Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
lipo tatizo kubwa na tatizo dogo; kubwa ni matumizi ya raslimali za serikali kwa ajii ya CCM. Watumishi wanaowahudumia ni wa serikali, vinywaji (I suppose) ni vya serikali n.k Lakini tatizo hili kubwa vile vile linakuja pale ambapo muda wa kazi za serikali unafanywa na kiongozi wa serikali kufanya kazi za chama kwenye jengo la serikali.
Ukubwa wa tatizo hili unaweza kuja hivi zaidi - kiongozi wa chama cha siasa (sema cdm) anaweza kuitisha kikao cha chama kwenye ofisi ya serikali na kikahudumiwa na raslimali za serikali? NIna u hakika mkubwa watu wengi watakataa kuwa haifai lakini tukifuata mfano wa Rais leo (na ameshawahi kufanya hivyo huko nyuma tukazungumza) jibu ni kuwa kuanzia sasa ni ruhusa kwa viongozi wa kisiasa (bila kujali vyama) kufanya vikao na mikutano yao sehemu zao za kazi. hili ni tatizo kubwa.
Tatizo dogo - nani atamwambia Rais ukweli huu kwa sababu hili linawezekana kwa sababu moja tu - anayefanya hivyo ni Rais; kiongozi mwingine hawezi kufanya hivyo akaachiliwa!
Hili linatuleta kwenye swali jingine angavu: je Rais anaongozwa na sheria/taratibu nyingine ambazo zinafuatwa na viongozi wengine wa umma? Do we have another set of laws zinazompa Rais impunity rais ya kufanya lolote?
Mwanakijiji umenena iliyo kweli tupu, tukiendelea kunyamazia huu utovu wa nidhamu wa CCM tujue kinachoendelea sasa ni kisemwacho; "Mazoea hujenga tabia" na sasa yametimia imeshakuwa tabia na wanaona wana haki kuyanya watakavyo. Magamba yameshikamana mno vigumu kuchubuka.