Ni haki ipi na uhuru upi ambao viongozi wa upinzani wanatafuta?

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,086
Nina maswali lukuki najiuliza kichwani mwangu nikiwa nimetulia. Kwamba ni haki na uhuru upi. Ni haki ipi na uhuru upi ambao viongozi wa upinzani wanatafuta.

Habari za leo ndugu zangu na marafiki. Kwanza kabisa nianze kwa kusema ndugu zangu siasa sio ugomvi lakini panapo bidi kuulizana lazima tuulizane na tujibizane kwa hoja na sio matusi.

Naomba sasa nilejee kwenye mada. Kwanza kabisa ikumbukwe kwamba Tanzania ilipata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza December 9 mwaka 1961. Kabla ya hapo watanzania hawakuwa na uhuru wala haki yeyote katika utawala huo. Basi tangu December 9 1961 ndipo watanzania walipo ipata haki na uhuru wao mpaka leo hii hivi navyo andika mimi mtanzania nipo huru na naendelea kupiga shughuli zangu kama kawaida kama kawa na nina haki ya kufanya lolote lile popote niendapo katika ardhi ya Tanzania. Ila tu nisivunje sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali yetu.

Sasa basi nirudi kwa Viongozi wa upinzani. Viongozi wa upinzani wanaitafuta Haki ipi na uhuru upi ambao sisi watanzania wa kawaida tumeukosa.

Nahataji kujua
Hawa viongozi wa upinzani wanaitafuta haki ipi na uhuru upi ambayo sisi watanzania wa kawaida tumeikosa.

Au wanatafuta haki na uhuru wao binafsi wa kivyama ili waweze kufanya mambo yao ya kivyama vizuri zaidi.

Mbona sijawai sikia mtanzania wakawaida analalamika huwa amekosa haki wa uhuru. Mbona Uhuru aliutafuta Mwl. Nyerere. Mbona watanzania wa kawaida tupo huru tunafanya shughuli zetu bila wasiwasi na kwa usalama wa hali ya juu.

Hiyo haki wanaitafuta kwa matakwa ya wao wenyewe au ni kwa matakwa ya watanzania?

Kweli kuna mataifa ambayo mimi nimewahi kusafiri ambayo unaweza kusema wananchi wamekosa haki na uhuru. Na unajionea kabisa ni kweli watu hawana haki wala uhuru. Mataifa hayo ni kama Iraq, Iran, Saud Arabia n.k.

Mfano nimewahi kusafiri katika taifa la Saudi Arabia nilishuhudia kabisa jinsi ambavyo watu hawana haki wala uhuru, wanawake hawaruhusiwi kuendesha magari. Na pia kuna mataifa mengine hakuna uhuru wala haki ya kuabudu n. k.
Mbona hapa Tanzania watanzania ukiwaangalia watanzania wa kawaida wote wana uhuru na haki. Wanafanya kila jambo watakalo kufanya wala hakuna wa kuwazuia?

Au wenzetu wanaitafuta haki na uhuru wa kuwatukana viongozi walio madarakani ili vyama vyao vipate kujulikana zaidi kwa wananchi?

Nimesoma civics nimeilewa vizuri sana, lakini hili swala la haki na uhuru unaozungumziwa hapa tunahitaji watanzania tuuelewe na una manufaa gani kwa mwananchi wa kawaida.

Na mtanzania mwaminifu.
 
Uhuru wa kuishi, uhuru wa kutoa maoni bila kubughudhiwa, uhuru wa kuandamana, uhuru wa kuwa na maoni tofauti na watawala, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru dhidi ya watekaji na wauaji. Uhuru wa Bunge kuamua bila shinikizo la rais. Haki katika uchaguzi wa viongozi, haki katika utoaji tenda za sirikali, haki kwa akina mama wanaodhalilishwa na viongozi majukwaani. Haki katika kuasambaza miradi mikubwa ya taifa mikoa yote. Uhuru dhidi ya ubaguzi wa kikabila na teuzi mbali mbali.
 
Kwani hizi haki hazipo Tanzania hii, mbona watanzania hawajasikika wakizilalamikia. Kwamba ninyi ndio mnaziona peke enu au.
 
Haya unayo yasema hayapo Tanzania hii labda unaishi Iraq
 
Acha kujitoa ufahamu mkuu, ina maana hujui hata kusema kuwa Lissu alipigwa risasi na hakuna hata mtuhumiwa alie weza kukamatwa? Azory je?
 
Sasa hayo mambo yanawahusu watanzania wote au ni mambo yao ya kichama na siasa
 
Nina maswali lukuki najiuliza kichwani mwangu nikiwa nimetulia. Kwamba ni haki na uhuru upi. Ni haki ipi na uhuru upi ambao viongozi wa upinzani wanatafuta.

Habari za leo ndugu zangu na marafiki. Kwanza kabisa nianze kwa kusema ndugu zangu siasa sio ugomvi lakini panapo bidi kuulizana lazima tuulizane na tujibizane kwa hoja na sio matusi.

Naomba sasa nilejee kwenye mada. Kwanza kabisa ikumbukwe kwamba Tanzania ilipata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza December 9 mwaka 1961. Kabla ya hapo watanzania hawakuwa na uhuru wala haki yeyote katika utawala huo. Basi tangu December 9 1961 ndipo watanzania walipo ipata haki na uhuru wao mpaka leo hii hivi navyo andika mimi mtanzania nipo huru na naendelea kupiga shughuli zangu kama kawaida kama kawa na nina haki ya kufanya lolote lile popote niendapo katika ardhi ya Tanzania. Ila tu nisivunje sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali yetu.

Sasa basi nirudi kwa Viongozi wa upinzani. Viongozi wa upinzani wanaitafuta Haki ipi na uhuru upi ambao sisi watanzania wa kawaida tumeukosa.

Nahataji kujua
Hawa viongozi wa upinzani wanaitafuta haki ipi na uhuru upi ambayo sisi watanzania wa kawaida tumeikosa.

Au wanatafuta haki na uhuru wao binafsi wa kivyama ili waweze kufanya mambo yao ya kivyama vizuri zaidi.

Mbona sijawai sikia mtanzania wakawaida analalamika huwa amekosa haki wa uhuru. Mbona Uhuru aliutafuta Mwl. Nyerere. Mbona watanzania wa kawaida tupo huru tunafanya shughuli zetu bila wasiwasi na kwa usalama wa hali ya juu.

Hiyo haki wanaitafuta kwa matakwa ya wao wenyewe au ni kwa matakwa ya watanzania?

Kweli kuna mataifa ambayo mimi nimewahi kusafiri ambayo unaweza kusema wananchi wamekosa haki na uhuru. Na unajionea kabisa ni kweli watu hawana haki wala uhuru. Mataifa hayo ni kama Iraq, Iran, Saud Arabia n.k.

Mfano nimewahi kusafiri katika taifa la Saudi Arabia nilishuhudia kabisa jinsi ambavyo watu hawana haki wala uhuru, wanawake hawaruhusiwi kuendesha magari. Na pia kuna mataifa mengine hakuna uhuru wala haki ya kuabudu n. k.
Mbona hapa Tanzania watanzania ukiwaangalia watanzania wa kawaida wote wana uhuru na haki. Wanafanya kila jambo watakalo kufanya wala hakuna wa kuwazuia?

Au wenzetu wanaitafuta haki na uhuru wa kuwatukana viongozi walio madarakani ili vyama vyao vipate kujulikana zaidi kwa wananchi?

Nimesoma civics nimeilewa vizuri sana, lakini hili swala la haki na uhuru unaozungumziwa hapa tunahitaji watanzania tuuelewe na una manufaa gani kwa mwananchi wa kawaida.

Na mtanzania mwaminifu.
Kuna Bunge Live?

MTU anasema hakuna mikutano ya siasa mpaka 2020?

Mtu anapigwa risasi 16 mwilini kwa kukosoa serikali mchana kweupe na hakuna MTU anahusishwa hadi leo?

Uhuru wa vyombo vya habari hakuna hadi watu wanavamiwa ofisini na silaha za moto?

Nawafahamu watu wangu na wale maarufu wamebambikiwa case na kunyimwa dhamana kisa wanasema ukweli?

Fatuma karume kafukuzwa kazi kila mahali kisa kusema ukweli?

Mambo ni mengi. Ila kama ni muelewa umepata picha hali ipoje nchini.
 
Kuna watanzania wa aina mbili
watanzania viongozi wanasiasa
Na watanzania wa kawaida
Uliaza na swali la watanzania saiza umekuja na aina ya Watanzania, ok fine. Je Azory yupo kwenye kundi lipi hapo?
Na je kwenye kitambulisho cha taifa kuna hizo aina? Au kwenye passport kuna hizo aina za utanzania?
 
Mkuu wewe umewahi kunyimwa uhuru wa kuhoji kitu gani, na wapi. Umewahi kunyimwa haki ipi.
 
Haya unayo yasema hayapo Tanzania hii labda unaishi Iraq

Kusingekuwa na uhuru na haki hizo, usingepata hata mwanya wa kuchapisha maoni yako haya! Haki na uhuru popote duniani unaendana na wajibu, uzingativu wa sheria, taratibu, miiko, mila na utamaduni, na utambuzi kuwa pale uhuru wako unapoishia, ndipo panapoanzia uhuru wa mwenzio!

Hakuna Uhuru holela; ndio maana, mathalani anayethubutu kumtoa uhai mtoto wake wa kumzaa anachukuliwa hatua hata za kunyongwa akitiwa hatiani, bila ya kujali kuwa mtoto huyo ni wa kwake. Tusipumbazwe na ulaghai wa makuwadi wa mabeberu waliohakikishiwa ukimbizi wa kulipwa ughaibuni!
Hala hala! Mwenyekulitafuta mwenye kulipata!
 
Ndio hivyo mimi nawashangaa wanavyo wadanganya watanzania kwamba wanapifania uhuru
 
Mkuu wewe umewahi kunyimwa uhuru wa kuhoji kitu gani, na wapi. Umewahi kunyimwa haki ipi.
Sio lazima iwe mm mkuu, kama leo ipo kwa jirani kesho itakuwa kwangu.
Na hatuwezi subiri kila mtu afanyiwe kitu ndio tuseme hiki kitu kipo
 
Mkuu sio rahisi sasa mimi hao polisi nipo nao saivi nagonga ulabu tunapiga na stori sasa ndio uniambie hamna haki wala uhuru kweli
 
Kwahiyo ikiwa wewe unakula nao ulabu ndio uthibitisho tosha kuwa hakuna wanacho kidai watu wengine?
Na kwa akiri yako unadhani watu wote wawe na mawazo sawa kama unavyo waza wewe and co?
 
Mimi bado huo uhuru mnadai chief kiukweli bado nashindwa kuulewa yaani hapo Mimi nacho hisi tunawabesha wananchi mzigo wa kudai uhuru na haki isio wahusu.
 
Back
Top Bottom