Mungu hapati faida yoyote kwa mtu yeyote kuchomwa moto; nitaeleza hili kwa mifano:
1. unapotupa nyama uliyonunua mwenyewe ukiikuta imeharibika
2. unapochoma takataka zilizotoka ndani ya nyumba yako
3. tunapozika wapendwa wetu waliotutoka
Katika mifano yote hii tunalazzimishwa na hali iliyokikuta kitu chetu tulichokuwa tunakithamini ila sasa kimeharibika, kwa huzuni tunakitupa au kukichoma
umauti uliomkuta mpendwa wetu, kwa huzuni sana tunamzika na kumuacha peke yake sehemu ambayo wakati akiwa hai asingekubali kukaa huko hata ungemuahidi nini!
Mungu anasema nafsi itendayo dhambi itakufa, na kwamba mshahara wa dhambi ni mauti, hivyo basi hali ya mtu kuwa na dhambi ambayo haijaondolewa (unahitaji toba liletalo ondoleo la dhambi), basi Mungu kwa huzuni atakuacha uende jehanam ambayo ni kama dampo la kiroho (uchafu wote huwashwa kwa moto dampo, ambapo moto wake hauzimi)
ili kudhihirisha huzuni ya Mungu, Mungu alimtoa mwanae pekee ili aje, ateswe na kufa kwa ajili ya mwenye dhambi mimi.
Na wewe pia unakaribishwa kama unajua kwamba ni mwenye dhambi (kama mimi) upokee msamaha bure.
YESU ANAKUPENDA