eneo hilo la kidijitali na kusahau kuwa wahenga walisema "Usilolijua ni usiku wa giza" na "Jambo la ukucha halichukuliwi shoka." CCM ilishaanza safari ya usajili wa kadi za kielektroniki kwa wanachama wake tangu mwaka 2018 na kupitia mfumo huo wa usajili mwanachama wa CCM anatambuliwa kwenye mtandao kuanzia shina, tawi, kijiji, kata, wilaya na mkoa anakotokea sambamba na taarifa nyingine muhimu kwa ustawi wa Chama Cha Mapinduzi.

Ndg. Daniel Chongolo Katibu Mkuu wa CCM mnamo tarehe 08/07/2021 akiwa Sumbawanga mkoani Rukwa aliutaarifu umma wa watanzania kuwa CCM itaanza kutoa kadi za kielektroniki kwa wanachama mnamo mwezi wa nane (Agosti) mwaka huu (2021) na Makao Makuu ya CCM kadi hizo zitaanza kutolewa mwezi wa Saba mwishoni (Julai 2021).

CHADEMA imepigwa katika suala la kadi za kielektroniki na bado inapigwa katika suala la programu tumizi za Chama (CCM App Vs CHADEMA Digital), tovuti za vyama, kurasa na akaunti za mitandao ya kijamii.

Watanzania wote wanajua kuwa CCM inaanza na wengine wanafuata. Salamu hizi Freeman Mbowe amezipata kabla hajahamia kwenye lengo namba mbili (2) la CHADEMA SACCOS chini ya operesheni haki.

Siasa ni sanaa na siasa ni sayansi, nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Kazi Iendelee.​

View attachment 1857183
Mawazo na kauli ya ukemwenza. NI uzi wa kipuuzi.
 
Chama i

CCM Chama imara chenye viongozi wenye uzalendo wa kweli kwa watanzania. Siyo kama wale wanaotaka kushika dola halafu waweke madini na rasilimali za nchi hii rehani.
Maandishi yako haya yanapingana na hali halisi uijuayo,ndio maana maandishi yakagoma kuandikika hapo mwanzoni.
 
Unakiona CCM kipo sawa na vyama vya saisa ?

Mbona kipindi cha marehemu baadhi ya vikao vya chama vilifanyika ikulu?

Nenda tafuta clip ya Bashiru anasema watatumia dola kubaki madarakani utaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu vikao kufanyika ikulu sio suala geni. Inategemeana na majukumu mbalimbali ambayo yanaendelea, hata wewe nyumbani kwako mara moja moja unaweza kukutana na watu na kuzungumza nao.
Dkt. Bashiru alimaanisha utekelezaji wa ilani ya CCM 2015 - 2020 ambao ulifanywa kwa mafanikio makubwa ndiyo ambao ungeibakiza CCM madarakani kwa sababu mambo ambayo Serikali inayoundwa na CCM imeyafanya yanaonekana.
 
Kwani wewe Baraka Mina ndiye Anna Muungano !!??
Kwa nini unakuwa na ID mbili mbili!!??
Screenshot_20210719_150301.jpg
 
Unakiona CCM kipo sawa na vyama vya saisa ?

Mbona kipindi cha marehemu baadhi ya vikao vya chama vilifanyika ikulu?

Nenda tafuta clip ya Bashiru anasema watatumia dola kubaki madarakani utaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Dkt. Bashiru alimaanisha utekelezaji wa ilani ya CCM 2015 - 2020 ambao ulifanywa kwa mafanikio makubwa ndiyo ambao ungeibakiza CCM madarakani kwa sababu mambo ambayo Serikali inayoundwa na CCM imeyafanya yanaonekana.
 
Tukiwa wadogo tulionywa na wazazi pamoja na jamii kuwa katika jambo lolote ni lazima ujipange ili ufanikiwe na waswahili wakaongeza kwa kusema "Asiyekubali kushindwa si mshindani." CHADEMA wamekuwa wakisahau methali hii ya wahenga na kuwa wahanga katika mengi kwa sababu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa kikishindana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia kwenye uchaguzi ili waweze kushika dola na masuala mengine ya kichama lakini katika yote CHADEMA imekuwa ikishindwa.

Mnamo tarehe 27/05/2021 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa katika uzinduzi wa operesheni haki jijini Arusha alijipata na kusema "Tunataka tuwaonyeshe CCM namna watu wanaweza kufanya kazi kisayansi. Tutafanya kazi kidigitali. Tunakwenda kutoa kadi mpya za Chama chetu, kadi za kidigitali. Tutakuwa na kadi za aina tano kwenye Chama chetu, utajipanga uwe na kadi ya daraja (level) gani."

Mbowe aliwaaminisha wanachama na wafuasi wa CHADEMA kuwa kazi imeisha na wameshaishinda CCM katika eneo hilo la kidijitali na kusahau kuwa wahenga walisema "Usilolijua ni usiku wa giza" na "Jambo la ukucha halichukuliwi shoka." CCM ilishaanza safari ya usajili wa kadi za kielektroniki kwa wanachama wake tangu mwaka 2018 na kupitia mfumo huo wa usajili mwanachama wa CCM anatambuliwa kwenye mtandao kuanzia shina, tawi, kijiji, kata, wilaya na mkoa anakotokea sambamba na taarifa nyingine muhimu kwa ustawi wa Chama Cha Mapinduzi.

Ndg. Daniel Chongolo Katibu Mkuu wa CCM mnamo tarehe 08/07/2021 akiwa Sumbawanga mkoani Rukwa aliutaarifu umma wa watanzania kuwa CCM itaanza kutoa kadi za kielektroniki kwa wanachama mnamo mwezi wa nane (Agosti) mwaka huu (2021) na Makao Makuu ya CCM kadi hizo zitaanza kutolewa mwezi wa Saba mwishoni (Julai 2021).

CHADEMA imepigwa katika suala la kadi za kielektroniki na bado inapigwa katika suala la programu tumizi za Chama (CCM App Vs CHADEMA Digital), tovuti za vyama, kurasa na akaunti za mitandao ya kijamii.

Watanzania wote wanajua kuwa CCM inaanza na wengine wanafuata. Salamu hizi Freeman Mbowe amezipata kabla hajahamia kwenye lengo namba mbili (2) la CHADEMA SACCOS chini ya operesheni haki.

Siasa ni sanaa na siasa ni sayansi, nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Kazi Iendelee.​

View attachment 1857183
Umeshakula sasa?
 
Kupotosha vipi,matendo,maneno ya kundi ama kikundi hutoa tafsiri ya wao ni nani,tena kwa majina yaliyo wazi na rasmi kabisa.
Sawa alikuwa hajajipanga,Je agenda,zake za utetezi wa wa Tanzania,zinawafíkia walengwa ,haziwafikii,na je mafanikio ya ajenda hizo umeweza kuyaona au bado?wengine wanasema mahasimu Wanapigwa kwenzi za kidigitali,je hata hilo haulikubali?
Juzi kati hapa Mdude CHADEMA amemtukana Rais hadharani na kujiona mjanja. Watanzania bila kujali itikadi za kisiasa walimkemea.
Utetezi upi ambao unatuleta pamoja zaidi ya kushadidia masuala yenye manufaa kwake kisiasa. Rais alieleza wazi kuwa suala lile linahitaji subira lakini kama kiongozi haelewi.
 
Kawaida uonevu unapozidi jiandae kwa lolote,kunyamnyamazisha anaeonewa ni bora ukaongeza nguvu kwenye kumwonea ,ila sii kumdhihaki.
 
Bila TISS hakuna CCM na bila Polisi hakuna CCM na bila TBC hakuna CCM na bila Ma RC ma DC na Ma Ded hakuna kitu kinaitwa CCM. TEHAMA ya CCM imelala hapo.
Mkuu fikra zako ni potofu. Tangu lini taasisi za umma zifanye kazi za vyama.
CCM imewekeza kwenye eneo hilo na azimio hilo lilitangazwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika kikao chake cha Desemba 13,2016.
 
Hiyo ipo kwenye makaratasi tu, ila kivitendo TISS ni idara maalum kwa ajili ya kuilinda ccm na mali zake. Kama unataka kufahamu hili fanya utafiti wa hii idara inavyofanya kazi. Kushindana na CCM lazima uguse vyombo vya ulinzi na usalama hasa usalama na polisi.
Hii ni dhahania tu ya wanafiki wamekuwa wanasema baada ya kushindwa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom