Ni furaha iliyoje kurejea nyumbani baada ya kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu?

Ni furaha iliyoje kurejea nyumbani baada ya kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu?

Ni takribani miaka 15 tangu nimeondoka nchini na kwenda kutafuta fursa katika nchi za wazungu. Ni katika harakati za binadamu kutafuta rasilimali za kuboresha maisha yake na ya watu wengine wanaomzunguka. Hivyo mimi si wa kwanza na sitakuwa wa mwisho. Hata muda huu ninavyoandika airport, bus stands na bandari zimejaa kuwasafirisha watu wanaokwenda sehemu mbali mbali za dunia.

Nilikuwa na shauku kubwa sana tangu nimeanza kupanga safari ya kurudi nyumbani. Playlist yangu ilijaa nyimbo za kunihamasisha kurudi nyumbani. Kila siku nilicheza nyimbo kama ya OLIVER ANTHONY ya I WANT TO GO HOME ambayo inasema
Nanukuu:
‘Cause everyday living in this new world,
Is one too many days to me,
I’m just down on my knees,
Begging Lord, take me home,
I just wanna go home.
It’s been so long,
….I didn’t used to wake up feeling this way,
….And I wanna go home.

Wimbo wa Skylar Grey I’m coming Home
“Still far away, from where I belong,
But it’s always darkest before the dawn,
But I know no matter what it takes,
I’m coming home,
Coming home
Tell the world
I’m coming home .

Nikimalizia na wimbo wa Remmy Ongala wa” I want to go home”.

Narudi Nyumbani, ooh
Nyarudi Nyumbani
Nyumbani ni nyumbani hata kukiwa kubaya.

I want to go home *2
I need to go back home *2
The place that is our home *2
Good or bad still home *2

Kama kawaida ya mwanadamu kuna waliokereka na shauku yangu hiyo na kuna walifurahi pamoja nami. All that I knew was that I just wanted to go back home.

Uzuri wa maisha ni kwamba ukishapanga tarehe tu na Mungu akakujalia neema ya afya basi ujue tarehe hiyo itafika.

Siku hiyo ilikuwa ni ijumaa tarehe 22 Dec 2023. Safari ilikuwa ndefu na shauku ya kurudi nyumbani ilikuwa kubwa. Nilitamani iwe safari ya kufumba na kufumbua nijikute nipo nyumbani. Baada ya masaa mengi angani mwisho wa siku tulifika salama.

Nilipokelewa na joto, nyuso zenye furaha, jiji limechangamka, kelele za kila aina. Masikio yalimiss vitu kama hivi. Nili miss kusikia mziki kila Kona, nyimbo za injili, watu wakihubiri kwa vipaza sauti, watu wakiomba. Nili miss Adhana. Nili miss kelele za ndege, vyura. Kuna mengi nili miss.

Nina furaha sasa nipo nyumbani.
Nipo na ndugu zangu
Nipo na rafiki zangu
Natembea kwa mguu hadi natoka jasho
Nakula chakula cha shambani kwetu
Nakula samaki wa ziwani kwetu
Nakula kitoweo kutoka zizini kwetu
Nakunywa maziwa kutoka kwa ng’ombe wetu
Nakula mayai kutoka kwa kuku wetu.
Nakula chakula ninachokipenda.

Ninafuraha sasa nimerudi nyumbani
Kushirikiana na ndugu na rafiki zangu
Kuijenga nchi yetu
Kwa nafasi na maarifa tuliyobarikiwa.

Nyumbani ni nyumbani.

Naipenda sana nchi yangu Tanzania
🇹🇿
Krb sn ngosha!
 
Attachments

  • IMG-20240108-WA0034.jpg
    IMG-20240108-WA0034.jpg
    127.9 KB · Views: 7
Una akili za kitumwa,no matter what, you will never be a King in a Foreign country!!
Kwani kila mtu anataka kuwa King?

Wengine wanataka ku abolish monarchy.

The opposite of slavery is not necessarily a Kingdom.

The opposite of slavery can be egalitarianism.
 
Funguka mkuu, umetumia mantiki gani kufikia hitimisho hili?
Imagine mtu kaamua tu kuelezea furaha yake ya kurejea nyumbani baada ya kukaa nje ya nchi kwa kiaka kadhaa. Comment za baadhi ya watu sasa mara oohh et "ulimbukeni",!!!! Yani mtu aogope kueleza mambo yake kuhofia ataonekana ulimbukeni? Serious??
 
Mimi nashangaa baada ya mrudi kwao kusema kalakiwa na Watanzania wenye furaha, naona watu wanaandika kama vile Tanzania hakuna watu wenye furaha.

Na mtu mwingine kasema mdogo wake karudi Tanzania baada ya kuona upweke Ubelgiji, kuna mtu kasema huyo mtu aliyerudi ni mjinga.
 
Na kuna wengine wanatamani bora wangezaliwa ulaya kama Mbwa au Paka kuliko kuzaliwa kama Binaadamu Africa!!
 
Na kuna wengine wanatamani bora wangezaliwa ulaya kama Mbwa au Paka kuliko kuzaliwa kama Binaadamu Africa!!
Mkuu,

Hatari sana.

Labda huwa wanaangalia vile vijibwa vya Paris Hilton halafu wanavionea wivu wakitamani wangekuwa hivyo vijibwa.

Jana nilikuwa naongea na bidada mmoja, kafiwa na paka wake, akamfanyia uchunguzi kujua kikichomuua. Uchunguzi umemgharimu dola za Kimarekani 250.

Nikasema hapo ushapata bima ya afya ya zaidi ya mwaka kwa Mtanzania.
 
Ni takribani miaka 15 tangu nimeondoka nchini na kwenda kutafuta fursa katika nchi za wazungu. Ni katika harakati za binadamu kutafuta rasilimali za kuboresha maisha yake na ya watu wengine wanaomzunguka. Hivyo mimi si wa kwanza na sitakuwa wa mwisho. Hata muda huu ninavyoandika airport, bus stands na bandari zimejaa kuwasafirisha watu wanaokwenda sehemu mbali mbali za dunia.

Nilikuwa na shauku kubwa sana tangu nimeanza kupanga safari ya kurudi nyumbani. Playlist yangu ilijaa nyimbo za kunihamasisha kurudi nyumbani. Kila siku nilicheza nyimbo kama ya OLIVER ANTHONY ya I WANT TO GO HOME ambayo inasema
Nanukuu:
‘Cause everyday living in this new world,
Is one too many days to me,
I’m just down on my knees,
Begging Lord, take me home,
I just wanna go home.
It’s been so long,
….I didn’t used to wake up feeling this way,
….And I wanna go home.

Wimbo wa Skylar Grey I’m coming Home
“Still far away, from where I belong,
But it’s always darkest before the dawn,
But I know no matter what it takes,
I’m coming home,
Coming home
Tell the world
I’m coming home .

Nikimalizia na wimbo wa Remmy Ongala wa” I want to go home”.

Narudi Nyumbani, ooh
Nyarudi Nyumbani
Nyumbani ni nyumbani hata kukiwa kubaya.

I want to go home *2
I need to go back home *2
The place that is our home *2
Good or bad still home *2

Kama kawaida ya mwanadamu kuna waliokereka na shauku yangu hiyo na kuna walifurahi pamoja nami. All that I knew was that I just wanted to go back home.

Uzuri wa maisha ni kwamba ukishapanga tarehe tu na Mungu akakujalia neema ya afya basi ujue tarehe hiyo itafika.

Siku hiyo ilikuwa ni ijumaa tarehe 22 Dec 2023. Safari ilikuwa ndefu na shauku ya kurudi nyumbani ilikuwa kubwa. Nilitamani iwe safari ya kufumba na kufumbua nijikute nipo nyumbani. Baada ya masaa mengi angani mwisho wa siku tulifika salama.

Nilipokelewa na joto, nyuso zenye furaha, jiji limechangamka, kelele za kila aina. Masikio yalimiss vitu kama hivi. Nili miss kusikia mziki kila Kona, nyimbo za injili, watu wakihubiri kwa vipaza sauti, watu wakiomba. Nili miss Adhana. Nili miss kelele za ndege, vyura. Kuna mengi nili miss.

Nina furaha sasa nipo nyumbani.
Nipo na ndugu zangu
Nipo na rafiki zangu
Natembea kwa mguu hadi natoka jasho
Nakula chakula cha shambani kwetu
Nakula samaki wa ziwani kwetu
Nakula kitoweo kutoka zizini kwetu
Nakunywa maziwa kutoka kwa ng’ombe wetu
Nakula mayai kutoka kwa kuku wetu.
Nakula chakula ninachokipenda.

Ninafuraha sasa nimerudi nyumbani
Kushirikiana na ndugu na rafiki zangu
Kuijenga nchi yetu
Kwa nafasi na maarifa tuliyobarikiwa.

Nyumbani ni nyumbani.

Naipenda sana nchi yangu Tanzania
🇹🇿
Picha
 
Limbukene ni yule anaejitangaza kwenda Ulaya sijui ni kweli au mkwara alafu sijasema members wote wa jamii forum wapo Ulaya kuna wengi Ulaya ila huwezi tukasikia akijitangaza
Na hapo ndipo shida ilipo, kwanini uone kujitangaza kuenda au kuishi ulaya ni vibaya au na wewe ni wale wanaochukizwa na mafanikio ya watu, acheni roho za kimasikini hizo
 
Back
Top Bottom