Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Tatzo mungu mwenyewe kajificha sijui anaogopa nn kujitokeza,,!'
 
UTAAHIRA ni pale ambapo unkuta huna hata baisikeli ama guta nyumbani kwako ila unajikamua hadi senti yako ya mwisho kumnunulia 'nabii wako' ndege binafsi!

UZUZU ni pale unapokosa hela ya kumpeleka mwanao shule ila ukijikamua hadi tone la mwisho kuchangia mfuko wa kanisa wa kujenga shule ambayo mwanao haruhusiwi wala kufika langoni mwa shule hiyo!

UJINGA ni pale 'nabii wako' anapokuaminisha kutoishi maisha ya duniani, huku akitusua kila aina ya anasa kwa mabilioni ya hela unazomchangia akikuaminisha kwamba siku utakapokufa ndipo utaenda kuanza maisha ya furaha peponi.

UBAHAU ni pale unapoacha kwenda hospitali ama kumpeleka mgonjwa wako hospitali kwa kuwa 'nabii' kasema usimpeleke wakati yeye hata akiumwa mafua anapanda ndege kwenda India kufanya check up!

cc #Wapendwa wote#
 
Salaaam..

Kwanza kabisa naomba niweke msimamo wangu kiimani, mimi naamini mungu yupo na ndie muweza wa yote.

Turudi kwenye mada..nacho jua mimi adhabu huwa inatolewa ili iwe funzo kwa mkosaji au kwa watu wanao mzunguka huyo mkosaji..adhabu hii huwa ni fundisho kwa mkosaji ili asirudie tena kosa pia ni funzo kwa wengine ili wasifanye kosa hilo.

Haya sasa binadam wote watakao kufa wakiwa na dhambi wameahidiwa moto wa milele kule jehanamu kama adhabu..lakini pia tuna ambiwa kuwa baada ya adhabu hiyo hakuta kuwa na kifo tena wala dhambi na watu watakao kuwa na dhambi watabaki motoni milele..

SWALI:

je adhabu hiyo ya moto itakua ni funzo kwa nan??

Na je ni faida gani mungu ataipata kwa kuwa choma moto viumbe alio waumba mwenyewe..

Je shetani alipangwa ili maisha yawe hivi??

Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu wanadam ambazo chanzo chake ni shetani..je shetani hawezi kudhibitiwa na kupewa adhabu kali kwa kuharibu ulimwengu???maana watu wanajaa kwenye anasa kuliko kwenye nyumba za ibada takatifu..


Nawasilisha..karibuni
Mmh ni mada hataree mi naogopa hasira za mungu
 
Hakuna kitu kama hicho ni nadharia tu ambazo watu kama wewe walizianzisha na kuwaaminisha watu kuwa kuna kuchomwa moto kwa watenda dhambi siku ya mwisho Ili kupunguza madhambi kwa kiasi fulani
Ndugu ka reference please.
 
Atatuchomaje moto na yeye ndio ametuumbia hizo dhambi? Sitakubali.
 
Nashindwa kabisa kupata majibu ya maswali yangu kwa maana. Cha mwisho ninachojibiwa ni kua ninakufuru.. Eeeh Mungu kam kweli upo hebu nipe muongozo kwa mambo yanayonitatiza
 
Mm naamini mwenyezimungu hana kurugenzi ya mawasiliano kama zilivyo ikulu zetu.
Kurugengi ya mawasiliano ya mwenyezimungu ni vitabu vyake tu.
Na wala mwenyezimungu hana msemaji wake hapa duniani kama tulivyo na Haji manara na wengine.
Mwenyezimungu anamiongozo tu ya jinsi gani anataka tuitumie ktk ulimwengu huu miongozo hiyo ni vitabu vyake alivyo tuteremshia yaani Quraan Taurati Injili nk.
Kwaharaka tu jibu lake ni kuwa atafaidika kwa kutimiza ahadi alizo tuahidi waja wema atawapa malipo mema na waovu atawalipa uwovu ikiwemo huo moto.
Mwenyezimungu atuepushe na ghadhabu zake na moto kesho akhera AMEEN;
 
Salaaam..

Kwanza kabisa naomba niweke msimamo wangu kiimani, mimi naamini mungu yupo na ndie muweza wa yote.

Turudi kwenye mada..nacho jua mimi adhabu huwa inatolewa ili iwe funzo kwa mkosaji au kwa watu wanao mzunguka huyo mkosaji..adhabu hii huwa ni fundisho kwa mkosaji ili asirudie tena kosa pia ni funzo kwa wengine ili wasifanye kosa hilo.

Haya sasa binadam wote watakao kufa wakiwa na dhambi wameahidiwa moto wa milele kule jehanamu kama adhabu..lakini pia tuna ambiwa kuwa baada ya adhabu hiyo hakuta kuwa na kifo tena wala dhambi na watu watakao kuwa na dhambi watabaki motoni milele..

SWALI:

je adhabu hiyo ya moto itakua ni funzo kwa nan??

Na je ni faida gani mungu ataipata kwa kuwa choma moto viumbe alio waumba mwenyewe..

Je shetani alipangwa ili maisha yawe hivi??

Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu wanadam ambazo chanzo chake ni shetani..je shetani hawezi kudhibitiwa na kupewa adhabu kali kwa kuharibu ulimwengu???maana watu wanajaa kwenye anasa kuliko kwenye nyumba za ibada takatifu..


Nawasilisha..karibuni
Ukifikiria tu hio pepo ilivyo enyewe nikama inasound as boring place, mko kwenye park mnamuimbia bwanatu, tena mnakaa hapo milele, kweli mtu hatachoka apo
 
Ukifikiria tu hio pepo ilivyo enyewe nikama inasound as boring place, mko kwenye park mnamuimbia bwanatu, tena mnakaa hapo milele, kweli mtu hatachoka apo
Daah..naskia hakunaga kuchoka kule
 
Hakuna kitu kama hicho ni nadharia tu ambazo watu kama wewe walizianzisha na kuwaaminisha watu kuwa kuna kuchomwa moto kwa watenda dhambi siku ya mwisho Ili kupunguza madhambi kwa kiasi fulani
Denis dennny
Wewe nadharia yako ikoje kuhusu mwanadamu nini asili yake, dhumuni la kuwepo hapa duniani na mwisho wake nini na hiyo nadharia yako source yake kutoka wapi na je na credibility hiyo source yako ikoje?
 
Kwenda motoni au uzimani ni chaguo lako wala Mungu hakulazimishi. Kwa upendo wake ametupa uhuru wa ama kutenda mabaya ama mema.. ila kila tutendalo lina malipo yake..
 
Kwani wewe ni nani aliyekwambia kwamba adhabu imewekwa ili ujifunze!?ndugu yangu mawazo ya kibinadamu hayo mungu hayuko hivyo.
You leap what you sow.
Nikirudi kwenye mantic yako ya kibinadamu ya "adhabu ni kujifunza." Kumekuwepo na adhabu aina mbali mbali kwa mfano adhabu kifungo kwenda jela ama kutumikia jamii,adhabu ya viboko adhabu ya kifo nk.
Adhabu ya kifo na adhabu ya kifungo jela labda kufungwa maisha au adhabu ya kifo kwa mfano hivi huyu tenda kosa kosa kuna kitu atajiza kitu chochote?kuna adhabu nyingine zimewekwa ili wengine wajifunzo...katika utawala wa mbingu kuna adhabu moja tu..kwenda Motoni ili sisi tuliobaki duniani tujifunze kwamba ukitenda dhambi stahili yako ni moto tu..Dini nyingine wao wametabainisha na kueleza uzuri wa mbingu kwamba ukitenda mema dunian mbinguni unapewa mabikra 74..kwa mukutadha huohuo ungehoji pia kwanini watu wapewe mabikra sabini!?na kwa manufaa ya nani..!
Acheni uzinzi wizi uasherati wizi nk tuziheshimu na kuishi amri za mungu.
Mungu yupo na adhabu zipo.
You reap what you sow. - This phrase really explains everything. The whole world operates on the principle of cause and effect. Nothing occurs on its own without reason. And all action is bound to have consequent corresponding reaction. If I boil water it will vaporize. If I get agitated, I lose my ability to concentrate and to focus. But there is no such linkage in saying that if I commit sin, I shall have to go through the agony of burning / boiling in cistern after I die.

Once I die my soul no more stays in my body. Burning / boiling body devoid of soul can not cause pain / agony to the soul because it is no more in the body. I stand to be corrected on the position that the soul stays within the body after death. Otherwise we need to interpret what has been said in holy books as refraining note for people inclined to do things not desirable and not to be taken literally.
 
Je, Mungu Atahukumu Watu
kwa Moto wa Mateso?
Je, umewahi kuona mtu akiteswa? Tunatumaini
kwamba hujawahi. Kumtesa mtu kimakusudi ni
jambo lenye kuchukiza sana. Hata hivyo,
namna gani Mungu mwenyewe kumtesa mtu?
Je, kweli anaweza kumtesa mtu? Dini nyingi
zinafundisha kwamba Mungu hufanya hivyo.
Hebu wazia jambo hili lenye kuogofya: Mtu
anakaangwa kwenye kikaangio chenye moto
mkali. Kwa sababu ya maumivu yake makali
analia kwa nguvu sana akiomba ahurumiwe,
lakini hakuna anayemsikiliza. Anazidi kuteswa,
saa baada ya saa, siku nenda siku rudi—
mfululizo!
Hata mtu huyo awe amefanya kosa gani, je,
hungemsikitikia? Vipi yule aliyeagiza ateswe? Je,
kweli ana upendo? Haiwezekani! Mtu mwenye
upendo huwa na huruma naye huwasikitikia
wengine. Baba mwenye upendo anaweza
kuwatia nidhamu watoto wake, lakini hawezi
kamwe kuwatesa!
Hata hivyo, dini nyingi hufundisha kwamba
Mungu huwatesa watenda-dhambi katika moto
wa milele. Tendo hilo linaitwa eti ni hukumu ya
Mungu. Ikiwa ni kweli, ni nani basi
aliyetengeneza mahali hapo pabaya sana pa
mateso ya milele? Na ni nani anayepasa
kulaumiwa kwa sababu ya maumivu makali
ambayo watu wanapata humo? Basi, majibu pia
ni wazi. Ikiwa kuna mahali kama hapo, Mungu
ndiye aliyepatengeneza, naye ndiye anayepasa
kulaumiwa kwa sababu ya mambo
yanayotendeka humo.
Je, unakubaliana na jambo hilo? Biblia
inasema: “Mungu ni upendo.” ( )
Je, Mungu mwenye upendo anaweza kuwatesa
watu kwa njia ambayo hata wanadamu
wenyewe wanaiona kuwa yenye kuchukiza
sana? Haiwezekani!
Fundisho Lisilopatana na Akili
Hata hivyo, watu wengi wanaamini kwamba
waovu wataenda motoni ambapo watateswa
milele. Je, fundisho hilo linapatana na akili?
Mwanadamu anaweza kuishi miaka 70 au 80.
Hata ikiwa mtu alifanya uovu mkubwa sana
maisha yake yote, je, angestahili kuteswa
milele? Hapana. Haingekuwa haki hata kidogo
kumtesa mtu milele kwa sababu ya dhambi
alizofanya katika maisha yake mafupi.
Ni nani anayejua ukweli wa mambo kuhusu
yanayotupata baada ya kufa? Ni Mungu tu
anayeweza kutueleza, naye amefanya hivyo
katika Neno lake lililoandikwa, Biblia,
iliyotangulia kutajwa. Biblia inasema hivi:
“Anavyokufa [mnyama], ndivyo anavyokufa
[mwanadamu]; nao wote wana roho moja . . .
Wote wanaenda mahali pamoja. Wote
wametoka katika mavumbi, nao wote wanarudi
mavumbini.” ( ) Andiko hilo
halitaji moto wa mateso. Wanapokufa,
wanadamu hurudi mavumbini katika hali ya
kutokuwapo.
Ili mtu ateseke, lazima awe na fahamu. Je, wafu
wana fahamu? Hapana. “Walio hai wanajua
kwamba watakufa; lakini wafu, hawajui lolote
kamwe, wala hawana malipo tena, kwa maana
kumbukumbu lao limesahauliwa.” ( )
Basi, wafu ambao “hawajui lolote kamwe,”
hawawezi kupatwa na maumivu makali ya moto
wa mateso.
Fundisho Hatari
Watu fulani hudai kwamba fundisho la moto wa
mateso, liwe ni la kweli au si la kweli, lina
faida. Kwa nini? Wanasema kwamba fundisho
hilo huwazuia watu wasifanye makosa. Je, hilo
ni kweli? Je, kiwango cha uhalifu katika maeneo
ambayo watu wanaamini kwamba kuna moto
wa mateso ni cha chini kuliko katika sehemu
nyingine? Hata! Kusema kweli, fundisho la
moto wa mateso ni fundisho hatari sana. Je,
mtu anayeamini kwamba Mungu anawatesa
watu atayaona mateso kuwa jambo lenye
kuchukiza? Kwa nini aone hivyo? Wale
wanaomwamini mungu mkatili mara nyingi
huwa wakatili kama mungu wao.
Vyovyote vile, mtu anayetumia akili hawezi
kukubali kwamba kuna mahali penye moto wa
mateso. Hilo ni jambo lisilopatana na akili hata
kidogo. Halipatani kamwe na utu wa
kibinadamu. Isitoshe, Neno la Mungu halisemi
kwamba kuna mahali kama hapo. Mtu
anapokufa, “hurudi kwenye udongo wake; siku
hiyo mawazo yake hupotea.”— .
Adhabu ya Dhambi Ni Nini?
Je, hilo linamaanisha kwamba hatuadhibiwi kwa
sababu ya dhambi zetu? Hapana, sivyo ilivyo.
Mungu wetu mtakatifu huwaadhibu watenda-
dhambi, lakini hawatesi. Nao watenda-dhambi
wanapotubu, yeye huwasamehe. Adhabu ya
dhambi ni nini? Biblia inatoa jibu la moja kwa
moja: “Mshahara ambao dhambi hulipa ni
kifo.” ( ) Uhai ni zawadi kutoka
kwa Mungu. Tunapotenda dhambi hatustahili
tena kupata zawadi hiyo, nasi hufa.
Huenda ukauliza: ‘Je, hiyo ni haki kweli? Kwani,
kila mtu hufa!’ Hilo ni kweli kwa sababu sisi
sote ni watenda-dhambi. Kwa kweli, hakuna
yeyote anayestahili kuishi. “Kupitia mtu mmoja
dhambi iliingia katika ulimwengu na kifo
kupitia dhambi, na hivyo kifo kikaenea kwa
watu wote kwa sababu wote walikuwa
wamefanya dhambi.”— .
Huenda kufikia sasa unajiuliza: ‘Ikiwa sisi sote
hutenda dhambi, na kwa hiyo sisi sote hufa,
kuna haja gani ya kujaribu kuwa wema?
Inaonekana kwamba mtu mwovu hutendewa
sawasawa na yule anayejitahidi kumtumikia
Mungu.’ Lakini sivyo ilivyo. Ingawa sisi sote ni
watenda-dhambi, Mungu huwasamehe wale
wanaotubu kikweli na kujaribu kubadili
mwenendo wao. Yeye hutupa thawabu
tunapojitahidi ‘kufanya upya akili zetu’ na
kufanya mema. ( ) Kweli hizo
hutupa tumaini zuri ajabu.
Thawabu kwa Ajili ya Mema
Tunapokufa huwa hatupo tena. Lakini hilo
halimaanishi kwamba huo ndio mwisho wa
mambo yote. Ayubu aliyekuwa mwaminifu
alijua kwamba angeenda kaburini baada ya
kufa. Lakini hebu sikiliza jinsi alivyomwomba
Mungu: “Laiti ungenificha katika Kaburi,
kwamba ungenificha mpaka hasira yako igeuke,
kwamba ungeniwekea kikomo cha wakati na
kunikumbuka! Mtu akifa, je, anaweza kuishi
tena? . . . Wewe utaita, na mimi mwenyewe
nitakujibu.”— .
Ayubu aliamini kwamba ikiwa angekuwa
mwaminifu mpaka wakati wa kufa kwake,
Mungu angemkumbuka na kumfufua. Hivyo
ndivyo watumishi wote wa Mungu wa nyakati
za kale walivyoamini. Yesu mwenyewe
alithibitisha tumaini hilo aliposema hivi: “Saa
inakuja ambayo wale wote waliomo ndani ya
makaburi ya ukumbusho wataisikia sauti yake
na kutoka, wale waliotenda mambo mema
kwenye ufufuo wa uzima, wale waliokuwa na
zoea la kutenda mambo maovu kwenye ufufuo
wa hukumu.”— .
Ufufuo huo utaanza wakati gani? Kulingana na
Biblia, utaanza karibuni sana. Unabii wa Biblia
unaonyesha kwamba katika mwaka wa 1914,
ulimwengu huu uliingia katika “siku za
mwisho.” ( ) Hivi karibuni,
Mungu ataondolea mbali uovu na kuanzisha
ulimwengu mpya chini ya utawala wa
kimbingu. Watu wengi wanauita wakati huo
‘mwisho wa ulimwengu.’—
.
Kisha dunia nzima itakuwa paradiso
inayokaliwa na watu ambao walijitahidi kikweli
kumtumikia Mungu. Watu waovu
hawatateketezwa katika moto, lakini
hawatakuwapo katika Paradiso inayokuja.
Katika , tunasoma hivi: “Mtu
mwovu hatakuwako tena; nawe hakika
utapaangalia mahali pake, naye hatakuwapo.
Bali wapole wataimiliki dunia, nao watapata
furaha yao tele katika wingi wa amani.”
Je, hayo yote ni ndoto tu? Hapana, ni ahadi ya
Mungu. Katika Biblia tunasoma hivi: “Ndipo
nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha
ufalme ikisema: ‘Tazama! Hema la Mungu liko
pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao,
nao watakuwa watu wake. Na Mungu
mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta
kila chozi kutoka katika macho yao, na kifo
hakitakuwapo tena, wala maombolezo wala
kilio wala maumivu hayatakuwapo
tena. Mambo ya zamani yamepitilia mbali.’”—
.
Je, unaamini maneno hayo? Unapaswa
kuyaamini. Neno la Mungu hutimia sikuzote.
( ) Tunakuhimiza ujifunze mengi
zaidi kuhusu kusudi la Mungu kwa ajili ya
wanadamu. Mashahidi wa Yehova watafurahi
kukusaidia. Ikiwa ungependa wakusaidie,
tafadhali waandikie ukitumia mojawapo ya
anwani zilizo hapa chini.
Isipokuwa imeonyeshwa vingine, Maandiko
yote yamenukuliwa kutoka katika Biblia
Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya.
SOURCE. Mashahidi wa YEHOVA tembea JW.ORG PIA UNAWEZA OMBA UFUNDISHWE BIBLIA NI BURE
 
Soka Malaki 4 Biblia inasema waovu wataangamia na kuwa majivu na kisha dunia itaumbwa upya na watakatifu wataishi humo bila dhambi. Faida aipatayo Mungu ni kuteketeza dhambi, kwa kuwa shetani na wafuasi wake wameng'ang'ania dhambi licha ya wokovu wa bure kupitia kwa Yesu Kristo. Moto wa milele hautawaka siku zote ila huitwa wa milele kwa sababu utateketeza waovu pamoja na shetani na malaika zake watoweke milele. Kama una swali zaidi niulize kuhusu moto wa milele.
 
Atatuchomaje moto na yeye ndio ametuumbia hizo dhambi? Sitakubali.
Hii kitu ipo, kuna watu watagoma kuingia motoni na kumpa lawama zote ibilisi,ibilisi yeye atawajibu kuwa msimlaumu yeye bali zilaumuni nafsi zenu.

Kuna malaika maalum watatumwa kuwashughulikia wale waliogoma kutii amri ya kuingia motoni.
 
Back
Top Bottom