1. nissan extrail, hii imeshachangiwa na members wengine humu tayari, cha kuongezea tu ni kwamba hizo nissan wenyewe walitoaga tamko kwama walibugi kwenye hizo gari, kuchemsha hilo gari ni ugonjwa mkubwa, labda ubadilishe rejeta uweke kubwa_modification
2. European cars ambazo hazijathibitshwa na wenyewe, kwamba umenunua kwa third part owners kama sbt, kwa mtu, befoward etc..yaani iwe bmw, volvo, honda etc kama umenunua used kwa mtu basi jua asilimia ya kuwajua mafundi wote hapa mjini ni mkubwa sana, nunua hata ikiwa used iwe imethibitishwa iko okay na authourised European car agent wa hayo magari..itakupa garantii kwamba sensor hazijawa bypassed etc etc engine haijawahi chezewa ili kukunusuru otherwise buy 0 km car.
ukitaka kuthibitisha hili nenda kuna mtaa mmoja hapo mwenge kule karibu na mapambano yamejaa mabmw, nenda kinondoni hananasif mtaa wote umejaa rangerover..au tembelea mitaa ya mbezi beach, makumbusho uone bmw na rangerover zimekuwa mapagale..
3. Daihatsu Terrios/ camry...automatic gear box zake mbovu
4. mazda tribute, hyundai , isuzu trooper, bighon, honda oddesy..hamna spare utachina na hela unayo, litaishia kupaki uwani liwe jumba la panya..spare mpaka nairobi au japan
5. Nissan kwa ujumla: ie terrano, navara.. hazikopeshi hizi gari, hazivumilii watu maskini, ihudumie ikuhudumie, ikose maji tu au oil mlimani inakukaangia engine dakika 0 tu..iwekee shock up og ukiweka za 80k wiki tu unayaingia mashimo mazima mazima.
Pendekezo.
Toyota ndo magari yako made for us, yanavumilia, hata ukiyawekea oil ya boda boda yatakuvumilia..nenda milimani mahenge uko utakua toyota corolla ya mwaka 89 inakilometa laki 6 na inapiga kazi mzee.