Ni chakula gani hupendi, mimi sipendi ndizi za kupika

Ni chakula gani hupendi, mimi sipendi ndizi za kupika

Mi sipendi viazi vitamu ,tusamaki twa ajabu ajabu sili
 
Viazi mbatata/mviringo zaid ya chips huwa sitaki kuvisikia....tembele weka mbali na mm mana silipendiiii
 
Kusema kweli ndizi nazipenda zilizoiva tu nakula kama tunda ila sio ndizi za kupika.

Ndizi za kupika nakula tu kuzuia kifo panapokua hakuna chakula kingine.

Katika chakula nisichokipenda zaidi Duniani ni ndizi za kupika.
Yaani wewe na mimi sawasawa Mimi sipendi ndizi kabasa zilizo pikwa
 
kuna makande yanapikwa kama pilau achana na hayo maharage yaani ukipikiwa na wataalam kama sisi utahamia.
ujue hakuna chakula kibaya sema ni mapishi na ulle mpangilio wa kula .chakula chochote ukila kila siku unakinai .chakula kilekile mapishi yale yale ndo tatizo la waafrica
Mimi sipendi MAKANDE hata yawekwe nini!!! Nimeshajaribu kuletewa kutoka wapishi mbalimbali lakini YAMENISHINDA! Sipendi makande kabisaaaaaaaa
 
Afunaona watu wanaongea sana wakati ubavu wakukwepa baadhi ya misosi mnayoidis ni midogo. ...mf ugali unaukwepaje bora kande unaeza mwaka ukapita ujala. ..tuache ushabiki usjonatija unaanzaje kuponda chakula ambacho ndio kila siku unakila niujinga
tuusan siyo kweli kuwa ni lazima uwe unakula ugali kila siku. Mimi pamoja na kutopenda makande chakula kinachofuata ambacho sikipendi ni UGALI! Ninaweza kukaa mwaka mzima sijala ugali hasa sembe au dona. Ugali ambao at least naweza kula walau mara 1 au 2 kwa mwezi ni ugali wa muhogo.
 
Ndizi iwe ya kupika au kukaanga haipandi,
makande yale ya kukoboa kwanza mixer maharage hayapandi,labda yale makande ya mahindi mazima mazima ndo yanapanda
 
Kusema kweli ndizi nazipenda zilizoiva tu nakula kama tunda ila sio ndizi za kupika.

Ndizi za kupika nakula tu kuzuia kifo panapokua hakuna chakula kingine.

Katika chakula nisichokipenda zaidi Duniani ni ndizi za kupika.
Wewe ni KE au ME?
Huu Uzi unawafaa zaidi akina Miss Natafuta, Miss Chagga, Farkhina n.k.
 
Nilipokuwa mdogo nilikuwa sipendi sukari na ndizi sasa sipendi wali kabisa hata uwe na mboga gani napenda ugali na samaki au na nyama mboga za majani nakula kwa vile najua umuhimu wake na kwa kuwa ndio ninachomudu kupata
 
mi kwangu hakijwahi kua chakula kabisa!ila nimewahi kula pale hali ilipolazimisha nile....ila kwakweli kam ni mara moja mbili tu,BORA KUSHINDA NJAA KULIKO NDIZI ZA KUPIKA!!!
 
Back
Top Bottom