Ni chakula gani hupendi, mimi sipendi ndizi za kupika



asee inabidi mimi unishawishi sana mpaka nile KANDE asee maana dah MAPURE HAPANA NGACHOKA
 
Mimi sipendi mlenda na bamia utaniua ila ujue sitakula haya madude.
 
Huwa sichagui chakula vyote vinapanda ila kuna combo sizikubali
Wali + mboga za majani tu = hii combo inachosha labda kuwe na chai pembeni.
Pilau bila kachumbari = Hapa sijatendewa haki.
Pilau + maharage = sipendi (ntakusanya maharage yote na kuyatupa huko mbali)😀
 
Kusema kweli ndizi nazipenda zilizoiva tu nakula kama tunda ila sio ndizi za kupika.

Ndizi za kupika nakula tu kuzuia kifo panapokua hakuna chakula kingine.

Katika chakula nisichokipenda zaidi Duniani ni ndizi za kupika.
Wewe ni lazima ni mngoni..wazee wa kupiga ugali na chai!?
 
Kisamvu na makande...

ingawa makande mengine yanapikwa vizuri hadi nayapenda

na kisamvu nimewahi kula mara moja tu nikapenda

kilipikwa na mwanamke mmoja hivi wa kiarabu kutoka tabora....
Basi vyote wavipenda tatizo hupati wapishi.
 
Mlenda ndo sipendi ile mboga imenishinda kabisa.Vilivyobaki nakula vyote.Makande nayapenda sana hasa nkiyaweka na njugu mawe na karanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…