Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Inaonesha humu wapinga mungu wengi walikuwa waumini wa ukristo,kama mtu atachunguza nilichokisema atagundua.
Sasa tatizo lake watu hutumia ukristo kusema hakuna mungu na kuna wenye mashaka na uwepo wa mungu kwa kutumia ukristo huo huo.
 
Hakuna kitu kama hicho ni nadharia tu ambazo watu kama wewe walizianzisha na kuwaaminisha watu kuwa kuna kuchomwa moto kwa watenda dhambi siku ya mwisho Ili kupunguza madhambi kwa kiasi fulani
Inawezekana watu walijifungia ndani wakapika sababu walijua kuna kipindi watawehuka so ili kuwatisha ikabidi kuwe na maandiko kama hayo.
 
Mungu hayupo! Ni mastory ya watu tu wajanja ! Nakuuliza swali: Kama Mungu aliwaumba Adamu na Eva, walikuwa weupe, sasa weusi , wachina, wazungu walitoka wapi? Aliwaumba siku moja, ilikuwaje wakaa kama walivyo sasa hivi! Kwa nini Mungu aliumba bacteria, virus etc wa kumuumiza mwanadamu? Aliwaumba lini na tunaambiwa aliumba vitu vya kumsaidia mwanadamu! Maswali ni mengi ukiyatafakari unaambiwa UNAKUFURU ili usidaisi
NB: Bacteria na virusi wametengenezwa na wanadamu...na wala usimsingizie Mungu
 
skia mkuu,faida atakayoipata Mungu we wala usitake kujua.utaijua hyo siku ikifika.cha muhumu we ishi alivyo kuagiza
 
Ulishawahi kujiuliza Mungu ni kitu gani? Kiuhalisia Mungu si kiumbe kwa hiyo hana sifa za kiasili kama za viumbe mithili ya binadam.
 
Swali kama hilo Mussa aliwahi kumuulza mungu na mungu akamwambia Mussa alime nafaka.Baada yakulima nakuvuna akachuku ngano nzuri na yale mabaki Musa akayachoma moto.mungu akamwambia musa kwann umechoma moto hayo mabaki.Musa akajibu kuwa hayana faida na hapo mungu akamwambia umepata jibu lako sasa ni kwanini na mm nawachoma wale wote wasiokua na faida kwangu.
 
Kwani ni faida gani wanayopata watu wanapomkamata mwizi na kumpa kipigo?
Tujihoji kwanza hili dogo kwanza
 
Unajua sio kila jambo tuna mamlaka nalo?unajua maana ya theocracy?
 
Maelezo ya kwenye hizo link yanaongeza maswali zaidi.
Orodhesha hayo maswali zaidi uliyoyabuni baada ya kupitia maelezo ya kwenye hizo link kama kweli ulipata muda wa kusoma kilichoandikwa kwenye hizo link.
Kwa uzoefu ni kawaida ya kwa watu wasiopenda kuishirikisha akili kuandika visingizio kama hiki "napata maswali zaidi".
Weka hayo maswali zaidi uliyoyapata, watatokea walio na majibu ya maswali yako. Andika maswali yako ili tunufaike sote pale yatakapojibiwa.
Hii ichukulie ni changamoto kwako. Itathibitisha kwamba umesoma kwenye link na umejaribu kuelewa.
 
Kweli shetani hajalala, bado anazungukazunguka amtafute mtu ammeze, na kwa humu jf ashameza wengi aiseeeeee.
 
Kwani hakimu anapotoa hukumu anapata faida gani? Au anapata hasara gani?

Vivyo hivyo kwa Mungu, hapati faida wala hasara yeyote ..faida na hasara zitakuwa juu yako.
 
Mungu wako alivyokuumba hakukuacha hivihivi bali alikuwekea sheria ili uzifuate,piq akakupa akili iliuwezekubaini "jema" na "ovu" jema ulifanye ovu uliache, miongoni mwatofauti kati mnyama na binadamu ni "akili".
Atakaye puuza sheria za mungu hapa duniani atapelekea kupata adhabu kwawote au yeye binafsi..adhabu hiyo huwa nikwaajiri yakukanya ie ilimkosaji arejee kwamungu wake asirudie tena. Pia kuna mambo mengi ambayo yapo ndani yauwezo wa mungu yanatokea ilikuwafanya wanadamu kurejea nakuacha maovu mfano, matetemeko, vifo, kupatwa kwamwezi au jua n.k, yote hayo hutokea ilikuwarudisha watu kwamungu nawamuabudu yeye tu.

Baada yakufa ndo kuna adhabu yamilele kwakuwa ulishapewa sheria namaonyo mengi ulipokuwa duniani, pia ukapewa masikio iliusikize sheria za mungu naukapewa akili iliuweze kuamua kufanya mema au maovu uliyoyasikia.
Nihuruma kiasi gani alionao mungu wako kwakupa chance yakujiuliza namaonyo ukiwa duniani??
Kwahiyo baada yakifo niwakat wahesab kwauliyoyafanya nakuonywa duniani, mema yako yatakuweka peponi namaovu yako yatakuweka motoni.

##yeye mungu,akikutia motoni au peponi hapungukiwi chochote##
 
Back
Top Bottom