Wasalam,kuna wimbi la dawa nyingi za meno zinauzwa. Naomba kufahamishwa dawa nzuri kwa matumizi,N.B uzi huu sio kupromote dawa ni kupata
Dawa Za Meno zina kemikali zisizopungua 9 kama zifuatazo ..;
1. Triclosan
2. Sodium Lauryl Sulfate (SLS)
3. Fluoride kama NaF, SnF2, MFP
4. Diethanolamine (DEA)
5. Propylene Glycol
6. Titanium Dioxide (TiO2)
7. Artificial Sweeteners (e.g., Saccharin, Aspartame)
8. Methylparaben
9. Sodium benzoate
1. Triclosan
Triclosan Ni kemikali ambayo hutengenezwa kwa mmeyuko wa kemikali unaoitwa
chlorination ya anisole (ambayo imeunganishwa na phenol) kwa kutumia chlorine ili kupata 5-chloro-2-(2,4-dichlorophenoxy)phenol โ ambayo ndiyo triclosan..!!
Kemikali hii utaipata kwenye
Dawa za Meno , Sabuni za mikono na mwili, Deodorant, Vipodozi, Dawa ya kusafishia sakafu na vifaa vya hospitali
TUANGALIE MADHARA YAKE KWA MWANADAMU
Kwenye Dawa za Meno wamekuambia kabisa Tumia ila usimeze ,Na kwa kawaida huwez kuingiza kitu kinywa halafu usimeze !!!!
Yafuatayo ni Madhara Yanayosababishwa na Kemikali ya
Triclosan
1. Huathiri homoni mwilini kwa Huathiri mfumo wa endocrine, hasa homoni za uzazi
2. Hufanya bacteria wabaya kuwa wagumu kutibika au kusikia dawa yeyote
3. Huathiri Ini
5. Inaweza kusababisha mzio Hasa kwenye ngozi au kupumua.
2. Fluoride kama NaF, SnF2, MFP
Fluoride ni kiungo muhimu kwenye dawa za meno lakini ni moja ya kiungo kinachovuruga kuzalishwa kwa homoni ya melatonin. Melatonin ndiyo inaratibu usingizi...
Mvurugiko huu unasababisha kukosa usingizi. Kadiri unavyokosa usingizi tarajia kupoteza nguvu za kiume kama ninlwa kiume na nguvu za kike kama ni wa kike ...
Mzunguko mkubwa wa fluoride kwenye mfumo wako wa damu unaathiri utendaji kazi wa kongosho kuratibu insulin.
Insulin inaratibu kiwango cha sukari kwenye damu. Tafiti zinaonesha kuwa fluoride inaweza kuvuruga uzalishwaji wa insulin na kuongeza hatari ya kisukari...
Hatari mojawapo ya kisukari ni kupoteza nguvu za kiume na za kike ( Hormon kuvurugika) ....
Hapo sijataka kwenda upande wa Pituitary Gland - hili ndiyo taa ya mwili. Ikitetereka kila kitu kinaharibika...
Upande wa Sex hormones - Fluoride inavuruga uwiano wa estrogen na testosterone. Hizi homoni mbili zikikosa uwiano sawa, UANAUME au UANAMKE lazima utetereke...
Pia kwa wengine Husababisha madoa meupe au ya kahawia kwenye meno, hasa kwa watoto...
Kwa Wengije Husababisha mifupa kuwa migumu lakini dhaifu na kuvunjika kwa urahisi.
Inapotumika kwa kiwango kikubwa sana kwa wakati mmoja buusababisha kichefuchefu, kutapika, kuhara, maumivu ya tumbo, hata kifo
Huharibu mfumo wa neva (Neurotoxicity) Tafiti zinaonyesha uhusiano kati ya kiwango kikubwa cha fluoride na upungufu wa IQ kwa watoto.
Kusababisha kansa Mara chache sana fluoride inaweza kusababisha saratani ya mifupa (osteosarcoma)
3. Sodium Lauryl Sulfate (SLS)
Madhara yake
๐Kukausha na kuharibu ngozi kwa huvuruga mafuta asilia ya ngozi, na kusababisha ngozi kuwa kavu, kuwasha au kukatika.
๐Inapogusa macho inaweza kusababisha muwasho au hata kuharibu tishu laini za macho, hasa wale wanaochanganya na baadhibya viambata kisha kujipaka usoni au sehemu za mwili
๐Baadhi ya watu hupata vipele, muwasho au uvimbe kutokana na mizio ya SLS.
๐ Inaweza kusababisha mdomo kukauka, vidonda kwenye fizi, au hata kuongezeka kwa hatari ya kupata vidonda vya mdomoni (canker sores)..
Mara chache sana kiwango ni kidogo,SLS inaweza kufyonzwa na kuingia kwenye mfumo wa damu, hasa inapokuwa kwenye ngozi kwa muda mrefu.
KUMBUKA
Kemikali hizi zinaweza kuingia mwilini kupitia kinywa, Lipis za Mdomo, Ngozi na zikaenda kuswbabisha hayo Madhara , Pale Mtumiaji anavyoendelea Kutumia !!!
Mdharau asili hufa kikatili
Muafrika anategemea kila kitu kwa mzungu