Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Nina hoja
Adumu rais wetu ajaye ambaye ni Tundu Antipas Lisu
- Tangu Tundu Antipas Lisu atangaze na kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti taifa wa CHADEMA. Watanzania karibia wote wamekuwa wanafuatilia na hususan kuonesha kumuunga mkono
- CCM imeporomoka umaarufu kwa ghafla mno. Hata mkutano Mkuu unaoandaliwa Dodoma umekosa shamsham zake kama ilivyo ada. CCM imepeleka wasanii wengi mkutanoni lakini hakuna Mtanzania anayefuatilia mkutano huo
- Idadi ya wanaomuunga mkono Lisu inazidi kuongezeka kilakukicha.
- Freeman Mbowe amepoteana kabisa kwa sababu kabla hajachukua fomu ya kugombea uenyekiti CHADEMA Taifa, alipochukua na hata aliporejesha fomu ameshindwa kueleza nini ama maboresho gani atayafanya kwenye nafasi anayogombea.
- CCM imetumia injini zake zote chafu za mitandaoni. Ukisoma maoni ya wanaCCM lialia wamejikita kumpigia kampeni Mbowe huku wakitimiza jukumu lao la kila siku la kisiasa za majitaka dhidi ya Lisu
- Media karibia zote zimejikita kufanya mahojiano na Lisu ambapo amepata nafasi kubwa kuelezea mambo mbalimbali ya kuwafumbua macho na fahamu Watanzania kuhusu nchi yao na haki zao.
Adumu rais wetu ajaye ambaye ni Tundu Antipas Lisu