Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Mchungaji wangu siku 1 aliniambia ( Kuna mambo mengine yaache kama yalivyo )
Kama jambo halijaandikwa kwenye biblia au kufunuliwa na roho mtakatifu ni ngumu kama mwanadamu kutoa jibu.Mchungaji wako alivyokujibu naamini alibase kwenye KumbukumbulaTorati 29:29 .Lakini kama kuna jambo linakusumbua na hulijui unaweza mwomba Mungu akufahamishe,tatizo lililopo kwa waamini wa siku hizi tunataka majibu kwa tusiyoyajua lakini hatuko tayari kuingia gharama kwa maana ya kufunga na kumwomba Mungu atujuze.
 
Bad enough tunasoma katika vitabu vya dini kwamba mamlaka ya Mungu ni ya juu sana na haihojiwi na chombo kingine chochote, ila nadhani kwamba wakati Mungu anatoa tamko lake hili alilitoa kwa ghadhabu na wala hakuangalia side effects zake!
Mkuu naomba andiko ili na mimi nijifunze kuhusu hayo uliyoandika kama yapo kweli.
 
Kabla hujajibiwa, na wewe jiulize kunafaida gani ya kutenda dhambi?
 
Binaadamu tunajitahidi kuhoji vitu visivyo tuhusu.
Faida anayoipata mungu ww binadam wataka kuijua ya nn?
Mm nakushauri Fanya yale unayoamin yanampendeza mungu wako utaepuka huo moto.

Lakini ukumbuke kuwa huo moto sio adhabu bali ni hukumu yaweza kuwa Na mwisho au isiwe Na mwisho

Kumbe unatenda mema sababu unaogopa moto?Basi wewe ni kama roboti,hujui unachokifanya

Fanya mema because it is a right way to do and live....Ukitenda mema na wewe mtenda mema unafaidika....ni ubinadamu kutenda mema,and it feels good

Ushenzi wa eti unatenda mema sababu unaogopa eti kuna moto is too feeble and childish...
 
Kumbe unatenda mema sababu unaogopa moto?Basi wewe ni kama roboti,hujui unachokifanya

Fanya mema because it is a right way to do and live....Ukitenda mema na wewe mtenda mema unafaidika....ni ubinadamu kutenda mema,and it feels good

Ushenzi wa eti unatenda mema sababu unaogopa eti kuna moto is too feeble and childish...
Noted
 
Hapo hapo kipindi cha gharika walioingia kwenye safina viumbe vyote binadamu, wanyama, wadudu mimea vilikuwa safi yaani hakukuwa na dhambi swali linakuja ilitoka dhambi na uovu ulitoka wap baada ya gharika
 
Ee bwana mimi ni nani hadhi nihoji mawazo yako?
Naomba unisemehe bure[emoji120]
 
Wewe sio wa kwanza kuzikataa/kupinga..
Walikuwepo waliopinga kinadharia kamaa ww.
Mwisho wa siku walipotea kinadharia.
Cha kufurahisha ni kwamba Mungu katupa zawadi nzuri ambayo hawezi kutunyang'anya..
Zawadi ya uhuru wa kuchagua..Ukiwa hai.
Unaweza ukachagua kumkubali au kumpinga kwa namna yeyote ile kama ww ufanyavyo.
Ku mwamini au kutokumwamini.
MUNGU SI DICTATOR.
Hata ukimtukana matusi makubwa makubwa au ya kinadharia.
Sawa tu.

LKN
Katika yote hayo..Siku utakapokuwa mbele yake.
Maneno yako hayatabadilisha kitu..
Kwamba ulikuwa huamini..
uliamini ni nadharia ya watu..hayata saidia kitu.
Kilio na machozi yako..haya badiliaha msimamo wake.

Neno moja kwako.
Mungu anakupenda.
Mlango uko wazi,bado nafasi unayo kwa sasa anaweza akakusamehe..akakufanya kuwa mwana wake
Acha kukutisha, jibu hoja!
 
Mungu mwenyewe hapendi wanadamu waangamie bali wafikirie toba. Jehanam iliweka kwa ajilu ya Ibilisi na Malaika wake. Binadamu kwa ukaidi wetu na jeuri zetu tunaikataa nuru na kuenenda katika giza. Kwa hiyo si suala la kuuliza faida apatayo Mungu wakati tumeshapewa option sahihi kuepuja moto wa milele

Hakuna moto hiyo ni biblia gani umesoma
 
Uwongo Unaomfanya Mungu Aonekane Kuwa Mkatili



MAONI YA WATU WENGI
“Punde tu baada ya kifo nafsi za watu wanaokufa wakiwa watenda dhambi zinaenda motoni, ambako zinateseka milele.” (Catechism of the Catholic Church) Baadhi ya viongozi wa kidini wanasema kwamba mtu akifa anatengwa kabisa na Mungu.
UKWELI WA BIBLIA
“Nafsi inayotenda dhambi—hiyo yenyewe itakufa.” (Ezekieli 18:4) Wafu “hawajui lolote kamwe.” (Mhubiri 9:5) Ikiwa nafsi inayokufa haijui lolote inawezaje kuteseka kwenye “moto wa mateso”?
Katika Biblia neno ambalo hutafsiriwa “kuzimu” kihalisi linarejelea kaburi la watu wote. Kwa mfano, Ayubu alipopatwa na ugonjwa mbaya sana, alisali hivi: “Laiti ungenificha kuzimuni.” (Ayubu 14:13, Biblia Habari Njema) Ayubu alitaka kupumzika kaburini na si mahali penye mateso.
KWA NINI NI MUHIMU?
Ikiwa Mungu ni mkatili hatuwezi kumpenda, tutamchukia. “Tangu nikiwa mtoto nilifundishwa kuhusu moto wa mateso,” anasema Rocío, anayeishi Mexico. “Niliogopa sana na kudhani Mungu ni mkatili. Nilifikiri kwamba alikuwa mwenye hasira na asiye na upendo.”
Rocío alibadili maoni yake kumwelekea Mungu aliposoma katika Biblia kuhusu hukumu za Mungu na hali ya wafu. Anasema, “Nilijihisi huru—ni kama nilikuwa nimeondolewa mzigo mkubwa wa kihisia. Nilianza kuamini kwamba Mungu anataka tufanikiwe, anatupenda, na ninaweza kumpenda. Yeye ni kama baba anayewapenda na kuwajali watoto wake.”—Isaya 41:13.
Watu wengi wamejitahidi kumcha Mungu kwa sababu wanaogopa kuteswa motoni, hata hivyo, Mungu hataki umtumikie kwa sababu unamwogopa. Badala yake, Yesu alisema hivi: “Lazima umpende Yehova Mungu wako.” (Marko 12:29, 30) Zaidi ya hayo, tukiwa na uhakika kwamba Mungu anatenda kwa haki sasa, tunaweza kutazamia kwamba atahukumu kwa haki wakati ujao. Kama Elihu, rafiki ya Ayubu, tunaweza kusema: “Hasha, Mungu wa kweli asitende kwa uovu, na Mweza-Yote kutenda isivyo haki!”—Ayubu 34:10.
 
Back
Top Bottom