Ni gari gani huwezi kununua Wala kumshauri mwingine anunue?

Ni gari gani huwezi kununua Wala kumshauri mwingine anunue?

EAPGS

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2021
Posts
282
Reaction score
334
Wana Jf salaam,

Ikiwa ni weekend tulivu kabisa.
Kama tujuavyo, kumiliki gari sasa hivi ni miongoni mwa vitu vya muhimu sana.

Wamiliki wapya wanaongezeka kila kukicha, na kwa bahati mbaya wengi hujikuta wanamiliki magari ambayo baadae yanakuja kuwapa changamoto na kujutia kabisa, hiyo inatokea mara nyingi kama kipato cha mmiliki hakiendani na aina ya gari analomiliki.

Leo tuambiane ukweli, pengine kupitia uzi huu utakuwa msaada kwa mtu au watu kabla ya kufanya maamuzi ya kuingia kwenye dunia ya umiliki wa gari.

Ni gari gani ambayo hauwezi kumshauri mtu kununua na ni kwanini?
 
Nissan Xtrail generation ya kwanza. Binafsi nimemiliki na waliomiliki ambao nipo nao karibu wamepatwa na mauza uza.

Inaweza chemsha isionyeshe kwenye dash, inaweza amua isiwake tu bila sababu ukaita fundi akifika akawasha tu ikawaka na asione tatizo. Unaishia kumlipa usumbufu.

Kuna moja iligoma kuwaka ikashtakia sensor, sensa mpya ikawekwa ikagoma, kila sensor ikiwekwa inagoma ikarudishiwa ya kwake iliyokuwepo mwanzo ikakubali.
 
Back
Top Bottom