Ni eneo gani au sehemu gani naweza kuwekeza Tsh. milioni 1 nikapata 5,000 kwa siku?

Ni eneo gani au sehemu gani naweza kuwekeza Tsh. milioni 1 nikapata 5,000 kwa siku?

Unahitaji elf 5 tu huna mambo mengi, huko Tanga sasa sijui kama ipo....ila ungekua mjini katika hiyo milioni chukua laki moja tu pita kwa wafanya biashara wadogo wadogo jioni chukua chenji zao we wape noti, chukua 50,100 na 200.

Nenda vituo vya daladala peleka uuze hizo chenji kila buku unapata sh 100, ukiwa na laki ni elf 10 unarudi zako nyumbani kulala hadi kesho tena
 
Ebu muwe seriously na biashara zingine jamani...

Kweli auze chenji et 😂😂😂😂😂😂
 
Kuna mtu juu huko..
Sitomtaja jina ioa katoa wazo la kuuza chenji kwa mwenzake yaani....

Biashara ya chenji ipo.hvi wakuu
Unapewa buku alafu wewe unampa mia tisa..

🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌
 
Kuna mtu juu huko..
Sitomtaja jina ioa katoa wazo la kuuza chenji kwa mwenzake yaani....

Biashara ya chenji ipo.hvi wakuu
Unapewa buku alafu wewe unampa mia tisa..

🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌
Lazma uidharau we si una duka sinza, full ac full vioo raba kali nne na tshrt nane kodi milioni na nje una ndinga....na huo mzigo uliufata china mwenyewe 😁.

Yes katika buku unapata mia, mia ni kubwa sana kwenye biashara sema we hauwezi elewa akiwa na elf 50 tuuuu anapata hiyo elf tano anayoihitaji kwa siku.

Hii biashara hata hausumbui akili.
 
Biashara inayoweza kuingiza hiyo pesa kwa siku ni ya mikopo
 
Habari wananzengo.

Nina fedha ya kitanzania Tsh 1,000,000/= nataka niiwekeze mahali nipate elfu tano Kwa siku. Nipe mawazo wajumbe lengo langu mtaji upo palepale. Mimi nakuwa muwekezaji yeye anatumia fedha yangu Kama mtaji na kwa siku elfu tano yangu ananitumia
Tuingie ubia mkuu kila siku nakuingizia hiyo 5000 sawa lkn iwe na limit kwa muda gani?
 
acha uongo mm nauza Gas mtaji wangu kabla sijachukua vibali na lesen ulikua laki 5. faida kwa mwezi zaidi ya laki 4 gawanya kwa siku hapi vile vile nina Lipa kwa simu sikosi elf 7 mpk 10 siku nyingin na mtaji laki 8 tu.
Acha kusoma kwa kukurupuka mkuu umeelewa kilichoandikwa hapo au kinakuzidi uwezo? Au ulivyo bongo lala hujui tofauti ya uwekezaji na biashara
 
Mwanangu banda la mpira
Hii biashara ni nzuri Sana hahitaji uwe sijui Barabarani. Ila zinatio hakikisha zile kampuni za kubeti na mabaa yasiwe mengi kwenye location yako.

Maana kampuni za kubeti watu wanaangalia bure na kwenye mabaa.

Ingia uswahilini uswahili huko. Kodi eneo au Banda Kwa bei hisiyozidi 50,000. Nunua dstv na Azam. Flati TV inch hisyopungua 50 au projector.

Weka mabench yako kadhaa na feni kadhaa. Simamia shoo.
Ukishindwa funga camera yako mbele ya Banda. Mechi inaendelea watu wanakula burudani huko Km 300 huko unahesabu tu mapato yako.

Hivi Sasa league ni nyingi kama Uingereza, saud Arabia, Spain, ufaransa league kuu, mabingwa, shirikisho nk.

hugombani na Mtu.
 
Kuna mtu juu huko..
Sitomtaja jina ioa katoa wazo la kuuza chenji kwa mwenzake yaani....

Biashara ya chenji ipo.hvi wakuu
Unapewa buku alafu wewe unampa mia tisa..

🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌
Huo ni uhalifu ..... Hiyo siyo biashara halali ya kifedha ni vile tu Benki kuu wamelala...
 
Naenda mnadani nanunua nyama ya nguruwe kwa 5000 kwa kilo nanunua kilo 100 sawa na laki tano nawauzia wanaokaanga kwa 8000 kwa kilo naingiza faida ya 300,000/ kwa tripu moja nikitoa gharama za usafiri nabaki na 250,000/ kwa wiki naenda mara mbili kwahyo wakika wa laki tano kwa wiki. Laki Tano inayobaki nalangua kuku mnadani kwa 10,000 kwa kuku nachukua kuku 40 sawa na laki 400,000/ nawaleta town nauza kwa 15000 kwa kuku mmoja sawa na faida ya laki 2 kwa tripu kumbuka ninaponunu nyama ndo hapo hapo napo nunua kuku kwahyo nafanya biashara mbili kwa wakati mmoja.
Nipe chimbo hilo
 
So bado hujawa tajiri mkuu kweli
 
Back
Top Bottom